sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,034
Baada ya kuona kimya, imemlazimu P-Funk aifute tu, huenda ni kuhisi kadharaulika
ila pia huenda WCB hawajafurahishwa na dogo Rapcha kuwashisha mara 2.
Majuzi kazi ya Rapcha Lisa iliachiwa, ikawa trending namba 1 huku ikiipindua video ya Mboso na Baba levo
Hayakupita masaa mengi WCB wakaachia nyingine ya Lavalava na Mbosso ila nayo haikufanikiwa kuipiku kazi ya Rapcha.
Nadhani ni wakati P-Funk ajuehuu mziki wa sasa ushindani ni mkali sana na wasanii kusapotiana imekuwa nadra sio kama zamani.
Ila pia atambue kwamba dogo tumeipenda kazi yake na ndio maana hadi saizi kakamata namba 1 youtube.