Baadhi ya Halmashauri kuwahifadhi watia nia kwa kutokatwa mshahara, mamlaka husika chunguzeni

makwagejo

JF-Expert Member
Nov 25, 2019
361
267
Licha ya kuwepo kwa zuio la watumishi kutolipwa mishahara kwa kutangaza nia ya kugombea kuna baadhi ya halmashauri kuwalinda wengine na kuendelea kufanya kazi kama kawaida licha ya katibu mkuu kutoa maelekezo ya kutolipwa miezi miwili huku wengine wakiombwa kuandika likizo ya miezi miwili.

Hoja ya kuzuia mishahara hiyo ni kwamba wengine walienda kufanya kampeni huku vyama vya siasa havikuelekeza hivyo,havikuruhusu kampeni ,sasa walifanyaje kampeni ikiwa walitia nia tu na kuchukua form na kuendelea na mchakato kazini?

Fomu za kugombea zilitolewa tarehe 14/07/2020,watumishi walifanya kazi tangu tarehe ya mwisho aa mshahara kutoka hadi tarehe ya kurejesha form,kwa nn wasilipwe stahiki zao?

Hata hivyo kanuni za katibu mkuu na maelekezo ni muhimu kuyazingatia lakini tusiwe na ubaguzi nani atolewe mshahara nani asitolewe mshahara huku wote walikuwa kwenye mchakato mmoja,sheria ina usawa ni vyema sana kuheshimu maelekezo ya katibu mkuu kama kutangaza nia ni kigezo cha kutolipwa mshahara wote tuheshimu maagizo hayo.

Kama hili halitafanyiwa kazi tutataja moja kwa moja halmaahauri husika na orodha zake.
 
Una roho ya kichawi wewe sio bure.
Kwani wakilipwa wewe unapungukiwa nini? Au wakikatwa wewe unaongezewa nini?
Sijui kwa nini sisi Watz ni Kila siku kuomba wenzetu waharibikiwe tuu? Acha roho ya kishetani fanya kazi,bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
 
Usishangae.
Ni pepo mchafu katika ubora wake
 
Licha ya kuwepo kwa zuio la watumishi kutolipwa mishahara kwa kutangaza nia ya kugombea kuna baadhi ya halmashauri kuwalinda wengine na kuendelea kufanya kazi kama kawaida licha ya katibu mkuu kutoa maelekezo ya kutolipwa miezi miwili huku wengine wakiombwa kuandika likizo ya miezi miwili.

Hoja ya kuzuia mishahara hiyo ni kwamba wengine walienda kufanya kampeni huku vyama vya siasa havikuelekeza hivyo,havikuruhusu kampeni ,sasa walifanyaje kampeni ikiwa walitia nia tu na kuchukua form na kuendelea na mchakato kazini?

Fomu za kugombea zilitolewa tarehe 14/07/2020,watumishi walifanya kazi tangu tarehe ya mwisho aa mshahara kutoka hadi tarehe ya kurejesha form,kwa nn wasilipwe stahiki zao?

Hata hivyo kanuni za katibu mkuu na maelekezo ni muhimu kuyazingatia lakini tusiwe na ubaguzi nani atolewe mshahara nani asitolewe mshahara huku wote walikuwa kwenye mchakato mmoja,sheria ina usawa ni vyema sana kuheshimu maelekezo ya katibu mkuu kama kutangaza nia ni kigezo cha kutolipwa mshahara wote tuheshimu maagizo hayo.

Kama hili halitafanyiwa kazi tutataja moja kwa moja halmaahauri husika na orodha zake.
Watu mna roho mbaya.
 
Taja hayo majina ya watia nia na halmashauri zao hapa hapa JF.

Halafu ule mwongozo ulielekeza kuzuia mshahara wa mwezi mmoja tu (July) au miezi miwili (July na August)?
 
Back
Top Bottom