Baada ya upasuaji hali ya Mhashamu Askofu Yuda Thadeus Ruwaichi inaendelea vyema. Rais Magufuli afika kumjulia hali

Chiumbe

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
561
816
Kuna habari...

Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi ni mgonjwa. Usiku wa kuamkia leo (Sept. 10) amefanyiwa upasuaji wa kichwa katika Hospitali ya Muhimbili (kitengo cha MOI) kuondoa damu iliyokuwa ikivuja kichwani. Operation hiyo imeenda vizuri, na sasa mgonjwa wetu yupo ICU kwa uangalizi zaidi.

Tumuombee ili Mwenyezi Mungu amjalie nguvu, afya njema na uponyaji wa mapema.
******

UPDATES:1730HRS

Dar es Salaam, 10/09/2019, Tunauarifu umma kwamba Jana tarehe 09/09/2019 saa 5 usiku tulimpokea Askofu Mkuu wa Jimbo katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwaichi baada ya kupata huduma katika hospitali ya KCMC.

Baada ya kupokelewa, wataalamu wa MOI walimfanyia uchunguzi na vipimo na kubaini alihitaji upasuaji wa dharura.

Jopo la madaktari bingwa pamoja na Wauguzi wa Taasisi ya MOI walimfanyia upasuaji mkubwa kwa muda wa masaa 3 kuanzia saa 7 usiku hadi saa 10 alfajiri. Upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa.

Baada ya upasuaji hali ya Mhashamu Askofu Ruwaichi inaendelea vyema na bado yuko kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU).

Taasisi ya MOI inawatoa hofu watanzania wote hususani waumini wa kanisa Katoliki kwamba hali ya Mhashamu Askofu Ruwaichi inaendelea vizuri na tumuombee ili aweze kupona mapema na kurejea kwenye majukumu yake ya utumishi.

Imetolewa na - Patrick Vungi

Kitengo cha Uhusiano MO!

IMG-20190910-WA0037.jpg

*********

89BBE710-9B84-4608-9D35-F3D7ECE5559D.jpeg

2B4A1B8D-7EFE-4FCF-AD6D-EA3D2C87FB1F.jpeg

4CB25342-6594-4473-80DA-9113B4AE0BB1.jpeg
 
Mama Bikira Maria wewe ni ni mama wa msaada, ni kimbilio la wenye shida mama, tazama mama mwanao anateseka kwa maumivu makali, mama tunakulilia tunaomba msaada wako wa maombezi. Kumbuka pale msalabani Yesu alimwambia yule mwanafunzi wake amtazame mama yake, pia ulimwambia mama amtazame mwanae. Tunakuja kwako mama, tunakulilia, msaidie baba Rwaichi apone haraka.

Povu ruksa kwa wale wanaopinga. Ila ndio nishaomba hivyo, na nina amini Mama yetu Bikira Maria atafanya yake na mhashamu atapona soon
 
Tatizo hilo linasababishwa na nini? Au ni ule unga wawasio julijulikana
 
BABA YETU ULIYE ENZINI POKEA MAOMBI YETU , MJAALIE AFYA NJEMA MTUMISHI WAKO. SISI ,PAMOJA WAPENDA MEMA TUNAKUOMBA .AMEN
 
Mama Bikira Maria wewe ni ni mama wa msaada, ni kimbilio la wenye shida mama, tazama mama mwanao anateseka kwa maumivu makali, mama tunakulilia tunaomba msaada wako wa maombezi. Kumbuka pale msalabani Yesu alimwambia yule mwanafunzi wake amtazame mama yake, pia ulimwambia mama amtazame mwanae. Tunakuja kwako mama, tunakulilia, msaidie baba Rwaichi apone haraka.
Povu ruksa kwa wale wanaopinga. Ila ndio nishaomba hivyo, na nina amini Mama yetu Bikira Maria atafanya yake na mhashamu atapona soon
Muombee kwa Yesu au Mungu mama Maria amesha kufa
 
Ngoja nikumwagie povu

Kwahiyo mama maria ndio ana uwezo wa uponyaji zaidi ya Mungu na Yesu Kristo ?

Kumbe Yesu si chochote si lolote
 
Acheni utani ninyi
Tunamuombea kupitia mama bikira maria uponyaji wa haraka.
Mama Bikira Maria wewe ni ni mama wa msaada, ni kimbilio la wenye shida mama, tazama mama mwanao anateseka kwa maumivu makali, mama tunakulilia tunaomba msaada wako wa maombezi. Kumbuka pale msalabani Yesu alimwambia yule mwanafunzi wake amtazame mama yake, pia ulimwambia mama amtazame mwanae. Tunakuja kwako mama, tunakulilia, msaidie baba Rwaichi apone haraka.

Povu ruksa kwa wale wanaopinga. Ila ndio nishaomba hivyo, na nina amini Mama yetu Bikira Maria atafanya yake na mhashamu atapona soon
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom