Baadhi ya mambo ambayo Wang Yi atayafanya akiwa katika ziara nchini Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi atafanya ziara hapa nchi Disemba, 7 na 8 mwaka huu.

Ziara hii imekuja mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya simu kati ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Xi Jinping mnamo Disemba 15, 2020.

Mhe. Waziri Yi akiwa hapa nchini atafanya shughuli zifuatazo; atakuwa na mazungumzo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli pia atakuwa na mazungumzo rasmi kati yake na ujumbe wake pamoja na mimi na ujumbe kutoka Tanzania.

Akiwa hapa nchini atazindua Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Wilaya ya Chato ambacho kimejengwa kwa fedha za watanzania ambapo Ukumbi mmoja umepewa jina lake.

Sababu ya kumuomba afungue chuo hicho ni utamaduni wetu wa kumpa heshima mgeni, sambamba na kutambua elimu ya ufundi ilivyopiga hatua huko China.

Aidha, Serikali ya China itajenga Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera ikiwa ni namna ya kufikia lengo la Serikali la kujenga Vyuo vya VETA kila Wilaya hapa nchini.

Siku ya Ijumaa asubuhi Mhe. Waziri Yi atatembelea mwalo wa Chato ili kuona shughuli za uvuvi, ikizingatiwa kuwa ziwa Victoria ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani.

Kati ya masuala ambayo Mawaziri wa Mambo ya Nje tutayazungumza ni pamoja na kupanua wigo wa biashara za Tanzania nchini China, kushiriki maonesho ya biashara ili kukuza bidhaa zetu pamoja uwekezaji katika sekta ya madini.

Tutajadiliana pia kuhusu utoaji wa mikopo pamoja na uzalishaji wa umeme wa maji katika baadhi ya maeneo nchini.

Nchi ya China imepiga hatua kubwa katika suala la teknololojia. Kuhusu utalii tunatarajia mwezi ujao kuanza safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es salaam hadi Guanzhou ili kukuza biashara na utalii.

Ziara hii imetusaidia pia kuwataarifu watu wa China kuhusu hifadhi mpya tano zilizofungulia hivi karibuni ikiwemo ya Burigi, Chato.
 
China ni mshirika wetu tangu nchi hii inapata uhuru.

Historia baina ya nchi hizi mbili ni ndefu na nzuri pia.

Tumekuwa tukishirikiana katika mambo mengi, ya kijamii, kama elimu, afya na pia biashara.

Binafsi nimeshuhudia wanafunzi wa kitanzania wakienda china kupata elimu zao kwa ngazi mbali mbali,

Ipo haja ya kuboresha mahusiano haya kwa manufaa ya wananchi wa mataifa haya mawili.

Karibu Sana Tanzania, Mh. Wang Yi.
 
Majjina ya ukoo ya mchina mafupi huyo Wang Yi jina la ukoo Yi

Jina ia ukoo La kinyakyusa lingekuwa la watanii zangu wanyakyusa lingekuwa refu hilo !!!!!! angeitwa Wang Mwakibumbilegete
 
"#Aidha, Serikali ya China itajenga Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera ikiwa ni namna ya kufikia lengo la Serikali la kujenga Vyuo vya VETA kila Wilaya hapa nchini"

Hiki chuo kikikamilika utasikia kimejengwa kwa fedha za Watanzania!
 
"#Aidha, Serikali ya China itajenga Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera ikiwa ni namna ya kufikia lengo la Serikali la kujenga Vyuo vya VETA kila Wilaya hapa nchini"

Hiki chuo kikikamilika utasikia kimejengwa kwa fedha za Watanzania!
Kwann wajenge hali tunao uwezo wa kujenga vyuo vya veta nchi nzima kila center penye uhitaji.Kama tunanunua ndege cash, SGR cash,mav8 cash tunashindwa vipi kujenga vyuo
 
Magufuli muombe atujengee vyuo vya ufundi/polytechnic colleges..na jinsi anavyotumia ujuzi wa wanafunzi waliohitimu kuinufaisha nchi....
 
Back
Top Bottom