Baada ya mashambulizi: Tumerejea hewani, Tupo imara zaidi!

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Staff member
Feb 10, 2006
4,234
13,422
Wakuu,

Tunafarijika kuwafahamisha kuwa tumerejea hewani baada ya kupata mashambulizi ya makusudi yenye kulenga kuzuia upatikanaji wa huduma kwa watumiaji wa JamiiForums (DDOS Attack) kwa takribani masaa 7, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 2 usiku.

rx37PuU.png

yfEIpw6.png


Mashambulizi haya yaliyolenga kuidhoofisha miundombinu yetu, yamefanywa kwa kupangwa na kwa kiwango tulichobaini kuwa yalifanywa na wataalamu waliobobea katika masuala ya mashambulizi ya kimtandao.

Tunalaani kwa nguvu zetu zote kitendo hiki na vingine vya mwelekeo kama huu vyenye kulenga kunyamazisha sauti za wananchi.

Timu yetu ya wataalamu itaendelea kufanya kazi kwa umakini zaidi katika kipindi hiki cha Uchaguzi na tunaomba ushirikiano wa wanachama na wadau wa JamiiForums pale mtakapoona huduma zetu zinasuasua kwa namna yoyote ile katika upatikanaji. Wasiliana nasi kupitia support@jamiiforums.com

Tunawashukuru sana kwa uvumilivu wenu katika kipindi hiki na tunawatakia kila la heri katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu.

Maxence M. Melo,
K.n.y Uongozi wa JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom