Baada ya Polisi Dar Kufuatilia kifo cha Mercy Mukandara, Mumewe Edward Bukombe akili kumuua

Kuna Jamaa yangu Mkewe kamzingua sana na watoto wadogo wanaomuhitaji Mama yao sana
Jamaa alichofanya ni kutokumfanya chochote Mkewe,kamuacha tu home kutunza watoto,yaani Kama House girl.
What a luck, House girl wako anakuwa Mama wa watoto wako
Safi Kabisa na Jamaa anaishi humo humo
Chumba chake peke, Siku akijisikia kugegeda demu anatafuta Chumba lodge
Safi kabisa
for how long?? bora uondoke kabisa ukaanze upya....how come mnaishi one house mnapishana kama korido za shule.....hamuwezani achaneni....
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Edward Bukombe, aliiambia Nipashe jana kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne saa 11 alfajiri nyumbani kwao maeneo ya Kimara Stop Over.

Alisema wanamshikilia mume wa marehemu kwa sababu inadaiwa ndiye aliyemshambulia kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso na kusababisha kifo chake.

“Ni kweli hilo tukio limetokea Juni 16, mwaka huu huko Kimara na tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mume wa marehemu kwa kumshambulia mke wake, yeye ndiyo chanzo cha kifo chake,” Kamanda alisema.

Mmoja wa majirani (hakupenda jina lake litajwe) alisema aliamshwa na mume wa marehemu usiku wa tukio kuomba msaada.

Alisema mume huyo alidai mke wake, amejigonga kwenye meza na kudondoka chini na kupasuka hivyo kuvuja damu nyingi.

“Tulipofika nyumbani kwao, badala ya mume kuingia ndani alirudi eneo la geti, tulipomuhoji mbona anarudi getini badala ya kuingia ndani, alitueleza anakwenda kutafuta usafiri, hivyo hatukuweza kuingia ndani tuliendelea kusimama nje hadi aliporudi na bodaboda.”

Jirani huyo alidai mume wake alimuhoji mtuhumiwa kama usafiri aliokuja nao mgonjwa anaweza kupanda ndipo alipojibiwa hapana.

“Tulikubaliana aende kutafuta gari na aliondoka na baada ya muda lilikuja gari aina ya Allex na ndipo tulipoingia chumbani kwa msaada wa mwongozo wa msaidizi wa ndani.

“Wakati huo ilikuwa giza umeme ulikuwa hakuna, tulipoingia chumbani tulimkuta Mercy akiwa amelala kitandani akitokwa na damu nyingi eneo la kichwani na alikuwa hajavaa nguo hivyo tulimsitiri kwa khanga ndipo wanaume walimbeba hadi kwenye gari.”

Alisema waliondoka watu watatu ambao ni mume wa marehemu, dereva ambaye ni mdogo wa marehemu na jirani kuelekea hospitali ya Bhoch iliyopo Kimara.

Alisema baada ya muda majira ya saa tisa usiku taarifa zilirudi kuwa vipimo vya daktari vimeonyesha Mercy amefariki dunia.

Mdogo wa mtuhumiwa, Anna Kurwa, alisema kuwa alifika nyumbani kwa kaka yake kuwasalimia na wakati tukio likitokea alikuwa ndani.

“Tulipoingia ndani (chumbani) kwa kweli kile kitendo kilichofanyika pale hapana, dada alikuwa na majeraha kwenye paji la uso na alivuja damu sana.

“Mpaka sasa swali ninalojiuliza ilikuaje na mbaya zaidi hatukusikia kelele yoyote kwamba kuna nini ili tutoke tuangalie kuna shida gani, kiukweli yule dada ameumia na ameteseka sana hadi kufikia umauti.”

Mama mdogo wa marehemu, Aglipina Dominic, alisema mama wa marehemu alimpigia simu kumjulisha kuwa, amepokea taarifa kuwa Mercy kapigwa na shoti ya umeme chumbani kwao.

“Alijulishwa kuwa shoti ilitokea chumbani akakimbilia sebuleni na akajigonga kwenye meza na kupasuka kichwa damu zinamtoka nyingi na wakati anakimbizwa hospitali akafariki dunia,” alisimulia.

Alisema baada ya kufika eneo la tukio walikuta mlango umefungwa na askari walikuwa wameshakuja na baadaye jioni ulipofunguliwa, hali ya sebule walibaini siyo kweli kama walivyosimulia ikilinganishwa na hali waliyoikuta chumbani.

“Zile damu tulizozikuta kwenye shuka, mito ni kama kitendo kingetendeka sebuleni haya makochi tungekuta yamedondokewa na damu nyingi, lakini hatukukuta chochote sebuleni. Wanandoa hawa walifunga ndoa miaka miwili iliyopita,” alisema.

Mama mkubwa wa marehemu, Letisia Kantunzia, alisema Mercy aliwahi kumweleza mdogo wake kuwa, endapo atafariki azikwe upande wa wazazi wake na siyo wa mume wake.

Nipashe
WAnaume wengi na wanawake wa kisasa "wanapenda harusi na siyo ndoa na wanafikir ndoa ni "kufanya sex pekee, kumbe ni zaidi ya hapo
 
tuache jeshi la polisi lifanye kazi yake ya uchunguzi, tusiingize hisia ktk kipindi hiki. uchunguzi utasema kweli, tusitende dhambi ya kudhania.
pole kwa wafiwa kwa kumpoteza mpendwa wao.
 
Watu wanajua ndoa ni kugegedana tu,wanawake wanapenda ndoa mana atavuna zawadi...akifika ndani shida zinaanza,mimi mke alikuja na begi la nguo tu kwangu.
Zawadi zote nlimuambia aache kwao isije niletea mazarua leo mwaka wa 8 heshima debe
 
Mbona mnadharau jeshi la Tanzania hivi, kama haya maelezo ni kweli kuna namna gani mtu anaweza kukwepa kuwajibika?

Jeshi la Tanzania nawaambieni ni makini sana na linafanya kazi kwa weledi sana, na vizuri sana!

Msisumbuke kuhangaika hangaika na kuweweseka, kama mnayosema ni sawa Dada yenu atapata haki yake vizuri sana bila shida!
Hapo ndio shida maana kilichofanyika ni hisia zaidi kabla ya uchunguzi wa jeshi la polisi na mbaya zaidi ndugu wamejigawa pande mbili (wa mwanaume na mwanamke ambao wameungana na majirani na wananzengo wengine maana tayari wametoa conclusion). Waache wazee wazima wafuatilie maana damu pekee kuenea kitandani sio ushahidi pekee maana wanatakiwa waone hata hilo jeraha maana mtu akijigonga inajulikana na akipigwa inajulikana pia maana mambo mengine ya damu kutapakaa huwa hata jeraha la kawaida huwa tunachukua vitambaa hata shati lililo karibu na kutumia kumwekea mtu)

Huyo Housegirl na huyo muuaji anaesadikiwa kutenda kosa hilo ndio wana nafasi ya kusaidia upelelezi na sio wengine
 
Back
Top Bottom