Baada ya maandamano ya chadema nchi nzima nini kifuate? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya maandamano ya chadema nchi nzima nini kifuate?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Mar 3, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wandugu,

  Maandamano ni njia mojawapo ya kuonyesha kutokuridhika na mambo fulani. Kwa muda sasa CDM imeweza kufanya maandamano makubwa kwenye mikoa kanda ya ziwa.

  Ni suala la msingi kuangalia mafanikio ya maandamano hayo na kujadili nini kifuate baada ya maandamano hayo. Haya ni mambo ya muhimu kufanyika. Ni jukumu letu wote kuangalia nini cha kufanya ili kuweza kuleta mabadiliko.

  Serikali inakosea pale ambapo badala ya kujifunza na kutekeleza majukumu yake baada ya wananchi kuonyesha kutokuridhishwa kwao yenyewe inalalamika na kulaumu CHADEMA kwamba wana nia ya kuvunja amani.

  Ni jukumu la serikali kutathmini wananchi wanapinga nini na hatua gani zichukuliwe. Endapo hilo litashindikana miaka mitano itakuwa migumu sana kwa upande wa serikali na haitakuwa sahihi kusema kwamba CDM wanachochea nchi isitawalike. Matatizo ya wananchi ndio yatasababisha nchi isitawalike, sio CDM.

  CDM wanachofanya ni 'kusema' matatizo ya wananchi. Wananchi wanachofanya ni 'kusikiliza' matatizo wanayoyaishi kila kukicha. Watanzania wengi wanaowatetea hawana afya, elimu, ajira, nyumba bora za kuishi nakadhalika. CDM wanatoa tu ujumbe, wananchi wanaishi hayo matatizo.

  Swali linabaki, nini kifanyike (wananchi na CHADEMA) baada ya maandamano? Toa mawazo yako na mapendekezo kwa faida ya taifa lako na chama chako.

  Nawasilisha.
   
 2. R

  RMA JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe ndiye mgeni usiyejua kilichotokea Tunisia na Misri? Baada ya maandamano ya Chadema sasa kilichobaki ni ku-Copy na ku-paste zile notice za Misri!. Kwa lugha rahisi nikwamba, iwapo katika mchezo golikipa wa timu mashuhuri anafungwa magoli zaidi ya saba kwa uzembe, na bado anaendelea kung'ang'ania kukaa golini. Mashabiki huwa wanamfanyaje?

  Chadema imeishawaambia mashabiki kuwa timu yao inafungwa kwa sababu golikipa amehongwa na kwamba hapo alipo anatetea tu maslahi binafsi. Hana uchungu na timu. Mashabiki wanapoamua kumuacha golikipa huyo aendelee kuwadhalilisha, ni utaahira mkubwa sana. Kikwete ameishahongwa na Rostam! Hana uchungu na nchi tena. Kuendelea kumuacha madarakani ni balaa, ni janga la kitaifa... naam, ni utaahira!
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  RMA, hii ya kwako kali. Nilikuwa nasinzia nimeamka. Sasa unamaanisha mashabiki watoke jukwaani wakamtoe kipa golini!?

  Hiyo sio kazi ya kocha tena? Au kocha na yeye kanunuliwa?

  Na je hata wakimtoa golini na wameshafungwa goli saba bila (7-0) inakuwaje? Wataweza kurudisha kweli? Na mashabiki wakishuka uwanjani kumtoa kipa refa si atamaliza mpira? Au ndio kusubiri mechi nyingine? Hakutakuwa na kufungiwa?

  Hayo yote ni masuali tu nimebaki nayo! Otherwise naamini la msingi ni cut and paste kilichotokea Tunisia na Egypt and now Libya! Ahsante
   
 4. Jahmercy

  Jahmercy Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mh. diwani wangu nakuku kubali sana kwa fikra zako makini, nadhan baada ya maandamano haya ningefurah kama wabunge wa CDM wangepeleka hoja binafsi bungeni ya kuitaka serikali kupunguza mishahara na posho za wabunge na mawazir pamoja na rais, kuacha kununua magar ya kifahar kwa mawazir na watumish wa umma na pia kupandisha kima cha chini cha mishahara, kwa watumish wake.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,198
  Trophy Points: 280
  Timu imeshafungwa 7-0, bora mechi iishie njiani kuliko kuendelea kufungwa mengine, wapenzi wa Simba na Yanga wanasema bora kuweka mpira kwapani tutapata la kujitetea mbele ya watani kuwa dk 90 hazikuisha.
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tatizo wakipeleka hoja binafsi bungeni kwa wingi wa wabunge wa ccm wataichakachua tu nakama ujuavyo spika mwenyewe naye ni walewale kawekwa na watu wenye nguvu.
   
 7. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi naona kupeleka hoja Bungeni kwenye Bunge lililogeuzwa kuwa Jumba la mipasho na CCM itakuwa haisaidii na haitakuwa na Tija kwani CCM hawatakuwa tayari kujadili na kuandaa anguko lao,sasa basi cha muhimu ni sisi wananchi ambao tunakabiliwa na hizi kero kutokana na unyonyaji na ukandamizwaji unaotokana na utawala wa kidhalimu wa CCM tuamue hata tukifanya maandamano ya kuwatoa ni lazima tuhakikishe watu wote waliochaguliwa na KJ hawatakuwa katika madaraka ya mpito ili kueousha mambo ya fadhila kwani hapa kwetu Tanzania tuna tatizo la ki mfumo hivyo tuandamane kuuondoa mfumo kandamizi na wala tusije kuandamana kwa lengo la kumtoa mtu kwani sisi tatizo sio mtu bali ni mfumo,sasa hata tukiandamana tuhakikishe tunaung'oa mfumo kandamizi.
   
 8. M

  MushyNoel Senior Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kitakachofuata ni kusema heri shari kamili kuliko nusu shari . Then we implement what Tunisia&Egypt have already done. We have that big heart to do it !
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hoja mbili tulizo nazo kwa kuziweka sawa (watoa hoja wanirekebishe) ni;

  1. Kupeleka hoja binafsi bungeni kuhusu matumizi ya serikali

  2. Kuendelea kuandamana kubadili mfumo kandamizi wa uongozi

  Ngoja tuendelee kujadili ili tufikie mahali tujue ni wapi tunataka kuelekea, tunaelekea vipi na lini.
   
 10. m

  mob JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote.
   
 11. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kinachotakiwa kufanyika bado kiko mioyoni mwa watanzania na siku ikifika utaona watakachofanya,natumai mifano tunaiona
   
 12. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mzee nyerere naye kakaa miaka 23 (maaana jk atasiku moja awezi kumwita nyerere baba wa taifa)sijui alimfanya nini....kazi kweli kweli maji ya shingo ssm.
   
 13. l

  limited JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hiyo ku copy and paste haitatusaidia, kuna kupanga na kutathmini siu tu kwamba leo hii ccm wakiondoka madarakani kutakuwa na neema.
  hata cdm(au chama chochote) wanaweza wakapewa nchi leo hii lakini wasipojipanga it will be the same thing, cha msingi ni kujiuliza how do we prevent uzembe wa aina hii kutokea? na mimi nafikiri kuweka katiba ambayo itawabana wanasiasa wote kuwajibika kwa watu waliowachagua
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na hofu ya serikali imeanza kujionyesha wazi. Jana Wassira kwenye TBC1 alihangaika sana na yanayofanywa na CHADEMA.
   
 15. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hawa nao walijaribu kudesa-onto bila ya kuzingatia tofauti ya mazingira na utayari wa watu wao kufa pale itakapobidi kwa ajili ya kufanikisha mabadiliko wanayoyahitaji.

  Wao walidhani tu kama wengi wanavyodhani kuwa kwa kuwa imewezekana kwa Waarabu wa Afrika basi itawezekana pia kwa Weusi wa Afrika.


  Anti-Mugabe protest fails to take off

  Cris Chinaka

  Harare - Internet campaigns calling for protests against the 31-year rule of President Robert Mugabe on Tuesday did not lead to any mass gatherings in Zimbabwe, where police have threatened to crush any "Egypt-style" protests.

  The two campaigns, on Facebook and Twitter, were trying to start popular uprisings similar to ones that toppled the long-serving leaders of Tunisia and Egypt and are threatening Libyan strongman Muammar Gaddafi.

  Although there was no unusual security deployment in Harare on Tuesday, private newspaper NewsDay reported that soldiers in armoured troop carriers had been "sighted" on Monday in traditionally restive townships in the capital.

  The Facebook campaign calling for a million citizen march and a separate one on Twitter were aimed at bringing down Mugabe, 87, leader since independence from Britain in 1980.

  Zimbabweans in London were planning to burn an effigy of Mugabe outside of the country's embassy in London in support of the Facebook campaign.

  But by mid-morning, there was no sign of any gathering in the large park in Harare named as the protest venue by the organisers operating under the banner FreeZimActivists.

  Other parks, normally packed with people, were largely empty, apparently over people's fears of being caught up in any protest.

  Zimbabwe's dominant state media made no reference to the planned demonstration against Mugabe, who rights groups say has used violence and intimidation to crush any challenges.
   
 16. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Kama chadema ikichukua nchi leo (coz haitakaa ipewe) kuna mabo ya msingi tayari umeshayaonge ili kubadilisha mambo yanavyoenda, kwanza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za watanzania, mf: magari ya kifahari, pili kufanya upya mikataba itakayokuwa na maslahi kwa watanzania, na kumbuka DR. Slaa alisema ataleta katiba mpya within 100 days!! ni hayo tu
   
 17. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Butola,

  Zimbabwe imeshindikana kwa sasa. So what should be done? Wait for the ballot box?

  One thing about Zimbabwe is, wana uhakika baada ya miaka mitano Mugabe atakuwa weak zaidi. Uzee umepiga hodi and he cant rule forever. Kama wamevumilia miaka 34 sidhani kwa tabia zetu waafrika miaka mingine michache iliyobaki kabla hajafa ni shida kusubiri.

  Just a thought
   
 18. H

  Haika JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Maandamano ni muhimu, kuamsha waliokata tamaa na uendeshaji wa nchi, wajue kuwa sasa kumejitokeza kundi linalotaka tena kupigania maslahi ya WENGI. ni kitu muhimu sana, kujua tu kuna dalili ya mapambazuko, kuamsha tena uzalendo.

  Wakati wa hotuba hizo ni muhimu kutaja shida na kujulisha wasikilizaji kuwa zinafahamika na ndio vipa umbele.

  Ni muhimu pia kuwataka wasibweteke, waamke wawe radhi kufanya tena bidi wakijua system itakuwa inawasapoti.

  Maandamano yalikuwa muhimu kutoa elimu ya uraia, uraia wa Tanzania

  Maandamano ni muhimu sana kuonyesha mshikamano, umoja katika jambo hili.

  ONYO
  Katika msafara wa mamba kenge nao huwepo, tuna uhakika katika safari yetu hii, kuna kenge wengi tu, watajichuja tu taratibu, ila safari itaendelea
  Ila tunagemea mikwaruzo mingi sana kutoka kwao, mingine itatoa michubuko na makovu, ila safari itaendelea.
  Tunategemea wasiopenda ukombozi wa WENGI watajitokeza tu, ila safari itaendelea.
  Kuna wenye nia nzuri tu, ila watatishwa na ugumu wa safari, ila safari itaendelea.
  Kuna wakati tutagombana wenyewe kwa wenyewe bila sababu ya msingi, ila safari itaendelea.

  TUOMBEANE SALAMA, SI LAZIMA TUFIKE WOTE HUKO KWENYE TANZANIA NZURI, TUNAYOIMBA TANGU UTOTONI,
  ila tunaombwa mashujaa wote wanaojitoa kwa ajili ya hili, kwa ajili yamchango wao mdogo/mkubwa wakumbukwe, vizazi hata vizazi!!
  Waandikwe kwenye vitabu vya historia.
   
 19. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,074
  Likes Received: 15,729
  Trophy Points: 280
  [BAADA YA MAANDAMANO SASA KINACHOFUATA CHADEMA wakalale wapumzike ikulu wameikosa
   
 20. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  YES.

  Utawala wa Tanzania bado si wa kimabavu kama ule wa Gaddafi na wala hauwanyimi wananchi wake haki yao ya kuchagua au kuchaguliwa kwenye uongozi kama ule wa Misri, bado tuna matatizo ya msingi katika nchi hii yaliyotokana na viongozi waliojisahau na wasiotekeleza wajibu wao kwa taifa lakini waliochaguliwa na watu kwa njia za kidemokrasia, hivyo bado wananchi hawa wanawajibika kwa uamuzi walioufanya, ndiyo maana ya uchaguzi.

  CDM na vyama vingine vya upinzani viendeleee kutumia fursa zilizopo kujijenga na kuonyesha uongozi mbadala wenye uwezo wa kuwaondolea wananchi matatizo wanayokabiliana nayo ndani ya utawala wa CCM, bado mazingira ya kisiasa yaliyopo yanaruhusu vyama pinzani kuyafanya haya na kama fursa hii wataitumia vizuri kwa kuonyesha "uongozi uliotayari kutawala kwa ajili ya watu" basi wananchi watakuwa na option ya wazi zaidi juu ya Tanzania waitakayo kati ya 2015-2020.

  Hakuna shortcut katika kujenga utawala wa kidemokrasia, ifike wakati sasa wananchi wawajibike kwa ubovu au umakini wa machaguo yao na kutokana kwayo waanze sasa kuona umuhimu wa kushiriki kwenye mchakato wa kuamua hatma ya nchi yao kwa njia ya uchaguzi.
   
Loading...