Kuna habari...
Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi ni mgonjwa. Usiku wa kuamkia leo (Sept. 10) amefanyiwa upasuaji wa kichwa katika Hospitali ya Muhimbili (kitengo cha MOI) kuondoa damu iliyokuwa ikivuja kichwani. Operation hiyo imeenda vizuri, na sasa mgonjwa wetu yupo ICU kwa uangalizi zaidi.
Tumuombee ili Mwenyezi Mungu amjalie nguvu, afya njema na uponyaji wa mapema.
******
UPDATES:1730HRS
Dar es Salaam, 10/09/2019, Tunauarifu umma kwamba Jana tarehe 09/09/2019 saa 5 usiku tulimpokea Askofu Mkuu wa Jimbo katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwaichi baada ya kupata huduma katika hospitali ya KCMC.
Baada ya kupokelewa, wataalamu wa MOI walimfanyia uchunguzi na vipimo na kubaini alihitaji upasuaji wa dharura.
Jopo la madaktari bingwa pamoja na Wauguzi wa Taasisi ya MOI walimfanyia upasuaji mkubwa kwa muda wa masaa 3 kuanzia saa 7 usiku hadi saa 10 alfajiri. Upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa.
Baada ya upasuaji hali ya Mhashamu Askofu Ruwaichi inaendelea vyema na bado yuko kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU).
Taasisi ya MOI inawatoa hofu watanzania wote hususani waumini wa kanisa Katoliki kwamba hali ya Mhashamu Askofu Ruwaichi inaendelea vizuri na tumuombee ili aweze kupona mapema na kurejea kwenye majukumu yake ya utumishi.
Imetolewa na - Patrick Vungi
Kitengo cha Uhusiano MO!
*********