Baada ya leseni za Drones serikali igeukie CCTV Camera

Mtukudzi

Senior Member
Nov 14, 2013
103
408
Tanzania ni nchi tajiri sana. Serikali ya awamu ya tano imetukumbusha kuwa tuna vyanzo vingi vya mapato vinavyoweza kuleta makusanyo mengi ya kodi kupitia serikali kuu, mashirika ya umma na Mamlaka za serikali za Mitaa.

Baada ya kugundua chanzo kipya ambacho ni leseni za kurusha ndege zisizo na na rubani(drones) naomba igeukie upande wa hizi CCTV camera. Leseni hizi pamoja na kuingiza kipato kwa serikali zitazuia matumizi holela ya Camera hizi. Camera hizi zimekuwa zikileta mtafaruku kwenye jamii na kwa ajili hiyo zinatakiwa kudhibitiwa.

Mara kadhaa Mh. Mkuu wa Wilaya ya Hai Bw. Sabaya amejikuta kwenye matata kwa sababu ya CCTV hizi. Tunajua kuwa teknolojia imekuwa kubwa na inawezekana mara zote serikali imefanya uchunguzi kubaini kuwa Bw. Sabaya amekuwa anaandamwa kwa sababu za kisiasa.

Kuonyesha matukio ya kuhusishwa na uingiaji wa nguvu kwenye mahoteli ya wawekezaji na kwenye studio za TV usiku wa manane siyo vizuri yakaachwa. Watakaopewa leseni wapewe na miiko ya matumizi yanayofaa ya picha zinazokutwa kwenye hizi Camera.
 
Tanzania ni nchi tajiri sana. Serikali ya awamu ya tano imetukumbusha kuwa tuna vyanzo vingi vya mapato vinavyoweza kuleta makusanyo mengi ya kodi kupitia serikali kuu, mashirika ya serikali na Mamlaka za serikali za Mitaa...
Itapendeza kwani mwendo ni kuibua vyanzo vipya vya mapato Hadi wanyonge wajinyonge.
 
Ccctv camera ni wachache.

Itungwe sheria Ili umiliki simu ni lzm ukate leseni ya kutumia simu na lzm ulipie mafunzo jinsi ya kutumia simu simu zote zisizo na vigezo hivyo zifungiwe hapa tutakusanya Kodi nyingi Sana itakayotosha kukamilisha miradi
 
Tanzania ni nchi tajiri sana. Serikali ya awamu ya tano imetukumbusha kuwa tuna vyanzo vingi vya mapato vinavyoweza kuleta makusanyo mengi ya kodi kupitia serikali kuu, mashirika ya umma na Mamlaka za serikali za Mitaa...
Wakishamaliza huko kwenye CCTV waje kukusanya kodi za "KUWEZANA".
 
Tanzania ni nchi tajiri sana. Serikali ya awamu ya tano imetukumbusha kuwa tuna vyanzo vingi vya mapato vinavyoweza kuleta makusanyo mengi ya kodi kupitia serikali kuu, mashirika ya umma na Mamlaka za serikali za Mitaa...
Kodi ya tv, kodi ya dish la satelite, kodi ya car alarm, kodi ya baiskeli, kodi ya kua na mke zaidi ya mmoja, kodi ya kua na watoto zaidi ya ya wawili, kodi ya kupaua kwa bati la msauzi. vyanzo vya mapato ni vingi, serikali inazembea tu
 
Kiuchumi usitegemee Sana kukusanya tegemea zaidi kwenye uzalishaji Ili uchochee export upate pesa za kigeni badala ya kutegemea mikopo. Maana mikopo inariba itakiwayo kuirejesha hata kabla ya mradi kuanza kulipa
 
Kwa wanaotumia mifumo ya security fulani fulani, ile panick button unailipia kiasi fulani kwa mwaka, ati ikibonyezwa mawimbi yake yanaenda TCRA sijui blah blah gani, kwahiyo inalipiwa!
 
Back
Top Bottom