Baadhi ya facts kuhusu nyoka

Baadhi ya facts kuhusu nyoka

Ipi dawa y nyokaa au huduma y kwanza kam tiba Mshana Jr
Mara nyingi kwa nchi zilizo endelea wana anti venom za kila aina wao huwa wanawakamata nyoka hao ambao ni venomous snakes sehemu mbalimbali na ku extract/kuvuna sumu zao kisha wanatengeneza anti venom kwa ku reverse engineering sumu hiyohiyo iwe dawa (antibodies) ya kutibu makali ya aina hiyohiyo ya nyoka aliekuuma....


Kiafrica huku anti venoms sidhani kama zipo mingi na mbaya zaidi hao wenzetu kuna aina ya snakes wanavuna huku huku Africa ila dawa wanatengeneza kwa ajili yao au waje watuuzie..
 
Nyoka aina ya BOOMSLANG
Nyoka barani Afrika ambaye sumu yake husababisha damu yako sio tu kuacha kuganda bali kutoka kwa kila shimo kwenye mwili wako.
📷: Nyoka dume katika mbuga ya wanyama ya Ruaha, TanzaniaView attachment 3305850
Huyu huwakomesha wezi wa maembe juu ya mti. Utaona ni Bora kujiachia udondoke kama jiwe kuliko kushuka taratibu. Huyu sio mkali/mkorofi au Kuanzisha Ligi na binadamu lakini ana mbio sana.
 
Mara nyingi kwa nchi zilizo endelea wana anti venom za kila aina wao huwa wanawakamata nyoka hao ambao ni venomous snakes sehemu mbalimbali na ku extract/kuvuna sumu zao kisha wanatengeneza anti venom kwa ku reverse engineering sumu hiyohiyo iwe dawa (antibodies) ya kutibu makali ya aina hiyohiyo ya nyoka aliekuuma....


Kiafrica huku anti venoms sidhani kama zipo mingi na mbaya zaidi hao wenzetu kuna aina ya snakes wanavuna huku huku Africa ila dawa wanatengeneza kwa ajili yao au waje watuuzie..
Hawana kosa; ni sahihi kwani kuna gharama ya utaalam na vifaa katika kuzitengeneza dawa hizo.
Huku kwetu Africa specific anti venoms sio nyingi ila kuna Universal anti venoms .
 
Nyoka simuamini hata kidogo. Unless amekufa au amefungiwa ndani
 
Ndiyo; na inakuwa ni uonevu mkubwa zaidi pale unapomkuta nyoka yuko porini ( kwenye makazi yake halali)halafu unamwua. Inasikitisha sana.

Nyoka kama black mamba ambaye anasumbua watu bila sababu za msingi nani amemchokoza?

South Africa kwa mfano wanaenda kwenye makazi kutafuta msosi
 
Kwamba nyoka ni muhimu ulishawahi kuishi vijijini na KUSHUHUDIA wanavyoua
Kwa mtizamo wako huo; Je, bunduki, panga na silaha unazozijua sio muhimu? lakini mbona zinaua. Ni ww kuchukua tahadhari ukijua madhara yatokanayo.
 
Nyoka kama black mamba ambaye anasumbua watu bila sababu za msingi nani amemchokoza?

South Africa kwa mfano wanaenda kwenye makazi kutafuta msosi
Nini kilikupeleka kwenye makazi yake? Je, ww mtu usiyemjua akija kwako huku kabeba silaha utatulia na kumkaribisha mkuu?
Ndiyo. Ukiyaweka makazi yako yakawa sio rafiki kwake hatakuja kwako e.g. kuondoa vichaka, Uchafu na makorokoro mengine ili asiweze kujificha humo. Kumbuka nyoka anao maadui wengi sana. Hivyo hujificha sana.
 
Chatu huyo. Yule aliyekomaa analia kama kondoo au jogoo
Sio kweli hata kidogo. Sauti ya nyoka wengi ni ile ya "shshshshs" hissing sound. Wapo wenye kitu mkiani kinachotoa sauti kama mchakacho wa haraka- chrrrp' ...Chrrp' Yote kwa yote sauti ya nyoka lengo huwa ni kutoa 'Onyo" .i.e....Usije hapa; usinikaribie hapa; Tahadhari ondoka...n.k. Ukikaza fuvu anakugonga chap' . Chatu mkubwa hutoa sauti (akichokozwa) inayofanana kwa mbali kama mngurumo wa kupuliza ref. sauti itolewayo na kinyonga) kabla ya kukimbia au kukugonga. "Pbffffffuu.......Pbfffffuu"
Unaweza kuGoogle na ukasikiliza sauti za nyoka aina mbalimbali. Uwe na amani.
 
#FAHAMU Huyu ndio nyoka mwenye kasi zaidi na mwenye sumu kali zaidi duniani,Nyoka huyu ujulikana kama KOBOKO au Black Mamba. hupatikana katika sehemu za Mashariki na Kusini mwa Afrika huishi katika Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu. Nyoka huyu akitaka kufanya shambulio hutanua kinywa chake na shingo yake na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa linatoa upepo. Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa (Neuro) hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni (Cardio-toxin) hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake yanaweza kuua lakini mbali na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, Koboko hana ujanja mbele ya Nguchiro,Mbweha, na Nyegere.
1745071082121.jpg
 
Kaa Mbali na Anaconda Ikiwa Hutaki Kufa

Anaconda si nyoka yeyote tu—ni mojawapo ya nyoka wakubwa na wenye nguvu zaidi Duniani. Anaconda wa kijani kibichi anaweza kukua zaidi ya futi 20 kwa urefu na uzani wa hadi pauni 500 anapatikana katika vinamasi, mito na misitu ya mvua ya Amerika Kusini, haswa Bonde la Amazon. Haitegemei sumu kuua. Badala yake, ni mdhibiti mkuu, akitumia nguvu kamili ya misuli kuponda mawindo yake.

Anaconda hupiga haraka na kimya kimya. Mara tu wanapomshika mnyama—au hata mwanadamu—hufunga miviringo yao minene kuzunguka mwili, wakikandamiza kwa nguvu kwa kila pumzi ambayo mwathiriwa anavuta, hadi kusiwe na hewa iliyobaki. Kifo huja kwa kukosa hewa au kusagwa ndani.

Ingawa mashambulizi kwa wanadamu ni nadra sana, yametokea. Na hebu tuwe waaminifu-huwezi kusimama peke yako ndani ya maji na moja.

Nyoka hawa ni wavumilivu, wenye wizi, na mara nyingi hufichwa chini ya uso wa maji. Kwa hivyo, ikiwa utajikuta katika eneo la anaconda, heshimu pori na uepuke. Huyu si kiumbe wa kumpa changamoto.

Kaa mbali na anaconda—si kwa sababu ni mwovu, bali kwa sababu asili iliifanya kuwa mwindaji kimya na mwenye nguvu.
1745456213679.jpg
 
Hizi story za kibongo kuhusu black mamba nyingi ni zakutunga tu. Mara eti anawika kama jogoo mara anakimbiza mtu. Zote ni uongo mtupu.

Sijakataa kuwa black mamba ni nyoka ambae ni aggressive na hatari lakini kuna chumvi nyingi sana zisizo na uhalisia kuhusu huyu nyoka kwenye soga za wabongo.
Nakubaliana na wewe kwa kiasi....lakini pia kumbuka wabongo ni wakorofi wa asili I mean tangu akiwa mtoto....kuponda nyau au mbwa akiwa amejipumzikia ni suala la kawaida.
So probably hii hulka huipeleka hadi katika viumbe wasiokuwa na maarifa navyo.... that's why utasikia oh hili mara lile kumbe ugomvi kauanza yeye mbongo, koboko wa watu alikua zake amejipumzikia au anatafuta riziki.
 
Yaan katika viumbe siwapendi ni hawa hapa akikuotea tu huponi umekufa maana sumu ya nyoka kupata dawa yake ni ngumu sana maana akishagonga akaenda bila kumuona na kujua ni wa aina gani ndio basi tena ushakufa
 
koboko wa watu alikua zake amejipumzikia au anatafuta riziki
Huyo nyoka ni kichaa ila sio kichaa km wanavyomzungumzia ingawa ni kweli anapenda kulipa kisasi hata kwa mtu ambae hajamchokoza ndio maana nyoka wanapenda kujificha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom