Umenikumbusha mbali sana Mkuu.
Nakumbuka mwaka 2011 night kali kwenye saa 7 natoka zangu kwenye sherehe,ghafla kucheki mbele nakutana na mtu kama 10 hivi kila mmoja ana silaha yake,mapanga,nondo,sime,bisibisi na silaha nyingine za kutisha.Sikuuliza,nikaanza kufukua,nao wakaanza kunifukuza.Kilichonisaidia nilikuwa nakimbia huku napiga makelele ya mwiiziii mwiiziii,hapo nikawakata moto,wengine wakawa wanapunguza mwendo,wengine wakawa wanateleza kwenye matope(kilikuwa ni kipindi cha mvua),mpaka nikawaacha wote.
Nimesha-survive sana kwenye matukio kama hayo.
Ila MUNGU mkubwa.