Baada ya marehemu Mzee Mengi, Bakhresa pekee ndiye mzalendo kwa Watanzania. Wengine ni cartels tupu!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Mungu Ampe Afya na Maisha Marefu Bakhressa na Azam Yake Tanzania.

Anatoa huduma huku akifanya biashara kwa wakati mmoja.

Haendekezi Tamaa kwa kupandisha bei yoyote kwa bidhaa na huduma zake zote!

Hatumii visingizio vya Ukraine na Urusi, kama wafanyavyo wengine wote nchi hii.

Bei zake ni rafiki kwa wananchi wa madaraja yote.

Analipa kodi za serikali na hatujamsikia hata siku moja kukumbwa na kashfa ya ukwepaji kodi.

Hahitaji kuwatumia wanasiasa kwa jambo lolote lile.

Amekamata Biashara halali katika nyanja zote, na wala hahitaji masifa,kupitia wapambe!

Usipokutana na Azam sebuleni kwenye Luninga kwa taarifa zote pamoja na Michezo yote. Utakutana nae mezani kwenye Chakula!

Usipokutana na Azam Mezani kwenye Vitafunio, basi utakutana nae kwenye Uwanja wa Mpira!

Usipokutana na Azam Viwanjani,basi Utakutana nae Baharini kuelekea Zanzibar!

Usipokutana na Azam kwenye Soka, utakutana na Azam kwenye Ndondi au Boxing!

Usipokutana nae Baharini kwenye boti za kisasa,utalala kwake hotelini Zanzibar!

Usipolala hotelini Azam,basi utakutana nae kooni kwako kupitia Maji ya Azam au lambalamba za Azam!

Na sasa ameamua kutuokoa kutoka genge la wapanga bei za Sukari.
Azam ameingia kwenye viwanda vya kuzalisha Sukari nchini.

Na tumjuavyo yeye, atakuja na bei inayolingana na uhalisia wa gharama halisi za uzalishaji!

Pia Azam ni mkombozi kwa teknolojia mpya ya Upambaji na urekebishaji magagati ya Upholstery!

Sasa tunamsubiria aje na "AZAM AIR" ili atuondolee ukiritmba wa upangaji bei zisizo rafiki kwenye sekta ya usafiri wa Anga.

Ndio Maana #Azam hashikiki, kwa sababu anampendeza Mungu Machoni kwa woote!

Alamsikhi!
 
pascal mayala ana-type.pumba zake
Mkuu MoseKing, usichokijua wewe ni kuwa hata hizo pumba kwako, ni chakula kwa mwingine!, kama lilivyo ganda la mua la jana, kuna mwingine kwake ni kivuno!.

Tuendelee kupepeta humu, wengine wapepete mchele waondoke nao, pumba watupe, wanakuja wengine kuziokota hizo pumba ni chakula kwa viumbe wengine!.

P
 
Bakhresa anastahili pongezi Kwa kweli Yule Mzee , tofauti na Yule mhuni mwekezaji
 
Mkuu MoseKing, usichokijua wewe ni kuwa hata hizo pumba kwako, ni chakula kwa mwingine!, kama lilivyo ganda la mua la jana, kuna mwingine kwake ni kivuno!.

Tuendelee kupepeta humu, wengine wapepete mchele waondoke nao, pumba watupe, wanakuja wengine kuziokota hizo pumba ni chakula kwa viumbe wengine!.

P
achana nae huyo mtoto wa juzi
 
Mungu Ampe Afya na Maisha Marefu Bakhressa na Azam Yake Tanzania.

Anatoa huduma huku akifanya biashara kwa wakati mmoja.

Haendekezi Tamaa kwa kupandisha bei yoyote kwa bidhaa na huduma zake zote!

Hatumii visingizio vya Ukraine na Urusi, kama wafanyavyo wengine wote nchi hii.

Bei zake ni rafiki kwa wananchi wa madaraja yote.

Analipa kodi za serikali na hatujamsikia hata siku moja kukumbwa na kashfa ya ukwepaji kodi.

Hahitaji kuwatumia wanasiasa kwa jambo lolote lile.

Amekamata Biashara halali katika nyanja zote, na wala hahitaji masifa,kupitia wapambe!

Usipokutana na Azam sebuleni kwenye Luninga kwa taarifa zote pamoja na Michezo yote. Utakutana nae mezani kwenye Chakula!

Usipokutana na Azam Mezani kwenye Vitafunio, basi utakutana nae kwenye Uwanja wa Mpira!

Usipokutana na Azam Viwanjani,basi Utakutana nae Baharini kuelekea Zanzibar!

Usipokutana na Azam kwenye Soka, utakutana na Azam kwenye Ndondi au Boxing!

Usipokutana nae Baharini kwenye boti za kisasa,utalala kwake hotelini Zanzibar!

Usipolala hotelini Azam,basi utakutana nae kooni kwako kupitia Maji ya Azam au lambalamba za Azam!

Na sasa ameamua kutuokoa kutoka genge la wapanga bei za Sukari.
Azam ameingia kwenye viwanda vya kuzalisha Sukari nchini.

Na tumjuavyo yeye, atakuja na bei inayolingana na uhalisia wa gharama halisi za uzalishaji!

Pia Azam ni mkombozi kwa teknolojia mpya ya Upambaji na urekebishaji magagati ya Upholstery!

Sasa tunamsubiria aje na "AZAM AIR" ili atuondolee ukiritmba wa upangaji bei zisizo rafiki kwenye sekta ya usafiri wa Anga.

Ndio Maana #Azam hashikiki, kwa sababu anampendeza Mungu Machoni kwa woote!

Alamsikhi!
Umesahau hata pale feri kwenda kigamboni utakutana naye kwenye vipantoni viwili vinaitwa tax
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom