COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,598
- 3,644
- Thread starter
- #21
Nimeona kipaumbele cha kwanza ni kumpiga dadaaa. Haya ongereni.
Swali. Je vyote ulivyoandika vinamsaidia nini mtanganyika wa hali ya chini?
Je vimeongeza idadi ya milo yake kwa siku?
Je vimepunguza gharama za matibabu?
Je gharama za elimu?
Je zimeongeza viwanda nakupunguza wimbi la wasio na kazi?
Je vimemsaidia nini mkulima mdogo wa mazinde na kule mgwashi?
Kutanua uwingi wa mtandao wa barabara za lami kunasaidia kukuza kipato hasa kwa Mtanzania anayejituma. Usifikiri serikali itakuletea fedha nyumbani kwako. Amka mapema katafute mkate wa kila siku uone kama kipato hakitaongezeka.
Ongezeko la vyuo vikuu vinavyozalisha madaktari kwa uwingi vimesaidia Medical Doctors wengi kupelekwa hospitali za wilaya hivyo kupunguza kwa kiwango fulani usumbufu wa wananchi kusafiri hadi miji mikuu kufuata huduma. Miaka ya nyuma ilikuwa kung'oa JINO ni mpaka uende mijini kwenye hospitali za mikoa ili ukmute Dental Surgeon, leo huduma hizo zinapatikana karibia 80% ya hospitali za wilaya.
Zimejengwa sekondari kila kata.....sasa hivi karibia watoto wote wanaomaliza elimu ya msingi wanajiunga sekondari. Miaka ya 90 rudi nyuma sekondari za serikali kila wilaya ilikuwepo sekondari moja ama mbili..Je UONGO? Vipi hali ya sasa.
Penye mazuri muwe mnasema, siyo kushupaa na mabaya tu. Muwe na shukrani.