The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 8,551
- 20,346
GT.
Venance alikuwa ni namba sita machachari kweli kweli alikuwa tegemeo kubwa sana la timu yake . Kile kitendo cha kukosa goli la wazi akiwa yeye na golikeeper kimeigharimu timu yake hadi leo.
Namba kumi wao tegemeo alikula umeme hivyo Venance akashikilia dimba, wapinzani walizidisha mashambulizi na kujilinda, lakini katika hali isiyotarajiwa ilipigwa counter attack moja na Venance akajikuta yeye na golikeeper badala ya kufunga goli aliteleza na kuanguka.
Mashabiki walimlaumu sana venance na toka kipindi hicho timu yake imeyumba motisha umepotea kabisa kila mtu anajipigia tu haina tofauti na Manchester united, kila mchezaji mzuri anayesajiliwa ana underperform wamefanya hata rotation ya makocha lakini haijasaidia lolote.
Kilichobaki ni mwekezaji aliyepo kuachia timu apatikane tajiri mwingine huenda akaleta mapinduzi. Mashabiki hawataki kabisa hata kumsikia huyu mwekezaji aliyepo maana anaoneka ameridhika na hana msaada kwa timu.
Kinachomfanya huyu mwekezaji aliyepo azidi kung'ang'ania ni mapato ya timu, Maana pamoja na timu kufanya vibaya ila mapato bado yapo juu kwa sababu ilijijengea jina kubwa. Shinikizo kubwa la mashabiki pekee ndo linaweza kumfanya aachie timu la sivyo mashabiki wasubiri hadi Mkataba wake utakapoisha.