Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,727
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,727 2,000
IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima.

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIO NAO

Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?

Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe

2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?

Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?

Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening.

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE.

Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa.

Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia

5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kadhalika.

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustarehe.

-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

8. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara.

9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi.

10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza

11. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika

13. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
- Maonyesho ya biashara
- Magazeti,
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
- Kwa marafiki.

14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako

SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUPATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA

********

Influenza SAID:
Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii. Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako.

Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara.

Chagua wazo unalolipenda
“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.” Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.

Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa.

Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu
Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.

Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.

Zingatia swala la fedha
Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.

Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.

Angalia uhitaji wa soko
Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.

Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.

Ushindani
Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.

Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza..

Kama nilivyoeleza hapo awali, uchaguzi wa wazo la biashara unahitaji utulivu na umakini mkubwa. Ni muhimu ukahakikisha kuwa wazo unalolichagua unalimudu vyema na linaweza kukupa faida ya uhakika katika eneo unalolilenga.

Usichague wazo kwa kuwa wengine wamelichagua au wengine linawapa faida; bali chagua lile linalokufaa wewe na mazingira yako.
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,727
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,727 2,000
Umesomeka mkuu, Mawazo ya biashara yapo mengi kama ulivyojaribu kuonesha, shida yetu kuu ni mitaji ya uhakika.

Historia haiishiwi wino.
Mkuu ni kweli kabisa kwamba Mitaji ni Tatizo, Ila si kwa kiwango tunacho taka kuaminishwa, wewe kama Entrepreners ni lazima pamoja na mambo mengine uwe na Mbinu za kupata mitaji, na tatizo lina kuwa mitaji kwa sababu tuna penda kufanya biashara kubwa sana kitu ambacho ni ndoto, mtu anataka aingie kwenye biashara na amfikie Mengi au jamaa wa Azam, sio rahisi,

Nchi kama Kenya wapo watu wanoenda hata Kupiga Debe ilimuradi wapate mitaji, wapo wanao enda kufanya vibarua vya kufyeka ilimuradi wapate mitaji, Je ulisha wahi jaribu hivyo na kukosa mtaji? AU unataka mtaji wa Milioni 100?

Tatizo tunataka kuanzia juu wakati wenzetu wote waliaznia chini na kufika hapo walipo sasa ingawa iliwachuku miaka mingi,

so ni vizuri kuanza na ulicho nacho, na kusonga mbele kwa sababu maswala ya mitaji yatakukuta mbele ya safari na si kusibiri mtaji ndo safari ianze, kwa sababu hata kama kuna sehemu Mikopo au mitaji inatolwe wanao pewa kipaumbele wa kwanza ni ambao tiyali walisha anza na si ambao wana mawazo
 

Kamuzu

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
996
Points
225

Kamuzu

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
996 225
@Chasha,

Unaweza kuwa sahihi, shida yangu ni pale unapotafuta mtaji kwa kupiga debe au kibarua cha kufyeka, malipo ya kazi hizo ni madogo sana, sasa ukiondoa matumizi yako ya lazima sijui unabaki na nini kwa ajili ya mtaji. Na hapo hatujazungumzia mtu mwenye familia.

Ninachokiona hapo, kama ni ki`gang`anizi sana basi utafauru kujitengenezea mtaji wa kuuza 'peremende' tu.

Historia haiishiwi wino.
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,727
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,727 2,000
Kamuzu,

Kwama Peremende si Biashaa? Biashara ni kuuza magari na kazalik? wapo walioanza na mafunfu mawili ya Mchicha na kwa sasa hivi wanaongea story zingine kabisa,

Watu tunakosa focus ndo maana unatuona tunauza sigara au pipi stendi miaka nena rudi, ni kukosa focus na si kingine kile

Wachina tunao walalamikia kwmba wanakuja kufanya biashar za uchuuzi si wajinga kabisa, wana tageti mbali sana sisi tunaakia kulaumu wakati kutembeza bidhaa kwnewe hatutaki,

Juzi nilikuata na jama mmoja huku Arusha ametokeakenya na Graduate, anatembeza madawa fulani ya kienyeji mtaani, kwa kukusanya watu na kunaza kuwaelezea madhara ya sijui Soda, na kazalika na mwisho wa siku anawauzia madawa, jamaa nilijaribu kumtafuta baada ya hp kwa kweli alinielezea lengo lake ndoto zake ni zipi,


Kwa kifupi sisi tutabaki kulaumu serikali mara wachina wanakuja kufanya umachinga mara sijui imepanda ikashuka wakati wenzetu wanacheza na furusa

Ok mkuu wewe tafuta mtaji wa mabilioni ili uanze iashara
 

ijoz

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
731
Points
500

ijoz

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
731 500
Nami naomba nichangie kidogo...

Mi nafikiri alichoandika mdau Chasha ni cha kweli. Tusianze kulalamikia mitaji kama excuse. Cha msingi ni kuwa na nia thabiti, ambayo kwayo inatoa nguvu kubwa sana. Ukiwa na nia, unaweza kutafuta mtaji through kupiga debe, kufanya vibarua and the like.

Nilijaribu kuongea na rafiki zangu pale Kariakoo, ambao wanauza maji, ambao walinieleza kuwa ukiondoa mtaji, wanaweza kutengeneza ziada ya Tsh. 12,000-13,000, na siku ya biashara mbaya wanatengeneza ziada ya Tsh. 4000 at minimal.

Aidha, wale akina mama wanaouza matunda nao wana make ziada ya kiasi kama hicho,ambapo wao wanachukua matunda kule Temeke Stereo kwa Tsh.50-70 kwa embe moja,lakini kariakoo wanauza kwa Tsh. 250-300, na kwa juhudi zao matunda haya yanaisha.

Niliozungumza nao wananieleza tayari wameshanunua plots (walianza biashara hiyo miaka mi3 iliyopita). Hawa waliongozwa na nia iliyowapa nguvu ya kusonga mbele, japo vipo vikwazo walivyokutana navyo, nawanavyokutana navyo, lakini wanasonga mbele.

Hivyo,nafikiri mtaji mkubwa aliokuwa nao mtu ni mind set,na mtaji mwingine ni kuwa na mahusiano mema na jamii, ambayo kwayo unaweza pata mawazo mengi mazuri, na inawezekana ukaaminika na mtu/watu w/akakupesha mtaji.

Nawasilisha mchango wangu
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,727
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,727 2,000
ijoz

Ni keli watu wanazania Biashara ni Mitaji mikubwa, Unaweza kabidhiwa Bilon Moja na ukashindwa vibaya sana katika biashara, Biashara sio kuwa na Pesa bali nistrategies,

Ni kweli kabisa hata wale mama Lishe wa miji mikubwa kama Dar na kwingineko wana kuwa wanapata faida za kutosha tatizo kubwa ni kukosa mikakati na Vision za kuweza kuvuka kutoka hapo walipo na kuja kumiliki Migahawa mikubwa, Inawezekana kabisa mama lishe kuja kumiliki migahawa mikubwa kabisa, Ila wanakosa focus that is why unawakuta katia levo moja kwa miaka zaidi ya 20, ambapo ilitakiwa wawe wamegraduate from Small to Medium business
 
Last edited by a moderator:

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Messages
1,395
Points
1,195

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2012
1,395 1,195
Unapoanza kufikiri kua biashara ni mtaji tayari umeshakwama wala usijaribu tena hiyo biashara, Mtaji wa kwanza na muhimu ni wazo la biashara. Niliwahi kupata wasaa wa Mzee Shirima mmiliki wa Precision Air, utastajabu kua wazo la biashara ni zaidi ya mtaji kwani wako wenye mitaji ila wazo lakufanyia biashara mitaji yao halipo. Chanzo kizuri cha mtaji ni kuuza pia wazo la biashara ulilo nalo kwa njia ya ubia ( Partnership)
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,727
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,727 2,000
Unapoanza kufikiri kua biashara ni mtaji tayari umeshakwama wala usijaribu tena hiyo biashara, Mtaji wa kwanza na muhimu ni wazo la biashara. Niliwahi kupata wasaa wa Mzee Shirima mmiliki wa Precision Air, utastajabu kua wazo la biashara ni zaidi ya mtaji kwani wako wenye mitaji ila wazo lakufanyia biashara mitaji yao halipo. Chanzo kizuri cha mtaji ni kuuza pia wazo la biashara ulilo nalo kwa njia ya ubia ( Partnership)
Mkuu ni true kabisa, wazo la Bishara ndo mtaji namba moja na unaweza kuuza wazo, na hata mashindani ya Michanganuo ya biashara moja ya vitu vinayo sisitiziwa ni kuwa na wazo ambalo ni very sound,

Ukiwa napesa kama huna wazo zuri la biashara ni kazi bure,
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,727
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,727 2,000
Safi sana Chasha, Nimesomea Biashara lakini haya sikuwahi kufundishwa, na kweli JF ni zaidi ya Chuo kikuu, ila CHASHA kuna moja ya thread yako baada ya kuiona huku kuna siku nimekuja kuikuta imetoka kwenye Gazetu fulani hivi, na naamini jamaa waliichota humu na kwenda kubandika kwenye Gazeti lao.
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,727
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,727 2,000
Chasha be blessed mkuu..

napenda sana namba 2 na 6.
Ni kweli Mkuu Hoby ya mtu ni moja ya maeneo makuu ya mtu kupata wazo bora kabisa la Biashara, Na inasikitisha sana kwamba unakuta mtu tangia utotoni alikuwa anapenda sana Mfano Kufuga Mbwa lakini leo hii utamkuta ni Askari Magereza,

Na kuhusu Namba 2 napo ni sehemu muhimu sana kwa wazo la biashara na inaweza kuwa ni

1. Mtaani
2. Kazini kwako
3. Kijiji kwako
4. Mtaa jirani na kwako
5. Wilayani kwako
6. Mkaoni kwako
7. Nchi kwa ujumla
8. Nchi Jirani
 

Forum statistics

Threads 1,380,802
Members 525,886
Posts 33,780,269
Top