Baada ya JK kumaliza ZIARA yake Kanda ya Ziwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya JK kumaliza ZIARA yake Kanda ya Ziwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MwanaHaki, Aug 30, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Wote mnaelewa kwamba kwa sasa JK HAFANYI KAMPENI, bali anafanya ziara, akielezea nini "serikali yake" imefanya kwa muda wa miaka tano.

  Baada ya kuondoka, kilichojiri ni .... Polisi watishia kupambana na wachimba madini

  Nenda kacheki, kwenye GAZETI LINALOSEMA UKWELI!

  -> Mwana wa Haki
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kazi wanayo mwaka huu!
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mwandishi Wetu,Mpwapwa

  POLISI katika Wilaya ya Mpwapwa, wameahidi kuendelea kupambana na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Winza, wilayani humo kama watu hao wataendelea kung'ang'ania kuchimba madini.

  Msimamo huo ulitolewa juzi Mkuu wa Polisi wilayani humo, Zedekia Makunja, ambaye alisema hatua hiyo inalenga katika kuwadhibiti wachimbaji katika machimbo hayo yasiyo rasmi.

  Msimamo huo ulikuja kufuatia mvutano mkali uliotokea juzi kati ya pande hizo mbili kiasi cha kuwalazimisha polisi, kutumia nguvu za ziada, ili kuwaondoa wachimbaji.


  Habari za awali zilisema wachimbaji hao wamevamia eneo hilo na kuanza kuchimba madini bila vibali vinavyowaruhusu kufanya hivyo.

  Mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio, alishuhudia vurugu kubwa kati ya wachimbaji wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2,000 na asari polisi.


  Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa, aliwataka wachimbaji hao kuondoka katika eneo hilo na kuwapisha wenye leseni, kuendelea na shughuli za uchimbaji.


  Akizungumza kuhusu hatua ya askari kutumia nguvu za ziada, Mkuu huyo (Makunja) alisema hatua hiyo ililenga katika kuhakikisha kuwa wachimbaji hawaendelei kuwa wakaidi na kuvunja amani katika eneo la machimbo.

  "Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani, hawawezi kurusha risasi bila sababu. Tatizo ni kwamba wachimbaji walikaidi amri na kibaya zaidi walianza kutoa maneno machafu na kuwarushia mawe askari," alisema Mkunja.  Alisema wachimbaji wote wasikuwa na leseni waliambiwa ama watoke au waungane na wenye leseni lakini wao walikaidi.

  ----mwananchi

   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  akija mtu wa nje ndio watamlinda na kumpa leseni
   
Loading...