Baada ya miaka michache, Dar es Salaam vs Mwanza

Baada ya miaka michache, Dar es Salaam vs Mwanza

mwanza haiwezi ifikia dar hata wakipendelewa vipi haiwezi... kule makao makuu wanapalazimisha ila haiwezekani
 
Fly over Mwanza hakuna uwanja Mkubwa wa ndege Mwanza hakuna barabara za mwendo kasi Mwanza hakuna tena hakuna kabisa kabisa
Ukisema Mwanza hakuna International Airport vilevile useme Dar hakuna flyover za magari. Hivi unafahamu kama uwanja wetu wa ndege umefikia hatua nzuri! Njia ya kurukia ndege tayari ilikuwapo tena ndefu tu 3km saaa wameongeza tena 500m fuatilia zile njia za huko Dar zina urefu upi kama sio 3km tu.

Shida ya uwanja wa Mwanza ilikuwa ni majengo tu ambayo kwa sasa yameshanza kujenga tena yameshafika hatu nzuri kuliko hata hizo flyover zenu.

Kuhusu mabasi ya mwendo kazi hayo si mahitaji ya Mwanza, hakuna mtu anayeshindwa kufika mahari kwa kukosa usafiri. Pia hatuhitaji flyover kama mnazojengewa huko Tazara na Ubungo jiographia ya Mwanza ni tofauti na huko Dar.
846297580821a5d349c30f2de13d1955.jpg
 
Nawachora tu Wale wakuja dar ndo uwa wana mdomo Sana kuliko si wazawa turieni basi mbna wazawa tumetulia zetu tu... [emoji23][emoji23][emoji23]kuji kuta wa dar akati niwa Kuja afu na nyie wa mwanza vungeni bac nyie bado Sana mtaendelea kua wa pili nyuma yetu
 
kwa hiyo mnahitaji zipi kama si hizo za Tazara na Ubungo!
Tunahitaji hizi flyover za waenda kwa miguu ambazo tumeshajengewa, pia barabara za rami na za mawe mitaani ambazo nazo si haba zinajengwa na halmashauri licha ya chama kinacho tawala hapa kuwa ni kile cha majizi, na yanaiba kweli kweli hasa yale ya kuja, mazee ya kuteuliwa.
Mwanza tunachukiwa bule, haya majizi hatukuyapigia kura hapa mjini ila yalijitangaza tu kwanguvu na sasa yanafanya juu chini kudanganya umma eti yanapendwa, ni uongo.
 
Wasukuma mmeanza Kutuchokoza tena eeeh
 
Habarini
Ngoja niende kwenye maono yangu.....

Kwakuwa serikali inahamia Dodoma, inamaana kuwa nguvu ya jiji pendwa DSM inapungua kwa maana shughuli, ofisi, wizara zinahamia Dodoma.

Pia endapo suala la kugenga reli ya kisasa Dsm- mwanza inamaana huduma nyingi sana zitkuwa zinapatikana nwanza kama dsm

Huku wakati jiji la Dsm likipungukiwa nguvu, jiji la mwanza linazidi kukua kwa kasi.... maana ndo litakuwa hub au jiji la kibiashara East Africa.

Nchi jirani wanaotegemea bandari za Tanzania watachukulia mwanza bidhaa zao kwa kusafirishwa na reli ya kisasa from dsm.

Pia uwanza wa ndege wa kisasa unajengwa ksa ushirikiano na nchi ya oman... hivyo basi watu tuine hizo fursa ambazo zipo mwanza and tuzithmie effectively

Baada ya muda tutakuwa na majiji makuu 2 yenye ushindani ya kibiashara

Nawasirisha
Hii ni projection au interpolation ya mawazo uko sawa kabisa japo sio vyema kulinganisha mjusi na mamba ukasema wote wako sawa.Ila kimantiki uko sahihi kabisa Mwanza itakua sana.Hata hivyo watu hawajui tu uwepo wa vilima Mwanza unaweza sema haikui lakini ingewezekana ukavitandaza vilima vyote vikawa tambarare na nyumba zake ungegundua Mwanza ni kubwa sana.Tatizo la dar ni moja tu joto kama tanuru la moto.Wakoloni walikosea sana kuichagua kuwa makao makuu wangefanya kama ilivokuwa Nairobi
 
Nikweli si rahisi Mwanza kuifikia Dar na bahati mbaya ile speed watu wa Mwanza tuliyokuwa nanazidiwa na Dar ime double mara 4 kiasi cha kuona vumbi tu.

Miaka michache nyuma Mwanza tulikuwa tunazidiwa na Dar kila kitu mara 2, kuanzia pato la taifa mpaka na population lakini kipindi hiki tunazidiwa mara 4 zaidi na hili limekuja kwenye kipindi cha awamu mbili za Kikwete.

Selikari kuu imehusika sana katika ujenzi wa miundo mbinu hasa barabara za rami wakati huku kwetu jukumu hilo limebaki kwa halmashauri.

Taasisi za majeshi zimejenga maghorofa na nyumba za kawaida nyingi sana.

Kumejengwa viwanja viwili vya michezo katika eneo moja, ule uwanja wa Taifa wa zamani ungeweza kujengwa hata Mwanza,

Ndani ya kipindi kifupi tu uwanja wa ndege wa Dar umetanuliwa mara mbili mfurulizo huku wa Mwanza ukipigwa danadana,

Kikwete kawajengea kwao hospital nyingine kubwa kimajengo karibu sawa na Bugando wakati tayari kulikuwa na Muhimbili, Mwanza hatuna hospitali kubwa ya serikali, Bugando ni ya wenyewe na nikubwa kimajengo tu ila sio vifaa tiba na wataalamu.

Kikwete alivipandiaha hadhi vyuo vya kati vya Dar kuwa University mfano kile cha ualimu Chang'ombe alafu akakiacha kile cha Butimba Mwanza.

Kajenga daraja la Kigamboni wakati kuna njia ya barabara ya kuzungukia Mbagala lakini kaacha kujenga Mwanza - Sengerema abako hakuna njia ya karibu zaidi ya kuzungukia Kahama.

Mifuko yote ya jamimii iliagizwa kujenga majengo marefu Dar japo kwa hili siwezi laumu labda walizingatia zaidi wapi watapata wapangani wanaolipa vizuri.

Ukweli lazima tuuseme, kama Magufuri akiamua kuifanya Mwanza kuwa mshindani wa kweli waDar inawezekana akipenda japo inaweza zusha vurugu.

Kujenga bomba la mafuta kutoka Dar mpaka Mwanza ili kufanya bei ya mafuta zikaribie kulingana.

Kujenga Mwanza vyuo vikuu vitano vikubwa kama UDOM.

Kuwapa mashariti rahisi zaidi wawekezaji watakao kubali kuwekeza Mwanza.

Kujenga Hospitali kubwa na ya kisasa kuliko ile Kikwete aliyojenga kwao.

Kujenga dimba la michezo kama like la Dar, pia kujenga magereza kubwa tano ili wafungwa wa mikoa mingine waletwe Mwanza, hii itasaidi kuongeza mzunguko wa pesa.

Serikali kwa makusudi ijenge Mwanza viwanda vyote muhimu kuanzia rangi, saruji, mabati na vifaa vingine vya ujenzi.

Yafungwe Mwanza majenereta makubwa ya kuzalisha umeme wa grid ya Taiga zaidi ya yale yalioko Dar.

Mwisho serikali ijenge Mwanza base kubwa ya jeshi kushinda zile za Dar na pia shule nyingi za A level ili kujaza wanafunzi na watumishi.

Mambo hayo niliyoyataja karibu yote yalifanyika Dar na ndio sabau pakaendelea hivyo. Fulsa za kazi za kuajiliwa zilitengeneza population kubwa sana ambayo ndio msingi wa kujiajiri pia.

Hata hivyo sioni rais mwenye dhamira ya kweli ya kuibeba Mwanza zaidi ya mimi jiwe la maji ikiwa ikatokea miujiza ya kuwa rais.
Mwanza ikikua sana bukoba nayo itakuja juu sana maana ni kama mwendelezo Wa mji hasa pakiwepo meli
 
Back
Top Bottom