Baada ya TEMBO kutembelea UDOM,sasa SIMBA aonekana UDOM Leo

Baada ya TEMBO kutembelea UDOM,sasa SIMBA aonekana UDOM Leo

8e46f63762141835c517ef4cb4b2b50b.jpg
mbona naiona expansion joint hapa
 
dodoma haiishi vituko next day utasikia na kenge kaonekana mkalama wakati ndo makazi yao
 
Huyo simba mimi namfahamu alichaguliwa hapo UDOM amechelewa kuripoti, ila hana noma kabisa kuweni na amani
 
Baada ya Tembo watatu kuvamia UDOM kuwasalimia wanafunzi mwezi wa 7 hatimaye leo jioni SIMBA aonekana UDOM

University of Dodoma

TAARIFA YA HATARI

28th Dec. 2017.
14:21.Pm

Wizara ya Ulinzi, Makazi, Cafeteria, Afya na Mazingira College of Humanities and social Sciences Inapenda kutoa taarifa ya hatari na tahadhali kwa wanafunzi wote Kuwa Kuna Taarifa zilizotufikia hivi punde Za Kuonekana Kwa SIMBA katika college yetu Maeneo ya bonde Linalo tenganisha Bweni za humanities na Jengo la Wizara ya Mambo Ya Ndani. Maarufu kama Kuelekea ujasi mwisho wa barabara ya Reli.

Hivyo nasi Tunaomba Wanafunzi wote Tusionekane Eneo hilo kuanzia sasa mpaka pale tutakapo pata taarifa za usala na utulivu. Wanafunzi waliozoea kwenda ujasi na Wengine waliozoea kukaa kwenye kichaka nyuma ya block 3, 6 na 7 Msiende huko.

Ukipata taarifa hii mfahamishe na mwenzako.

Imetolewa na Juma Amadi.
Waziri wa Ulinzi, Makazi, Cafe na Mazingira.
Hizo ni njia za mababu zao wanyama huwa wanakumbuka hivyo kuweni makini tu na mzoee
 
Back
Top Bottom