Baada ya kuona hamna nafuu, Manji aamsha popo

Bora aende kuepuka misukosuko isiyo ya lazima. Hi nchi Bado haijatulia kivile!
Mzimu wa jamaa bado umeshika hatamu.Naona kamatakamata ya wapinzani imeanza,soon wasiojulikana watatoka likizo ngoja turejee toka Rwanda kwanza
 
Kwa mambo aliyoyafanya huyu jamaa na wanayoendelea kuyafanya wenzie wanaojiita wahindi au waarabu wenye asili ya Tanzania ni bora waende tu..

Ule uamuzi wa Iddi Amin kufukuza wahindi Uganda ulikuwa sahihi sana, kuendelea kuishi na jamii yenye ubinafsi na kandamizi kwa wengine ni bora kuwa masikini na kutafuta namna nyingine ya kujinasua kuliko kuendelea kuishi na hizi jamaa...
 
Awamu ya nne Watanzania tulio wengi tulilalamikia sana wizi na ufisadi wa akina Manji, Rostam nk na kelele zikapigwa sana dhidi ya hawa waasia, washiraz na waarabu wengine..lakini maajabu leo eti tunawatetea tena..
 
Lazima wawekezaji wakimbie kutokana serikali kuitangazia dunia kwamba kuna magaidi nchini na matukio ya kubambikia watu kesi.

Hata kama ni wewe huwezi kuweka mtaji wako sehemu ambapo hujui kesho mamlaka zitakupa kesi gani au zitaharibuje biashara zako

Taratibu...wakimbie sababu gani? DRC Congo ingesuswa kabisa.
Vita vya panzi furaha ya kunguru
 
Sasa wewe ulitaka ghaidi Mbowe aendeleze ugaidi bila kutiwa nguvuni? Kila lenye mwanzo Lina mwisho,ugaidi nchini upo na Mbowe Ni kweli kuwa Ni gaidi
 
Taratibu...wakimbie sababu gani? DRC Congo ingesuswa kabisa.
Vita vya panzi furaha ya kunguru
DRC ni tofauti na huku... Wanaoharibu usalama DRC ndio haohao wanaochota rasilimali za nchi ile wakishirikiana na baadhi ya watu serikalini
 
Mfanyabiashara Yusuf Manji amerejea ughaibuni baada ya kukaa nchini kwa takribani mwezi mmoja huku akikumbana na misukosuko baada ya kukamatwa na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kisha kuachiwa kwa dhamana.

Taarifa zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na watu wa karibu wa Mwenyekiti na mfadhili huyo wa zamani wa klabu ya Yanga, zinaeleza kuwa aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi uliopita Julai akielekea Afrika Kusini aliko mpaka sasa na kwamba kuna uwezekano ikamchukua muda zaidi kurejea tena nchini.
Uonevu unazidi kushika kasi.
 
Yaani binafsi ningekuwa na mamlaka ningefukuza Indians na Arabs wote tukaanza upya....hawa ni watu wanaoitafuna hii nchi kimya kimya sana na kutengeneza utajiri mkubwa then wanauhamishia ughaibuni, India, Oman, na Dubai..
 
Kwa yanayoendelea ni ngumu Sana kutoka mzimu wa mwendazake ndio umeshikilia darubuni ushahidi ni kwa yanayotendeka.

Yule Bwana nadhani amerudi kwa staili ya kimzimu hivi kwa jinsi mambo yanavyoenda.

Wanasema mwili ndo ufa roho uendelea kuishi.
Wenzako tunatamani hiyo mizimu ya mwendazake irudi hata 100000
Ile ilikuwa machine ya kazi na maendeleo
 
Nilitoa alert mapema kuwa it's too early kukubali sarakasi na maneno matamu ya huyu mama miezi miwili ya mwanzo! I was definitely right CCM ni ile ile ukubwa wa matatizo waliyoyaleta ni wao kutoka tu ndio tunaweza kufumbua macho na kuanza upya
 
Wenzako tunatamani hiyo mizimu ya mwendazake irudi hata 100000
Ile ilikuwa machine ya kazi na maendeleo
Aaah Kwa uchumi upi au makusanyo yepi hali Wawekezaji na matajiri walihamishia kodi zao nchi jirani,hadi leo tumecollaps wameishia kuwapora wananchi masikini kupitia dabo tozo za dhuluma,means ziwa limekauka.
 
Kukamatwa kwa Mbowe na kamatakamata ya wapinzani lazima imshtue kila investor, maana wanajua, uvunjaji haki ukianza huwa hauishi kirahisi
 
Aaah Kwa uchumi upi au makusanyo yepi hali Wawekezaji na matajiri walihamishia kodi zao nchi jirani,hadi leo tumecollaps wameishia kuwapora wananchi masikini kupitia dabo tozo za dhuluma,means ziwa limekauka.
Wezi ndiyo waliokimbia na kuamisha biashara wewe ukumsikia mama alipo sema wawekezaji wanataka kuondoka baada ya kifo cha magufuli hii ina maana magufuli alivutia wawekezaji wa kweli sio matapeli singasinga
 
Manji sasa anaishi kama digidigi kweli maisha haya we acha tu,eti muhindi akakimbizwa mchakamchaka na msukuuma tena mchato
 
Mfanyabiashara Yusuf Manji amerejea ughaibuni baada ya kukaa nchini kwa takribani mwezi mmoja huku akikumbana na misukosuko baada ya kukamatwa na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kisha kuachiwa kwa dhamana.

Taarifa zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na watu wa karibu wa Mwenyekiti na mfadhili huyo wa zamani wa klabu ya Yanga, zinaeleza kuwa aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi uliopita Julai akielekea Afrika Kusini aliko mpaka sasa na kwamba kuna uwezekano ikamchukua muda zaidi kurejea tena nchini.

Soma zaidi hapa: Yusuf Manji mikononi mwa Takukuru

Jumapili Agosti 1, 2021 Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni aliiambia tovuti ya Mwananchi kuwa uchunguzi dhidi ya Manji unaendelea na yupo nje kwa dhamana, lakini anaruhusiwa kusafiri.

"Unajua bado tunaendelea na uchunguzi wetu kuhusu Manji na kama unavyojua yupo nje kwa dhamana ambayo haimbani kusafiri, " alisema Hamduni na alipoulizwa kama Manji yupo nchi ama la na kama alitoa taarifa za kusafiri alisema, "Sina uhakika kama amesafiri ama la."

Manji, aliyeondoka nchini mwaka 2018, alirejea nchini Juni Mosi na baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alishikiliwa na maofisa wa Takukuru kwa mahojiano.

Mfanyabiashara huyo aliyeshikiliwa kwa siku nne na Takukuru ikielezwa kuwa ana tuhuma tatu, ikiwemo ya kuisababishia Serikali hasara kwa kukwepa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika biashara yake na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), baada ya kuachiwa kwa dhamana moja ya shughuli alizoshiriki ni mkutano mkuu wa klabu ya Yanga na ndio tukio pekee aliloonekana hadharani na kuzungumza.

Tuhuma nyingine zinazomkabili ni udanganyifu wakati wa ununuzi wa hisa za kampuni ya Tigo ambayo tayari imeuzwa kwa kampuni nyingine ya Madagascar na udanganyifu katika mapato ya klabu ya Yanga.

Licha ya tuhuma hizo, Manji aliamua kurejea nchini, jambo ambalo wachambuzi wa masuala ya siasa, biashara na utawala bora walisema halingewezekana bila mwelekeo wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi sambamba na kuishukia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akiitaka kurekebisha mfumo wake wa ukusanyaji kodi ikiwa ni pamoja na kuzifungua akaunti za wafanyabiashara.

Watu wake wa karibu walilieleza gazeti hili kwamba alirejea nchini kutokana na kutokuwa na wasiwasi na mambo yanavyokwenda na jana wakalieleza Mwananchi kuwa ameondoka kwa sababu kuna vitu anaona havijakaa sawa.

Akizungumza na Mwananchi siku ya Jumapili kwa sharti la kutotajwa jina gazetini, mmoja wa watu wa karibu wa mfanyabiashara huyo alisema; "Aliondoka Julai mwanzoni yupo Afrika Kusini kwa sasa."

"Mambo ya hapa (Tanzania) hayawezi kuna vitu vinaendelea ameona aondoke kidogo ila mwanawe bado tupo nchini."

Alieleza kuwa akiwa Afrika Kusini, Manji anaendelea na biashara zake akisisitiza kuwa anaweza kurejea nchini ila si kwa sasa.
Msitu mpya nyani wale wale
 
Wezi ndiyo waliokimbia na kuamisha biashara wewe ukumsikia mama alipo sema wawekezaji wanataka kuondoka baada ya kifo cha magufuli hii ina maana magufuli alivutia wawekezaji wa kweli sio matapeli singasinga
Alisema lini acha uongo
 
Back
Top Bottom