Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Sasa hivi umeamua kuandika articles controversial ili uone tuta react vipi. Paschal na wewe umekuwa mtu wa kutafuta kiki?
 
Na ile kanda huwa haishindwi,
Makonda akipitishwa na chama basi ndio atakuwa rais wetu 2025
 
Nami nimeshangaa sana mtu anayejiita mwanahabari mbobezi na msomi leo hata 2020 bado anazungumzia 2025!!! Na yupo na uhakika kwamba aliyepo atafika huko bila kuhesabu sababu zinazoweza mfanya asifike!!

Huyu kijana anatia kinyaa sana!
 
Jambo la kushukuru ji kwamba Watanzania ni wa aina moja tu, waliosoma na wasiosoma hawana tofauti yoyote ile.
Ukitaka kujua hebu fatilia kazi za wakuu wa mikoa halafu utajua watanzania ni wa aina gani. Wanatakiwa kufanya nini kwa wananchi? Nani anaiona kazi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu ? hayupo kabisa kwasabau tuna tatizo kubwa moja la kuendeshwa na matukio.
Makonda ni mzuri ila sio kwa kiwango watu wanachotaka kuaminishwa, kipi ambacho amebuni na kimekuwa productive kwa wananchi wa jiji lake? Sio huyu anayehangaishana na machinga bila hata kupata suluhisho? Sio huyu anayehangaika na madada poa, shisha, kofia ngunu za pikipiki, utambuzi wa kila mtu ndani ya nchi, zoezi la kupanda miti na usafi(dar ishakuwa safi kama kigali?)
Hayo yote yangewezekana kiurahisi kama tungeanzia kwenye sheria zetu tulizojiwekea wenyewe.
Tanzania haitahitaji tena nguvu 2025 zaidi ya akili kwani wakati huo kila mtu atakuwa mjuaji, sheria tu tulizojiwekea ndio itakuwa rahisi kwetu na sio mtu mmoja.
 
No way, yani tuongozwe na wagonjwa wa akili kwa miaka 20? NO WAY!
 
Majanga haya,mtu kama makonda hafai kupewa madaraka makubwa
 
Kwa lugha yetu Mayala maana yake njaaaa,, Hivyo hatukushangai
 
Makonda awe rais sipati picha aisee! Labla awe waziri ila rais duh! Raia watapelekeshwa balaa yaana tutapangiwa hadi time ya kulala na wake zetu
 
Nami nimeshangaa sana mtu anayejiita mwanahabari mbobezi na msomi leo hata 2020 bado anazungumzia 2025!!! Na yupo na uhakika kwamba aliyepo atafika huko bila kuhesabu sababu zinazoweza mfanya asifike!!

Huyu kijana anatia kinyaa sana!
Haya mazungumzo ya wazee wenye ndevu na mvi za kutosha tunapojadili masuala ya Nchi na utawala tunajua...kabla ya kupeleka kwa wananchi.Wewe kaa kimya tukichoka tunakutuma gazeti
 
Huyu jamaa kwa kukurupuka ndiye mwenyewe! Sijui anataka kuchukua ushekh yahya!?

Makonda ana kipi special kiasi cha kumuona anafaa?
anza na mwaka wake mmoja wa ukuu wa mkoa ni innovation idea gan iliyowasaidia wananchi zaidi ya siasa za muda mfupi?
 
Uthubutu huu huweza kufika mahali mtoto akamwambia mzazi wake ungechelewa ningekuzaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…