Tunahitaji madaktari wa vichaa Tz, vinginevyo jamii inaelekea pabaya.:A S 13:
Kuna mwanadada mmoja alikuwa anatoa ushuhuda Radio Safina, mh kasema makubwa.
kasema kuwa alikuwa amechukuliwa msukule na waziri mmoja na kazi yake usiku ilikuwa kuwanga, kwenda kuzima, kuua na kunywa damu za watu.
Siku moja akiwa katika mizunguko yake, akapita nyumba moja palikuwa panafanyika maombi, ndo akachanganyikiwa akajistukia anakimbia uchi, ndo watu wakasema mchawi mchawi wakampeka kuombewa. Baada ya hapo akakubali kuokoka na kueleza A to Z. Amesema ameua wajawazito, ameuwa hata wale watoto waliofiwa kwenye kumbi za Disco Dar.
Alikuwa anakaa kwenye Jumba la Waziri mmoja Dar. huyo dada anaendaga kwenyekumbi za disco, anakuwa mzuri na wanaume wanampapatikia. Mwanaume akimchukua kwenda kulala nae, huyo mwanaume anapelekwa kuzimu
Nawaambieni kuwa Mungu yupo, na Anaweza kufanya maajabu. Wanadamu tuache dhambi na kusali.
Mkuu polisi hawawezi kuchunguza mambo ya kishirikina!!Hatuwezi kukimbilia kuwa ana matatizo ya kiafya (kichaa) hadi jopo la Madaktari wa magonjwa ya akili watakapothibitisha.
Kwa vile kasema mwenyewe kuwa aliwahi kuuwa. Polisi inatakiwa kumuhifadhi mahala kwa usalama wake sasa, kisha kuchukuwa maelezo yake kwa kina na kuyachunguza. Ikithibitisha kuwa ana kesi ya kujibu iihusuyo mauaji na kujihusisha na imani za kichawi asogezwe Mahakamani mara moja kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Kwamba alitumwa kuuwa akiwa Msukule na Waziri, hilo la (UCHAWI) ni gumu sana kulithibitisha (beyond reasonable doubt) mahakamani. Hata hivyo maelezo hayo nayo yatafanyiwa kazi kwa kina akiulizwa kuonyesha jinsi alivyokuwa anakutana na huyo Waziri na kupewa maelezo na faida aliyokuwa anaipata huyo Waziri katika kuuwa au hata uthibitisho wowote kuwa huyo Waziri anahusika na hayo Mauaji.
Nasikitika kuwa ikishindikana kuoneka kuhusika kwa Waziri, mtajwa hapa, atakabiliwa na kesi nyingine ya kujibu ya slander per se ambayo itaonekana kuwa anakusudia kumchafua Mh. Waziri kwa sababu anazozifahamu yeye.