Baada ya hotuba ya Mh. Rais; Naanza Kula Rushwa

Hivi ukiwa kwenye kiti cha uprezidaa huwa namna ya kufikiri inabadilika?

Mbona JK kabla hajaingia Ikulu alionyesha kuyajua sana matatizo yetu wananchi mpaka tukamwamini na kumwingiza ikulu!!

What happened to our brother now? Is it the problem of the system or the person himself?
 
1. Amesema kuwalipa wafanyakazi kima cha chini cha Tsh. 315,000 ni kuwadhulumu majority ya watanzania, je anajua kiasi gani anacholipwa yeye kama mshahara na marupurupu mengine ya mikutano, safari na n.k. Je haoni kama na yeye anawadhulumu Watanzania?


Napenda kuwa kumbusha pia alisemaaaaa mfanyakazi kulipwa mshahara huo haito wezekana sasa, JK anataka kuniambia 46 yrs ya UHURU kweli katika hotuba ile alishindwa kuja na mikakati na hoja ya msingi ya kuwa weka wafanyakazi sawa jamani Kodi ya nchi hii inakwenda wapi sasa??

Hapo nyuma nilisha wahi sema NCHI HII HAINA MUSTAKABARI KATIKA NYANJA ZOTE KIUCHUMI KIELIMU etc inaendeshwa ilimladi tu bora liende, Objectives za kiuchumi nchii ndio hakuna kabisa kweli twategemea maendeleo leo au ni siasa ndio zaturisha na sio uchapakazi?

Pili hotuba ya JK hapo juzi nadhani inadhihilisha hakuna wafanyakazi na hii ndio picha harisi ya nchi yetu na ukubwa wake wote na inaonekana wanofanya kazi ni wachache sana na kipato kipatikanacho ndicho hicho nchi yakipigia hesabu nini?na kuwadanganya wananchi au wafanyakazi wa serikali wao wanakodi yao inayotozwa tofauti na TRA na hupelekwa HAZINA??

Kwahiyo JK atakubariana na mimi kuhusiana na maneno(HOTUBA) aliyo toa kuwa nchi hii watu hawafanyi kazi kabisa tokea siku ya uhuru tulivyo upata.

UKISHAKUWA KIONGOZI JUA JINSI YA KUJENGA HOJA VIVYO HIVVO NANDIVYO UTAITOA VYEMA NA WATU WATAKUKUBALI, mwanzani ilikuwaje kwa Mwl.JK NYERERE hoja ndizo zilimjenga mpaka kuheshimiwa,kukubarika huko na kukumbukwa milele na sio Politics tuuuuuu
 
Divide and rule tactics, law of jungle-: survival for the fittest that's TZ
 
Wakuu hii hotuba naona imetuacha midomo wazi wengi sana.lakini mda ulivyozidi kwenda umenifanya nimpe pongezi JK kwa kuwa mkweli kwenye swala moja,kutokana na hotuba yake JK kaonesha kwamba serikali yake haiwajali watanzania hata kidogo.Ukweli wake ni kwamba wao hawatujali na kura zetu sio muhimu hata kidogo octoba kwani hazina nguvu kwenye nchi hii.Angekuwa muongo na kujali kura zetu angetoa matumaini kwa watanzania kwani uchaguzi unakuja lakini kwa vile anajua kwamba kura zetu si kitu kwani second term yake hipo guranteed ndio maana tumekumbuna na hotuba hiliokosa elimu.

Kwahio ndugu zangu akili kichwani.
 
Hivi ukiwa kwenye kiti cha uprezidaa huwa namna ya kufikiri inabadilika? Mbona JK kabla hajaingia Ikulu alionyesha kuyajua sana matatizo yetu wananchi mpaka tukamwamini na kumwingiza ikulu!! What happened to our brother now? Is it the problem of the system or the person himself?
Kwa hali ilivyo ni vigumu kujua chanzo ila jibu rahisi na uhakika na prezidaa mwenyewe na chama chake....jamani hebu tufike mahala tuseme CCM sasa basi...............
 
Nayakumbuka sana maneno ya Prof. Lipumba wakati wa kampeni mwaka 2005: "Mtajuta kumchagua Kikwete. Ni mtu wa mizaha tu, sio mtu serious..." Hakika sasa Watanzania wanajuta kumchagua mtu huyu. Mimi binafsi niliwaonya wenzangu wengi tu wasimpigie kura mtu huyu kwani nilikuwa namfahamu vizuri sana kwamba sio mtu serious na hawezi kufanya lolote kusukuma maendeleo ya nchi hii. Bahati nzuri hii hotuba yake ya ajabu ajabu imemuumbua. Sasa naamini Watz wengi wanamfahamu fika, na hawatarudia makosa tena.
 
Angalia TAKUKURU tunao humu ndani wasije wakakukamata kabla hata hujaanza kula hapo mezani pako.Huna habari kama wala rushwa wadogo ndio hukamatwa?wale vigogo wenyewe wanapeta kama hawaoni vile.Umesahau maneno ya Waziri Mkuu?kwamba hao mafisadi papa wana nguvu kushinda serikali?angalia usije ukaozea segerea ukaisahau hata Mtogole yako na watoto wako wapendwa.
 
Kwahio ndugu zangu akili kichwani.

Watanzania wagumu sana kubadilika, haya watayasahau baada ya wiki 2 tu.

Si unajua nchi hii inaongozwa kwa ngonjera.........!!

Nafikiri pia hatuna chama mbadala........CUF ndo haooo wameshajiunga na CCM wakati Chadema ndo hatua moja mbele kisha hatua 100 nyuma!!

Pengine tumebaki na Mch. Mtikila kwenye mapambano dhidi ya wadhalimu!!
 
Si sahihi kutatua tatizo kwa kuleta tatizo lingine. Hao utakao waomba rushwa nao wanashida kama wewe. Kitu cha maana ni kuzidisha harakati zaidi za haraka ili kurudisha heshima ya wafanyakazi.
Na wale watakaoombwa rushwa nao wataendelea kuomba wengine rushwa hadi ngazi ya chini kabisaaaaaaaaaaa kila mmoja anaomba rushwa wa chini yake kwani kila mmoja anakula mezani pake. Sijui mtoto anayekwenda shule chekechea atamuomba nani rushwa. Hii ndio hali inakoelekea.:hurt:
 
Kikwete Kasema muwe wajanja kama Mbayuwayu, mle kwa urefu wa kamba yenu, maana wao wananeemesha matumbo yao na familia zao, sisi tukaze mikanda wao walegeze.
mimi nilitoka kwenye Utumishi wa umma kitambo kidogo, ila najua fadhaa walizo nazo baada ya kauli za huyu Mkwere, wamekereka sana, Bkweli wengi wanafadhaika sana.
 
kijana sio sababu rais kutoa maneno makali ndio uanze kubomoa nchi yako
rais ni mtu wa kawaida kama kakosea jiandae kumtoa madarakani tuu sio
ukate tamaa
 
Ni masaa 60 yamepita toka hotuba ya Mh. Rais iishe pale Diamond Jubilee. Katika hotuba ile aliyoifanya mbele ya 'vikongwe' vya DSM (which to me is a wrong audience cosidering his theme) ilijaa mipasho mingi ya kimwambao.

Binafsi sikuweza kutofautisha 'mipasho' ya pale Lango la Jiji Bar au hotuba za Katibu Mkuu wa CCM Bw. Yusufu Makamba au hata mwanapropaganda Tambwe Hiza. Nili bahatika kuirekodi hotuba yote na kupata nafasi ya ku replay zaidi ya mara tano ili mradi nipate uhakika kama kweli niliyekuwa namsikia na kumtazama ni mkuu wa nchi? Ni yule yule anayetajwa kwenye katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania? Ni yule yule aliyeshinda kwa kishindo (82%) mwaka 2005? Ni yule yule aliyetajwa kama "....Tumaini lililorejea"? Je ni yule yule aliyeahidi kuleta Maisha Bora kwa kila Mtanzania?

Jibu nikapata kuwa ndiye haswaaaaaaa!!

Mengi yamesemwa kuhusu hotuba ile, sitaki niyarejee hapa. Ingawa kuna mitizamo tofauti juu ya hotuba ile, yangu ni haya;

1. Amesema kuwalipa wafanyakazi kima cha chini cha Tsh. 315,000 ni kuwadhulumu majority ya watanzania, je anajua kiasi gani anacholipwa yeye kama mshahara na marupurupu mengine ya mikutano, safari na n.k. Je haoni kama na yeye anawadhulumu Watanzania?

2. Je ni kiasi gani kinalipwa kwa wabunge na mawaziri? Kwa maoni yake kinalingana na pato la taifa?

3. Vipi kuhusu gharama za magari ya kifahari yanayonunuliwa na serikali? Je yanalingana na pato la taifa?

4. Nini mantiki ya kutoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji isiyo na lazima wala tija? Huko ni kuwatendea haki majority ya watanzania?

5. Je Mh. Rais anajua gharama ya maisha kwa sasa? Au kwa vile yeye kila kitu analipiwa? Namkaribisha aje aishi na sisi hapa Tandale kwa Mtogole kwa siku moja tu......naamini hatorudia kuongea yale aliyozungumza pale Diamond.

6. Je yale mahesabu ya Tirioni saba kwa mwaka aliyapiga vipi? Mbona sie tunapa TZS. 1.8 tilioni au alijumlisha na mshahara wa rais, mawaziri, wabunge?


MKAKATI WANGU

Kwa kuwa nimekuwa nikilitumikia Taifa langu katika utumishi wangu wa umma kwa unyenyekevu na uadilifu mkubwa, huku nikijituma pasipo kudai wala kutegemea chochote bali mshahara wangu tu wa Tzs. 163,000 huku nikihangaika huku na kule kulipa pango la nyumba, ada za shule kwa watoto wangu watatu wanaosoma sekondari, chakula, gharama za matibabu, mavazi na matumizi mengine ya msingi.

Nimegundua nchi hii kwa sasa unatakiwa kujali tumbo lako na si utumishi uliotukuka (public service), kwa sasa naahidi kula mezani kwangu kwa kila khali.

Regards,

Mlala hoi
Tandale kwa Mtogole

Utakuwa unaendeleza kula rushwa na si kuanza kula rushwa eti baada ya hotuba ya KJ,rushwa ni utamaduni bongo tusidanganyane.
 
Back
Top Bottom