Baadhi ya mambo machache mazuri kati ya mengi yaliyofanywa na CCM toka mwaka 1977-2015

Nimeona kipaumbele cha kwanza ni kumpiga dadaaa. Haya ongereni.
Swali. Je vyote ulivyoandika vinamsaidia nini mtanganyika wa hali ya chini?
Je vimeongeza idadi ya milo yake kwa siku?
Je vimepunguza gharama za matibabu?
Je gharama za elimu?
Je zimeongeza viwanda nakupunguza wimbi la wasio na kazi?
Je vimemsaidia nini mkulima mdogo wa mazinde na kule mgwashi?

Kutanua uwingi wa mtandao wa barabara za lami kunasaidia kukuza kipato hasa kwa Mtanzania anayejituma. Usifikiri serikali itakuletea fedha nyumbani kwako. Amka mapema katafute mkate wa kila siku uone kama kipato hakitaongezeka.
Ongezeko la vyuo vikuu vinavyozalisha madaktari kwa uwingi vimesaidia Medical Doctors wengi kupelekwa hospitali za wilaya hivyo kupunguza kwa kiwango fulani usumbufu wa wananchi kusafiri hadi miji mikuu kufuata huduma. Miaka ya nyuma ilikuwa kung'oa JINO ni mpaka uende mijini kwenye hospitali za mikoa ili ukmute Dental Surgeon, leo huduma hizo zinapatikana karibia 80% ya hospitali za wilaya.
Zimejengwa sekondari kila kata.....sasa hivi karibia watoto wote wanaomaliza elimu ya msingi wanajiunga sekondari. Miaka ya 90 rudi nyuma sekondari za serikali kila wilaya ilikuwepo sekondari moja ama mbili..Je UONGO? Vipi hali ya sasa.
Penye mazuri muwe mnasema, siyo kushupaa na mabaya tu. Muwe na shukrani.
 
Kwahiyo mnajitekenya na kucheka wenyewe? kama mungekuwa mmetekeleza hayo yote mnahangaika nini na kampeni na kuspend over 100 Million per day kuwalipa wasanii ili mpate nyomi? CCM Out

Wasanii wana haki ya kutumia kodi zao walizolipia serikalini. Wewe hutaki wasanii walipwe? Wangetumiwa bure mngepiga kelele, wanalipwa mnapiga kelele...nyie watu mkoje?
 
Wasanii wana haki ya kutumia kodi zao walizolipia serikalini. Wewe hutaki wasanii walipwe? Wangetumiwa bure mngepiga kelele, wanalipwa mnapiga kelele...nyie watu mkoje?

Mbona kodi hizo hizo hamuwapi walimu, madaktari, manesi, askari ili nao wazitumie maana nao wamezilipa serikalini.
 
miaka 50 unakuja na vitu 13, mnastahili kupumzika
Daraja la mto Malagarasi.....

Kikwete%2BBridge-753512.JPG

90626260.jpg
 
Mbona kodi hizo hizo hamuwapi walimu, madaktari, manesi, askari ili nao wazitumie maana nao wamezilipa serikalini.
Kawaambie madaktari na manesi wakuambie ukweli wakuambie ukweli..mfumo wao wa mshahara ni tofauti na kada zingine zote za serikali.
 
Ni sawa na mtumishi anayelipwa mshahara na marupurupu aliye kabidhiwa dhamana ya fedha na mali za tajiri halafu akachukua hizo mali na kuzitumia na wanawe na kujilimbikizia na kugawana na wageni, huku akimtupia tajiri na wanawe makombo, mabaki na mitumba. Tajiri akilalamika mtumishi anajitapa kwa kazi alizofanya ambazo ni wajibu wake na analipwa na kama hiyo haitoshi anamwambia tajiri aseme asante kwa makombo na mitumba anayopata.

Ccm, tumewapa kodi zetu na dhamana ya kulinda mali asili zetu ili zitufaidie wote, raisi na mawaziri etc wanalipwa kwa kodi zetu ili wafanye hiyo kazi lakini yaliyofanyika hayalingani na thamani ya kodi zetu na utajiri tulionao wa maliasili, na sisi pia tunataka kuishi maisha ya neema kama ninyi na wageni mnavyoishi...
 
ponte_da_unidade.jpg

(2010-05-13) The Presidents of Mozambique and Tanzania, Armando Guebuza and Jakaya Kikwete, on Wednesday inaugurated the "Unity Bridge" over the Rovuma river, making it possible, for the first time, to drive between the two countries.
 
Halafu mnapotoa "ushahidi" humu msisahau asilimia 78 ya watanzania wanaishi vijijini, wamesahaulika wametupwa kiasi kwamba wengine hawajawahi kuona maendeleo kabisa! Wala hawajui maendeleo ni nini...
Inasikitisha sana mnapoleta mapicha ya mjini na madaraja na kujitapa ati ni maendeleo, maendeleo ya nani kwa ajili ya nini?
 
Hapo ni makao makuu ya wilaya ya Mvomero....Je Mvomero ni mjini?
WP_20150924_12_52_06_Pro.jpg
 
Wanao ibeza CCM na kusema miaka 54 haijafanya kitu ni mateja kwa kua wao hawajui wanako toka wala wanapo kwenda wanacho jua ni KUSINZIA na KULALA muda wote ,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mimi nadhani tuanzie na baba zenu na mama zenu kwamba nao tangu wazaliwe hawajafanya kitu ikiwemo kuwazaa nyie wanachadema, kuwatawaza mikojo na vinyesi, kuwanyonyesha, kuwalinda muwe salama nk. Walichofanya wazazi wenu ni kuwafundisha ukosefu wa hekima. Hivi katika hali hii kama hamuoni yaliyofanywa na ccm basi hamuwezi kuona yaliyofanywa na baba na mama zenu na maana yake ni kwamba siyo tu kuwa hamna macho basi hata akili, busara na hekima wenzetu hamna! Hatuwezi kuwapa nchi vichaa
CCM walifanya haya kwa kutumia pesa waliyoipata kwenye biashara gani?yaani wewe unataka kila mtu awe mjinga kama wewe?
 
Halafu mnapotoa "ushahidi" humu msisahau asilimia 78 ya watanzania wanaishi vijijini, wamesahaulika wametupwa kiasi kwamba wengine hawajawahi kuona maendeleo kabisa! Wala hawajui maendeleo ni nini...
Inasikitisha sana mnapoleta mapicha ya mjini na madaraja na kujitapa ati ni maendeleo, maendeleo ya nani kwa ajili ya nini?

Labda kwenu ..katafute picha ya kijiji cha kwenu ya mwaka 1961 alafu utuletee na ya leo ili tuone kama ni kweli pako vile vile
 
Wanao ibeza CCM na kusema miaka 54 haijafanya kitu ni mateja kwa kua wao hawajui wanako toka wala wanapo kwenda wanacho jua ni KUSINZIA na KULALA muda wote ,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Teja ni wewe ambaye hata huwezi pima resources za nchi zilizotumika for 54 year na maendeleo tuliyoyapata.kumbuka Tulawaka tumebaki na mashimo tu,dhahabu ishaisha?Je nini ilikuwa malengo yetu in 54?tumefikia malengo hayo kwa asilimia ngapi?Mkuu think big
 
Halafu mnapotoa "ushahidi" humu msisahau asilimia 78 ya watanzania wanaishi vijijini, wamesahaulika wametupwa kiasi kwamba wengine hawajawahi kuona maendeleo kabisa! Wala hawajui maendeleo ni nini...
Inasikitisha sana mnapoleta mapicha ya mjini na madaraja na kujitapa ati ni maendeleo, maendeleo ya nani kwa ajili ya nini?
Tena bado ni masikini na mafukara wa kutupwa,80% ya watanzania wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku
 
CCM walifanya haya kwa kutumia pesa waliyoipata kwenye biashara gani?yaani wewe unataka kila mtu awe mjinga kama wewe?

Mjinga ni wewe usiyejua nani mjenzi wa nyumba kati ya mnunua matofali na fundi aliyeyapanga matofali hayo hadi nyumba ikatokea. Kwa akili yako unadhani nani aliratibu hadi hayo yaliyotokea yakatokea kama siyo ccm ya akina lowasa na sumaye ambao eti leo wanajitapa kwamba hakuna walichofanya? Kama ccm haikufanya kitu basi sumaye na lowasa nao hawakufanyaga kitu bali walikuwa wanakula bata wa baba na mama zenu kwa mrija pasipo lolote la faida na leo wanataka kumalizia uzee wao pasipo kesi kwani mkishtuka mtawamaliza
 
Back
Top Bottom