Baada ya TEMBO kutembelea UDOM,sasa SIMBA aonekana UDOM Leo

Baada ya TEMBO kutembelea UDOM,sasa SIMBA aonekana UDOM Leo

huyo jirani kaja kusalimia mnamtangaza nchi nzima! siku akitembelea UDSM itakuwaje
 
nadhani hiko chuo ni kiwe moja wapo ya national park,

kwangu mie hio ni fursa ya kufuga wanyama, patengenezwe zoo flani hivi amaizing kama ya pale canada, kisha iwe kivutio kama kwa madiba wanafunzi wasome uhifadhi mazingira na wanyama siasa wawekee pembeni
 
8e46f63762141835c517ef4cb4b2b50b.jpg

hebu tuondolee photoshop hapa.
 
Baada ya Tembo watatu kuvamia UDOM kuwasalimia wanafunzi mwezi wa 7 hatimaye leo jioni SIMBA aonekana UDOM

University of Dodoma

TAARIFA YA HATARI

28th Dec. 2017.
14:21.Pm

Wizara ya Ulinzi, Makazi, Cafeteria, Afya na Mazingira College of Humanities and social Sciences Inapenda kutoa taarifa ya hatari na tahadhali kwa wanafunzi wote Kuwa Kuna Taarifa zilizotufikia hivi punde Za Kuonekana Kwa SIMBA katika college yetu Maeneo ya bonde Linalo tenganisha Bweni za humanities na Jengo la Wizara ya Mambo Ya Ndani. Maarufu kama Kuelekea ujasi mwisho wa barabara ya Reli.

Hivyo nasi Tunaomba Wanafunzi wote Tusionekane Eneo hilo kuanzia sasa mpaka pale tutakapo pata taarifa za usala na utulivu. Wanafunzi waliozoea kwenda ujasi na Wengine waliozoea kukaa kwenye kichaka nyuma ya block 3, 6 na 7 Msiende huko.

Ukipata taarifa hii mfahamishe na mwenzako.

Imetolewa na Juma Amadi.
Waziri wa Ulinzi, Makazi, Cafe na Mazingira.
Mh!

Hawa wanaopenda kukaa kwenye vichaka huwa wanafanya nini huko?

Jamaa wameamua kutishana tu hawa!
 
Amekuja kukagua vijana mnasoma kweli au mnalilia boom tu.Maana kazi ya kutafuta hiyo boom mmewaachia wao wakija kukagua matumizi kelele ooh tumemuona tumemuona!BTW mwambieni Manara aende kumchukua ndg yake
 
Watu wanaamia dodoma na mambo yao yasiyo eleweka eleweka ..soon utasikia kiboko kaonekana
Subiri kuna siku utasikia ameoneka Papa au nyangumi apo Dodoma. Ukiona ivyo, watu wa Dodoma wajipange kisaikolojia kuwa watoto wa uswahilini wanaingia Dodoma. Amani waliokuwa wameizoea itaisha na kitakachofatia nadhani mnawaelewa watoto wa uswahili walivyo na mambo ya Kiswahili
Waganga wa kienyeji wataongezeka kila kona ya Dodoma
 
eboo kumbe simba tu

nchi yetu si ya amani jamani

sasa mbona wanakuwa na khofu ivyo simba hana nouma kabisa
hahaaa nchi yetu ya Amani mbona TLs kapigwa bomba..
hao simba nao akili zao zitakuwa kama hao waliompiga bomba TLs
hawataki mazoea nakuzoena
 
Safi sana photoshop imekubali ila umemkata kucha mrudishie kucha
 
Mimi mwenyewe leo asubuhi nimemuona YANGA katika chuo kikuu cha SAUT hapa Mwanza
 
Back
Top Bottom