Baada ya maandamano ya chadema nchi nzima nini kifuate?

Kitakachofuata ni kusema heri shari kamili kuliko nusu shari . Then we implement what Tunisia&Egypt have already done. We have that big heart to do it !

MushyNoel, tatizo litabaki moja tu!! baada ya hapo (aftermath) tutaishije? maana kidogo tulicho nacho tutakua tumegawana kama sii kuchoma moto. Wenzetu Tunisia na Egypt wana pa kuanzia. Tunisia wana mafuta kiasi, Egypt wana Suez Canal piga ua lazima meli zipite ukiachia mbali vyanzo vingine vya mapato. Sisi bado tunatarajia wahisani ambao nao wako mbioni kuivamia Libya kwa sababu wataiba mafuta kulipia gharama za uvamizi wao, je, ni nani atakuja kutuamulia sisi? inabidi tupate taarifa za kiintelijensia kabla ya kuanza shughuli hiyo.
 
Nyamungo, hilo pia ni wazo kutoka kwa Mtanzania. Hii nchi ni yako pia na una haki ya kutoa wazo.

Wafikirie watanzania wamekosa nini na sio CHADEMA wamekosa ikulu.

Kufikiri ni ombi kubwa sana?
 
Tatizo wakipeleka hoja binafsi bungeni kwa wingi wa wabunge wa ccm wataichakachua tu nakama ujuavyo spika mwenyewe naye ni walewale kawekwa na watu wenye nguvu.

Hapo ikishindikana wailete kwa wananchi kama ilivyo kuwa epa, na hyo ndo itakuwa hoja ya kuongeza mvuto kwa chama na hatimaye kupata ushindi uchaguz ujao.
 
rma, hii ya kwako kali. Nilikuwa nasinzia nimeamka. Sasa unamaanisha mashabiki watoke jukwaani wakamtoe kipa golini!?

Hiyo sio kazi ya kocha tena? Au kocha na yeye kanunuliwa?

Na je hata wakimtoa golini na wameshafungwa goli saba bila (7-0) inakuwaje? Wataweza kurudisha kweli? Na mashabiki wakishuka uwanjani kumtoa kipa refa si atamaliza mpira? Au ndio kusubiri mechi nyingine? Hakutakuwa na kufungiwa?

Hayo yote ni masuali tu nimebaki nayo! Otherwise naamini la msingi ni cut and paste kilichotokea tunisia na egypt and now libya! Ahsante

"tunasema heri ya lawama kuliko fedheha"
 
Wandugu,

Maandamano ni njia mojawapo ya kuonyesha kutokuridhika na mambo fulani. Kwa muda sasa CDM imeweza kufanya maandamano makubwa kwenye mikoa kanda ya ziwa.

Ni suala la msingi kuangalia mafanikio ya maandamano hayo na kujadili nini kifuate baada ya maandamano hayo. Haya ni mambo ya muhimu kufanyika. Ni jukumu letu wote kuangalia nini cha kufanya ili kuweza kuleta mabadiliko.

Serikali inakosea pale ambapo badala ya kujifunza na kutekeleza majukumu yake baada ya wananchi kuonyesha kutokuridhishwa kwao yenyewe inalalamika na kulaumu CHADEMA kwamba wana nia ya kuvunja amani.

Ni jukumu la serikali kutathmini wananchi wanapinga nini na hatua gani zichukuliwe. Endapo hilo litashindikana miaka mitano itakuwa migumu sana kwa upande wa serikali na haitakuwa sahihi kusema kwamba CDM wanachochea nchi isitawalike. Matatizo ya wananchi ndio yatasababisha nchi isitawalike, sio CDM.

CDM wanachofanya ni 'kusema' matatizo ya wananchi. Wananchi wanachofanya ni 'kusikiliza' matatizo wanayoyaishi kila kukicha. Watanzania wengi wanaowatetea hawana afya, elimu, ajira, nyumba bora za kuishi nakadhalika. CDM wanatoa tu ujumbe, wananchi wanaishi hayo matatizo.

Swali linabaki, nini kifanyike (wananchi na CHADEMA) baada ya maandamano? Toa mawazo yako na mapendekezo kwa faida ya taifa lako na chama chako.

Nawasilisha.

Mimi nawashauri sana wana Chadema kuwa badala ya kupoteza muda mwingi kulalama basi wajipange kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa hapo mwakani na uchaguzi mkuu 2015 na sio kutaka kuchafua hali ya hewa hapa nchi na kuleta machafuko.

Huo ni ushauri wa Bure. wajifunze toka kwa CUF Zanzibar
 
Mkuu kwa hiyo CHADEMA nao wakomae na maandamano mpaka CCM itakapokubali kufanya nao mazungumzo yatakayounda serikali ya mseto?
 
Tokea uhuru watanzania tumejifunza kuwa watii na waadilifu. Uadilifu wetu umepitiliza na tunajikuta tukigeuzwa wajinga. Tunaingia Shirikishoi la Afrika Mashariki. Elimu yetu haba na uwezo wetu wa kufanya kazi ni mdogo. Uchumi wa mtu mmojammoja ni duni sana. Nina hofu siku moja baadhi ya wananchi wataitwa wapumbavu kwa kushindwa kumudu gharama za maisha kutokana na mabadiliko ya hali ya uchumi. Walio nacho watatuona si kitu si lolote, maana tutaishia kuwa wapagazi wa wakenya na kufanya biashara kwenye maduka ya waganda ambao wamefunzwa biashara tokea utotoni. Mashamba yetu yatavamiwa na wafugaji wa kenya, tutakuwa wachungaji/walinzi wa mifugo yao.

Mafisadi wa Tanzania wataanza uwekezaji katika mapori makubwa nchini. Sisi makabwera tutakuwa wapagazi wao.

Haki zetu zote zitaminywa na walio nacho.

Nikirudi kwenye hoja, baada ya maandamano, lazima watanzania tuamue kufanya mabadiliko. Tuamue kukipa chama madaraka ya kututoa pale tulipo na kwenda mbele zaidi. Nachanganyikiwa kusikia Kauli hii: Nyerere alitawala miaka 23 alituacha masikini, Mwinyi miaka 10 na Mkapa vivyo hivyo, nami nitawaacha vivyohivyo!!! Nini maana ya kuchagua kiongozi?? Vipaumbele vyake 13 ni vya nini??? Ilani ya Uchaguzi ni ya nini? Kampeni zake zilikuwa za nini?? Kama hana mikakati ya kupunguza umaskini wa Mtanzania, Ikulu yuko anafanya ninini?? Tuna haja ya kumsaidia, apumzike, apishe wengine wenye vision na mission za kutusukuma! Si wengine ni CHADEMA. Muda umefika, twende Mnazimmoja Square, tung'ang'ane hadi kieleweke. Jana Bukoba walifurika wafuasi. Watu walitoka Ngara, Karagwe, Misenyi, Chato, Biharamulo kuja kusikiliza tu, hawajalipiwa na mtu nauli wala posho ya malazi na chakula, je wakiambiwa twende Mnazi mmoja kudisplay mabango, tuimbe, na kucheza ng'oma za kumwondoa IKulu, nani atashindwa kwenda??? That is the next step!!
 
Baada ya maandamano ya chadema nchini kuwahamasisha na kuwelimisha wananchi juu haki zao na demokrasia warudi maofisini na wabunge waende kwenye majimbo yao wakafanye kazi na kamati maalumu iandike ripoti na kuiwasilisha kunakotakiwa wapewe chao fasta.

Swala la tunisia ni tofauti na misri na misri ni tofauti na kwa gadafi kwa hiyo ukicopy na kupaste utaumia wewe kwanini usilianzishe kabla ya kuona wenzio wamelianzisha? Kama unafuatilia swala la libya vizuri tayari mataifa jambazi yanayotumia demokrasia na haki za binadamu kupora mali za nchi nyingine wanaangalia uwezekano wa kuivamia libya ili kumuondoa gadafi unahani watauwa wangapi katika zoezi lao? Uingereza inataka kuivamia Libya na kuweka majeshi ya kulinda usalama, duh yaleyale ya DRC Congo, Iraq na Afghanistan wanajidai kulinda usalama ilihali majeshi yanakamua dhahabu sasa Libya wanascramble for oil and gas na si democrasia wala haki za binadamu wanzosingizia. Sasa wewe leta ya misri, libya na tunisia hapa uone kama kuna mtu atakusapoti hata tuuwawe wangapi wala hutasikia haki za binadamu wala demikrasia maana tayari wanamiliki migodi, wanatafiti mafuta na uranian. Tujihadhari.

Cha msingi ni kuwasihi wabunge wa CHADEMA kugomea malipo ya 90mln kama wameshachukua warudishe wabakiwe na hela ya kununua landrover au gari zisizohitaji gharama kubwa kuziendesha kiasi kingine wapeleke mswada kuwa kitumike kununua vitanda na magodoro kwenye hosipitali kubwa za mikoa au ziongezewe katika ile bajeti ya kununulia bajaji ya kusafirisha wagonjwa inunue ambulance kadhaa. pili wakatae mshahara mkubwa wanoupewa na posho wakubali kupata mshahara wa kawaida hata angalau wa maprofesa yaani kati ya milion 2-3.

Kama vipi waanzishe maandamano mengine ya kuamsha wananchi juu ya wajibu wao kama wananchi katika kujenga taifa. Maana kwa sasa wanawaendea kwa mada ya dowans. Naamnisha kutoa civic education kama ilivyofanyika juzi kule kenya kwa nchi nzima na mkenya yoyote popote pale walipokuwa waliimba wimbo wa Taifa kufufua mshikamano katika kuijenga nchi.
 
Mi naona cdm wavumilie tu jamani si mnaona afya ya rais wetu jinsi ilivyo? Hata maaandamano yetu sasa kwa mkwere ni shida tupu kwa hiyo si tunavyoandamana tunazidi kumpunguzia siku za kuishi sema tuanze kujiandaa kwa uchaguzi kabla ya 2015 maana jeshi watachukua nchi kwa muda afu tutasubiri muda mfupi ili kupisha uchaguzi mkuu nadhani ni 2013 kama sikosei.
 
Wandugu,

Maandamano ni njia mojawapo ya kuonyesha kutokuridhika na mambo fulani. Kwa muda sasa CDM imeweza kufanya maandamano makubwa kwenye mikoa kanda ya ziwa.

Ni suala la msingi kuangalia mafanikio ya maandamano hayo na kujadili nini kifuate baada ya maandamano hayo. Haya ni mambo ya muhimu kufanyika. Ni jukumu letu wote kuangalia nini cha kufanya ili kuweza kuleta mabadiliko.

Serikali inakosea pale ambapo badala ya kujifunza na kutekeleza majukumu yake baada ya wananchi kuonyesha kutokuridhishwa kwao yenyewe inalalamika na kulaumu CHADEMA kwamba wana nia ya kuvunja amani.

Ni jukumu la serikali kutathmini wananchi wanapinga nini na hatua gani zichukuliwe. Endapo hilo litashindikana miaka mitano itakuwa migumu sana kwa upande wa serikali na haitakuwa sahihi kusema kwamba CDM wanachochea nchi isitawalike. Matatizo ya wananchi ndio yatasababisha nchi isitawalike, sio CDM.

CDM wanachofanya ni 'kusema' matatizo ya wananchi. Wananchi wanachofanya ni 'kusikiliza' matatizo wanayoyaishi kila kukicha. Watanzania wengi wanaowatetea hawana afya, elimu, ajira, nyumba bora za kuishi nakadhalika. CDM wanatoa tu ujumbe, wananchi wanaishi hayo matatizo.

Swali linabaki, nini kifanyike (wananchi na CHADEMA) baada ya maandamano? Toa mawazo yako na mapendekezo kwa faida ya taifa lako na chama chako.

Nawasilisha.
....wananchi tushinikize serikali kuhusu utekelezaji wa ahadi "hewa" wanazotoa!!!
 
Aliyofanya Dr. Slaa kule maswa yanadhihirisha yale ya Arusha alitaka akamatwe wananchi walete fujo apate pa kulaumu kuwa JK kasema watalinda usalama wa nchi. Sasa kakamatwa nje hakuna mwenye hila kama zake wa kuhamasisha watu wakamtoe kwa nguvu, wamaswa si waarusha!!

Cha kushangaza hakuna mwana JF aliyepost tukio lile humu!!
 
Mh. diwani wangu nakuku kubali sana kwa fikra zako makini, nadhan baada ya maandamano haya ningefurah kama wabunge wa CDM wangepeleka hoja binafsi bungeni ya kuitaka serikali kupunguza mishahara na posho za wabunge na mawazir pamoja na rais, kuacha kununua magar ya kifahar kwa mawazir na watumish wa umma na pia kupandisha kima cha chini cha mishahara, kwa watumish wake.

Hii hoja kaka itakuwa ngumu kusikilizika, kwa sababu pale bungeni tuna Makinda ila Speaker bado simuoni
 
Aliyofanya Dr. Slaa kule maswa yanadhihirisha yale ya Arusha alitaka akamatwe wananchi walete fujo apate pa kulaumu kuwa JK kasema watalinda usalama wa nchi. Sasa kakamatwa nje hakuna mwenye hila kama zake wa kuhamasisha watu wakamtoe kwa nguvu, wamaswa si waarusha!!

Cha kushangaza hakuna mwana JF aliyepost tukio lile humu!!

Wewe kwanini usipost?? Au na wewe ulikamatwa???
Sasa kama alikamatwa anafanya hila za vurugu, kwa nini walimwachia badala ya kumfungulia mashitaka ya uchochezi na uvunjifu wa amani?
 
Aliyofanya Dr. Slaa kule maswa yanadhihirisha yale ya Arusha alitaka akamatwe wananchi walete fujo apate pa kulaumu kuwa JK kasema watalinda usalama wa nchi. Sasa kakamatwa nje hakuna mwenye hila kama zake wa kuhamasisha watu wakamtoe kwa nguvu, wamaswa si waarusha!!

Cha kushangaza hakuna mwana JF aliyepost tukio lile humu!!

Off topic!
 
Kwanza nakupongeza kwa kuona mbali,
kuhusu maandamano mimi naona bado hayajafanyika effectvely kwasababu inatkiwa kila mwananchi anaeguswa ashiriki kikamilifu kiti ambacho bado hakijafanyika
kwa hiyo mi naona kuna haja ya kila mdau wa maendeo kushiriki then tupange cha kufanya
 
Hawa nao walijaribu kudesa-onto bila ya kuzingatia tofauti ya mazingira na utayari wa watu wao kufa pale itakapobidi kwa ajili ya kufanikisha mabadiliko wanayoyahitaji.

Wao walidhani tu kama wengi wanavyodhani kuwa kwa kuwa imewezekana kwa Waarabu wa Afrika basi itawezekana pia kwa Weusi wa Afrika.

Harare - Internet campaigns calling for protests against the 31-year rule of President Robert Mugabe on Tuesday did not lead to any mass gatherings in Zimbabwe, where police have threatened to crush any "Egypt-style" protests.

The two campaigns, on Facebook and Twitter, were trying to start popular uprisings similar to ones that toppled the long-serving leaders of Tunisia and Egypt and are threatening Libyan strongman Muammar Gaddafi.

Although there was no unusual security deployment in Harare on Tuesday, private newspaper NewsDay reported that soldiers in armoured troop carriers had been "sighted" on Monday in traditionally restive townships in the capital.

The Facebook campaign calling for a million citizen march and a separate one on Twitter were aimed at bringing down Mugabe, 87, leader since independence from Britain in 1980.

Zimbabweans in London were planning to burn an effigy of Mugabe outside of the country's embassy in London in support of the Facebook campaign.

But by mid-morning, there was no sign of any gathering in the large park in Harare named as the protest venue by the organisers operating under the banner FreeZimActivists.

Other parks, normally packed with people, were largely empty, apparently over people's fears of being caught up in any protest.

Zimbabwe's dominant state media made no reference to the planned demonstration against Mugabe, who rights groups say has used violence and intimidation to crush any challenges.

Butola,

nafikiri zimbabwe na Tanzania kuna tofauti kubwa sana . Licha utawala huo wa mda mrefu lakini Mugabe amekuwa mwiba kwa mabeberu .Katika hotuba yake aliyoitoa UN alimkaribia Bush waziwazi akimwita muuwaji na hana mamlaka ya kumfundisha mtu democrasia . Akamkumbusha Bush kwamba licha ya Ian Smith kuwaonea wazimbabwe lakini baada ya weusi kushika madaraka hawakumwua au kulipiza kisasi (ian smith aliua watu zaidi ya 50,000) mugabe akasema after we take power "" We tought him democracy,we gave him back his humanity ''' na kwa wakati huo ambao mugabe alikuwa anazungumza ian smith alikuwa analima shamba la hekta 7000 na kuchangia kwenye GDP ya nchi . Mugabe pengine ni mzalendo aliebakia ( mawazo yangu ),,kajijengea heshima kwa nchi yake na hataki vibaraka au unyonyaji wa hao makaburu.

Kwetu hapa hali ni tofauti . Wananchi wanaibiwa na wamekata tamaa.Serikali haina majibu haimjui nani anamiliki kagoda inflation inakimbilia 2 digits . Ukitaka kujua wananchi wamechoka angalia baada ya Raisi kuwaonya wananchi wasiudhurie mikutano ya Chadema akisema kwamba Chadema wanacheza mchezo hatari,kesho yake huko kahama wanachi walijitokeza kwa wingi sana . Walienda kinyume na Tangazo la Raisi na tafsiri rahisi hapa ni kwamba hawamwamini tena,

Tusiwe na kumbukumbu fupi,tusisahau tuliyofanya tayari . Arusha kila makamanda wa CDM wanapopandishwa kusomewa kesi watu wanajaa wakionesha kwamba hawako tayari kuona uonevu .Wakapigwa mabomu wakimsindikiza Lema ofisini kuonesha kwamba mitazamo yake kwa Arusha hasa kipindi hiki ndo sahihi.

Tusikandamize utashi ambao watu wanao kuleta mabadiliko . Yote yanawezekana ni muda tu unabeep !
 
Tatizo wakipeleka hoja binafsi bungeni kwa wingi wa wabunge wa ccm wataichakachua tu nakama ujuavyo spika mwenyewe naye ni walewale kawekwa na watu wenye nguvu.

Wakichakachua basi wananchi na viongozi wa vyama vyao wanapata sababu ya kuendelea kuweka presure. Wakitia akili basi utaona vitabia vya kibabe vinaanza kupungua....Hivyo hivyo mpaka kina eleweka
 
Mimi nawashauri sana wana Chadema kuwa badala ya kupoteza muda mwingi kulalama basi wajipange kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa hapo mwakani na uchaguzi mkuu 2015 na sio kutaka kuchafua hali ya hewa hapa nchi na kuleta machafuko.

Huo ni ushauri wa Bure. wajifunze toka kwa CUF Zanzibar

Hivi Zanzibar ni kipi kimebadilika? Welfare imeongezeka au? Je serikali ya umoja wa kitaifa ndo suluhisho au? I think we miss the basics of what it meant by opposition!
 
Hapa tuwe na subira sumu ya mabadiliko haijakolea bado tusubiri tuone mwitikio wa maandamano Mbeya, iringa kigoma, moshi na kwingineko.Viongozi wetu wa CDM wamesema YANAFANYIKA NCHI NZIMA, Tuache watu waonje waone maandamano yalivyo matamu, kumbukeni hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanganyika kufanya maandamano ya kupinga sera/mfumo ya serikali , kwa hiyo it is a historical event, hapa tu panatosha kutoa sifa kwa watanganyika kuthubutu.
Swala la kuukataa utawala litakapofika haitakuwa isssue tena.
Na mkumbuke iwapo watu watakaa .....squares hakuna askari atakayepata ujasiri wa kurusha mabomu kwani hata wao wataona ndiyo muda muafaka wa kudai haki zao , lazima watakuwa upande wetu.mFANO HAI TUMESHUHUDIA JINSI ASKARI WALIVYOKUWA WATULIVU KULE MAANDAMANO YALIKOFANYIKA KWANI WANAJUA KUPITIA HAYO MAANDAMANO NA WAO KERO ZAO ZITKUWA SOLVED SIMULTENEOUS.
 
Back
Top Bottom