Baada ya maandamano ya chadema nchi nzima nini kifuate?

Aliyofanya Dr. Slaa kule maswa yanadhihirisha yale ya Arusha alitaka akamatwe wananchi walete fujo apate pa kulaumu kuwa JK kasema watalinda usalama wa nchi. Sasa kakamatwa nje hakuna mwenye hila kama zake wa kuhamasisha watu wakamtoe kwa nguvu, wamaswa si waarusha!!

Cha kushangaza hakuna mwana JF aliyepost tukio lile humu!!
Jana kulikuwa na threads mbili humu ndani ya JF juu ya kukamatwa kwa Dr. Slaa; na ya tatu ilianzishwa wakati taarifa zilishaenea toka kwa Regia kuwa ameshaachiwa na walikuwa wanaelekea BKB.
Inaonekana hizo threads zilikupita pemebeni; pia radio one hukusikiliza kwani nayo ilizungumzia suala hilo.
JF hapafichiki kitu.
 
Kanda ya ziwa ni mwanzo tu, lazima kwenda Mtwara, Lindi, Songea, Mbeya, Iringa, Morogoro; then dodoma, singida, Tabora. Kigoma, Rukwa, Katavi; halafu Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, na DSM.
Baada ya hapo unapima kuona wananchi wamefikia level gani ya kuweza kudai kwa njia ya maandamano.
Kwa kuanzia, maandamano haya yanapaswa kuamsha serikali ili itimize hayo waliyoahidi; siyo kuilalamikia CDM. Kama serikali itatimiza, basi hakuna haja ya maandamano zaidi, ikikaidi, na watu wakawa wameshahamasika, them wimbi la mapinduzi ya africa litachukua nafasi.
Kwa hiyo kwa sasa kuamua nini kitafuata si rahisi kwa kuwa next step inategemea vitu mbalimbali ( a lot of ifs)
 
Wandugu,

Swali linabaki, nini kifanyike (wananchi na CHADEMA) baada ya maandamano? Toa mawazo yako na mapendekezo kwa faida ya taifa lako na chama chako.

Nawasilisha.

Cha kufanya hapa ni kusubiri na kuona Serikali iliyoingia madarakani itafanya nini baada ya uchaguzi. Kuangalia je, itatimiza ahadi zake, itarekebisha kasoro, itaondoa kero n.k. na hapakuwa na haja hata ya kuandamana na kupoteza muda wa wananchi. Serikali inajua wajibu wake na naamini inegundua kasoro ziko wapi bila kuambiwa. Asante kwa kuchangia
 
Cha kufanya hapa ni kusubiri na kuona Serikali iliyoingia madarakani itafanya nini baada ya uchaguzi. Kuangalia je, itatimiza ahadi zake, itarekebisha kasoro, itaondoa kero n.k. na hapakuwa na haja hata ya kuandamana na kupoteza muda wa wananchi. Serikali inajua wajibu wake na naamini inegundua kasoro ziko wapi bila kuambiwa. Asante kwa kuchangia

suala la kusubiri ndio limetufikisha hapa tulipo leo.. if we really need change za kweli kwa manufaa ya taifa la kesho inabidi tuwangoe hawa watu kwa njia yeyote ile ila sio kwa kupeleka hoja bungeni.. bunge lenyewe wamejaa vilaza wa ccm sijui hata nani aliwachagua wale watu... ukipeleka hoja utaishiwa kuzomewa na kutolewa vijembe huku wananchi wakiendelea kuteseka,,

saa ya ukombozi ni sasa..
 
suala la kusubiri ndio limetufikisha hapa tulipo leo.. if we really need change za kweli kwa manufaa ya taifa la kesho inabidi tuwangoe hawa watu kwa njia yeyote ile ila sio kwa kupeleka hoja bungeni.. bunge lenyewe wamejaa vilaza wa ccm sijui hata nani aliwachagua wale watu... ukipeleka hoja utaishiwa kuzomewa na kutolewa vijembe huku wananchi wakiendelea kuteseka,,

saa ya ukombozi ni sasa..

Subira yavuta Kheri. Haraka haraka ...... Mbio za sakafuni ....... Tusiwe na pupa, huko tunakokimbilia wala hatupajui sana. Jambo jema hupatikana kwa njia ya Amani. 2015 haiko mbali.
 
Mh. diwani wangu nakuku kubali sana kwa fikra zako makini, nadhan baada ya maandamano haya ningefurah kama wabunge wa CDM wangepeleka hoja binafsi bungeni ya kuitaka serikali kupunguza mishahara na posho za wabunge na mawazir pamoja na rais, kuacha kununua magar ya kifahar kwa mawazir na watumish wa umma na pia kupandisha kima cha chini cha mishahara, kwa watumish wake.

Mimi nilitaka wabunge wa CDM wangegomea ile mikopo ya terms poa ya milioni 90 za kununua gari la mbunge na badala yake waombe hizo pesa ziwe directed kwenye miradi ya maendeleo. Yaani ki ufupi Wabunge wa CDM wanapaswa waanze kuonyesha efforts zao ki vitendo katika kuwasaidia wa Tanzania msaada wa kiukweli sio huu wa mbunge kulipia wanafunzi 40 ada ya sh. alfu 20 kwenye shule za kata.

Ikiwezekana waige mfano wa Mbunge wa Tanga mjini..Mh! Omari Nundu ,yeye ame fanya projection ya mshahara wake kwa miaka mitano na sasa anazigawa kwa wakazi wa jimbo lake katika mfuko wake wa jimbo wa maendeleo . Hii bla blaa ya kuonyesha kama tunaajali wananchi sasa kuna haja ya kuonyesha ki-vitendo.
 
Labda ungewauliza na CHADEMA, nini yatakuwa mafanikio yao baada ya haya maandamano?

Badala ya kipindi hichi watu kujipanga na kuanza kuuza sera au kutunga sera za kuikosoa serikali kwa mbinu zao hafifu zinazoleta umaskini lakini wapi, Ukweli wenyewe ufisadi ni tatizo moja kati ya mamia tuliyonayo. Wenzetu wapo busy na maandamano na kuja hapa na mbwebwe za signature waziri kivuli wa sijui wizara gani (I doubt kwa mfano kama waziri kivuli wachadema wa ajira hataweza jibu hakitupiwa makombora ya sera zake kuhusu ajira kwa wanafunzi wanaomaliza chuo kupata kazi let alone the masses of idle young adults without education being used in the employment sector).

Labda tunazani kuendesha nchi ni suala la mchezo? Kuchokwa kwa CCM aina maana yoyote anaweza leta maendeleo bali chama chenye sera mbadala ambazo inaziamini zitaleta maendeleo yes ufisadi ni tatizo lakini si sera. Its time people got to politics and if Im honest I'm beggining to question Chadema's depth as an alternative to the current gov.

IM JUST REALISTIC.
 
Rais astep down ye mwenyewe asisubiri ka ya misri au tunisia au libya au yemen
 
Butola,

Kwetu hapa hali ni tofauti . Wananchi wanaibiwa na wamekata tamaa.Serikali haina majibu haimjui nani anamiliki kagoda inflation inakimbilia 2 digits . Ukitaka kujua wananchi wamechoka angalia baada ya Raisi kuwaonya wananchi wasiudhurie mikutano ya Chadema akisema kwamba Chadema wanacheza mchezo hatari,kesho yake huko kahama wanachi walijitokeza kwa wingi sana . Walienda kinyume na Tangazo la Raisi na tafsiri rahisi hapa ni kwamba hawamwamini tena,

Tusiwe na kumbukumbu fupi,tusisahau tuliyofanya tayari . Arusha kila makamanda wa CDM wanapopandishwa kusomewa kesi watu wanajaa wakionesha kwamba hawako tayari kuona uonevu .Wakapigwa mabomu wakimsindikiza Lema ofisini kuonesha kwamba mitazamo yake kwa Arusha hasa kipindi hiki ndo sahihi.

Tusikandamize utashi ambao watu wanao kuleta mabadiliko . Yote yanawezekana ni muda tu unabeep !

Mkuu unawazungumzia hawa wananchi wa Tanzania ambao pamoja na matatizo uliyoyazungumzia waliipa CCM ushindi miezi minne tu iliyopita??hawa wananchi wa Arusha walioandamana siku moja tu na kisha kunywea ata pale ambapo serikali ilitoa taarifa ya uamuzi wake wa kutotekeleza kile walichokuwa wanakipigania??

Ni kweli uchumi umedidimia sana, ni kweli CCM imepoteza uadilifu na umakini wa kiuongozi, na ni kweli uongozi wa Kikwete umekuwa dhaifu mno....lakini haya hayakuanza baada ya uchaguzi wa 2010, wananchi wamemchagua na wamewachagua wabunge wengi wa CCM huku wakiyafahamu yoote haya, kwanini tusijiulize ni kwanini wananchi hawa pamoja na udhaifu woote huo bado waliichagua CCM na CDM? kwanini waliwachagua wabunge wa CCM na sio wa CDM?? kwanini waliwachagua madiwani wa CCM na sio wa CDM?? majibu marahisi hayatatusaidia!!

Kama vyama vya upinzani vinahitaji kuiondoa CCM madarakani havina namna mbadala bali kuitumia miaka hii 4 iliyobaki kabla ya uchaguzi wa 2015 kujijenga zaidi na kuueneza mtandao wa vyama vyao sehemu zote za nchi hii na kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii yetu, hii ni kazi kubwa na isiyokwepeka.

Ifahamike kuwa maandamano hayawezi kuwa ni njia ya kidemokrasia ya kuubadilisha utawala wa nchi, katika nchi yenye jumla ya watu Million 40 endapo utakuungwa mkono na na waandamanaji Million 2 tu ambao ni 5% tu ya wananchi wote unaweza ukauchukua utawala wa nchi ata kama kuna watu Million 30 (75%) ambao hawakuungi mkono kabisa, hii sio demokrasia.

Uchaguzi ndio njia pekee ya kuisikiliza sauti ya wananchi kwa usahihi, tumeisikia sauti hiyo miezi minne iliyopita na wananchi wataongea tena miaka minne ijayo, hatuna njia ya mkato.
 
Uchaguzi ndio njia pekee ya kuisikiliza sauti ya wananchi kwa usahihi, tumeisikia sauti hiyo miezi minne iliyopita na wananchi wataongea tena miaka minne ijayo, hatuna njia ya mkato.

mmmmmmmmmh?
 
Sina hakika na katiba inasemaje juu ya hili, ila nadhani kura ya maoni ingekuwa safi. Kujaribu kufahamu kama watz wanataka serikali ilioko madarakani iondoke au ibaki.
 
Sina hakika na katiba inasemaje juu ya hili, ila nadhani kura ya maoni ingekuwa safi. Kujaribu kufahamu kama watz wanataka serikali ilioko madarakani iondoke au ibaki.

Kwa nchi maskini kama yetu kuna kweli wa umuhimu wa kuongeza gharama za hizi? kwanini tusichague viongozi wetu kila baada ya miaka 5 kama ilivyo sasa?
 
Kwani wewe ndiye mgeni usiyejua kilichotokea Tunisia na Misri? Baada ya maandamano ya Chadema sasa kilichobaki ni ku-Copy na ku-paste zile notice za Misri!. Kwa lugha rahisi nikwamba, iwapo katika mchezo golikipa wa timu mashuhuri anafungwa magoli zaidi ya saba kwa uzembe, na bado anaendelea kung'ang'ania kukaa golini. Mashabiki huwa wanamfanyaje?

Chadema imeishawaambia mashabiki kuwa timu yao inafungwa kwa sababu golikipa amehongwa na kwamba hapo alipo anatetea tu maslahi binafsi. Hana uchungu na timu. Mashabiki wanapoamua kumuacha golikipa huyo aendelee kuwadhalilisha, ni utaahira mkubwa sana. Kikwete ameishahongwa na Rostam! Hana uchungu na nchi tena. Kuendelea kumuacha madarakani ni balaa, ni janga la kitaifa... naam, ni utaahira!

Hiyo ya ku copy na ku paste yale ya tunisia na misri nimeyapenda wakuu, hamna option nyingine inayoonekena kuwa nzuri zaidi. Tukisubiri uchaguzi 2015, kura zita chakachuliwa kama kawa.
 
Kwa nchi maskini kama yetu kuna kweli wa umuhimu wa kuongeza gharama za hizi? kwanini tusichague viongozi wetu kila baada ya miaka 5 kama ilivyo sasa?

Kweli sisi ni masikini namna hiyo!. Kwa umasikini huo tuendelee kunyanyaswa?
Da! Kweli masikini hana thamani. Na gharama ya umasikini ni kubwa mno.
 
Ni muhimu kwa CDM kuangalia kwa makini mwazo yote yaliyotolew hapa mpaka sasa. Naamini mpango wa maandamano una manufaa yake lakini ni lazima mpango huo endelevu. Ni vyema kukawa na mikakati ya nini baada ya maandamano. Kwa mfano, pale Mwanza nini kinaendelea baada ya maandamano kufanyika? CDM inaendelea kukua?

Nia na madhumuni ni kuikomboa hii nchi kutoka kwenye utawala kandamizi. Hatuwezi kuendelea kusubiri bila kuchukua hatua za mabadiliko hata kama ni kwa njia ya box la kura. Lazima tujipange. Tusisubiri kuwa kama Ivory Coast. Tujipange kulinda ushindi wetu.
 
Juma Contena,

Kuhusu depth ya CHADEMA as an alternative political party. CDM has depth. Just in simple words, CDM is not a solid mass. It has members. The two layers of members and leaders should be differentiated. The leaders are doing their work, political work. Building the party. At the background some brains are working on alternative and viable solutions to our problems. Some of those solutions CCM is adopting and we are happy about it.

And, kuna msemo wa kiswahili, 'kama unadhani elimu ghali jaribu ujinga'.

Kama unadhani CDM haina depth, jaribu NCCR, CUF, TLP, UDP, CCM au DP.

Karibu.
 
Mi mawazo yangu ningependa baada ya kuhamasisha hao wananchi tungoje serikali Kama itabadilisha mfumo mzima wa uwongozi na mikataba, ilishindwa Nguvu za umma zipo, Ushauri kwa mfumo mpya, nchi ins population watu million 40 na something kwa nini serikali isigawe majukumu, kwa mfano kier na serikali za majimbo kila mkowa ili kuipunguzia serikali Mzigo ?
 
Naona CCM wameona kabla hata ya maandamano wawape nafasi wananchi kutimiza lengo. Unaposema unafuta chadema unamaanisha unawashaulisha wananchi shida zao? Amani ya nchi hii haitapotea kwa sababu ya chadema. Chadema ni mjumuiko wa wananchi. Hao ndio wenye kuijua na kuilinda amani yao.

Muda wa kutuibia kwa kisingizio cha amani umepita! Fanyeni kazi za wananchi
 
kwa kujibu swali la kichwa cha habari cha hii thread ni kwamba baada ya hapo ni mapinduzi yaani hii naiweka black n white.wala hapo simung'unyi maneno tunataka mabadiliko na tutayapata by hooks or crooks
 
Back
Top Bottom