Baada ya kutua mwezini, India sasa yaelekea Juani

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,194
10,929
India ndio nchi ya mwanzo kufanikiwa kutua kwenye ncha ya kusini ya mwezi ambako ndiko kwenye matumaini zaidi ya kuwepo kwa maji yatakayorahisisha kupiga kambi huko kwa ajili ya tafiti zaidi kuhusu ulimwengu.

Baada ya mafanikio hayo wiki kadhaa zilizopita kwa kutumia chombo cha Chandrayaan sasa nchi hiyo imefanikiwa kurusha roketi ya Aditya-L1 inayotarajiwa kufika juani baada ya miezi 4.

Adity itasafiri kilomita 1,500,000 mpaka itakapofikia sehemu ijulikanayo kama Lagrange kwenye uso wa Jua.Nchi kadhaa ikiwemo Japan tayari wameshapeleka vyombo vyao tangu 1981 ili kupata takwimu mbali mbali zinazohusu jua na matokeo yatokanayo nalo.

1693657599308.png
 
Back
Top Bottom