makwagejo
JF-Expert Member
- Nov 25, 2019
- 361
- 267
Licha ya kuwepo kwa zuio la watumishi kutolipwa mishahara kwa kutangaza nia ya kugombea kuna baadhi ya halmashauri kuwalinda wengine na kuendelea kufanya kazi kama kawaida licha ya katibu mkuu kutoa maelekezo ya kutolipwa miezi miwili huku wengine wakiombwa kuandika likizo ya miezi miwili.
Hoja ya kuzuia mishahara hiyo ni kwamba wengine walienda kufanya kampeni huku vyama vya siasa havikuelekeza hivyo,havikuruhusu kampeni ,sasa walifanyaje kampeni ikiwa walitia nia tu na kuchukua form na kuendelea na mchakato kazini?
Fomu za kugombea zilitolewa tarehe 14/07/2020,watumishi walifanya kazi tangu tarehe ya mwisho aa mshahara kutoka hadi tarehe ya kurejesha form,kwa nn wasilipwe stahiki zao?
Hata hivyo kanuni za katibu mkuu na maelekezo ni muhimu kuyazingatia lakini tusiwe na ubaguzi nani atolewe mshahara nani asitolewe mshahara huku wote walikuwa kwenye mchakato mmoja,sheria ina usawa ni vyema sana kuheshimu maelekezo ya katibu mkuu kama kutangaza nia ni kigezo cha kutolipwa mshahara wote tuheshimu maagizo hayo.
Kama hili halitafanyiwa kazi tutataja moja kwa moja halmaahauri husika na orodha zake.