Baada ya hotuba ya Mh. Rais; Naanza Kula Rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya hotuba ya Mh. Rais; Naanza Kula Rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Brooklyn, May 6, 2010.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ni masaa 60 yamepita toka hotuba ya Mh. Rais iishe pale Diamond Jubilee. Katika hotuba ile aliyoifanya mbele ya 'vikongwe' vya DSM (which to me is a wrong audience cosidering his theme) ilijaa mipasho mingi ya kimwambao.

  Binafsi sikuweza kutofautisha 'mipasho' ya pale Lango la Jiji Bar au hotuba za Katibu Mkuu wa CCM Bw. Yusufu Makamba au hata mwanapropaganda Tambwe Hiza. Nili bahatika kuirekodi hotuba yote na kupata nafasi ya ku replay zaidi ya mara tano ili mradi nipate uhakika kama kweli niliyekuwa namsikia na kumtazama ni mkuu wa nchi? Ni yule yule anayetajwa kwenye katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania? Ni yule yule aliyeshinda kwa kishindo (82%) mwaka 2005? Ni yule yule aliyetajwa kama "....Tumaini lililorejea"? Je ni yule yule aliyeahidi kuleta Maisha Bora kwa kila Mtanzania?

  Jibu nikapata kuwa ndiye haswaaaaaaa!!

  Mengi yamesemwa kuhusu hotuba ile, sitaki niyarejee hapa. Ingawa kuna mitizamo tofauti juu ya hotuba ile, yangu ni haya;

  1. Amesema kuwalipa wafanyakazi kima cha chini cha Tsh. 315,000 ni kuwadhulumu majority ya watanzania, je anajua kiasi gani anacholipwa yeye kama mshahara na marupurupu mengine ya mikutano, safari na n.k. Je haoni kama na yeye anawadhulumu Watanzania?

  2. Je ni kiasi gani kinalipwa kwa wabunge na mawaziri? Kwa maoni yake kinalingana na pato la taifa?

  3. Vipi kuhusu gharama za magari ya kifahari yanayonunuliwa na serikali? Je yanalingana na pato la taifa?

  4. Nini mantiki ya kutoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji isiyo na lazima wala tija? Huko ni kuwatendea haki majority ya watanzania?

  5. Je Mh. Rais anajua gharama ya maisha kwa sasa? Au kwa vile yeye kila kitu analipiwa? Namkaribisha aje aishi na sisi hapa Tandale kwa Mtogole kwa siku moja tu......naamini hatorudia kuongea yale aliyozungumza pale Diamond.

  6. Je yale mahesabu ya Tirioni saba kwa mwaka aliyapiga vipi? Mbona sie tunapa TZS. 1.8 tilioni au alijumlisha na mshahara wa rais, mawaziri, wabunge?


  MKAKATI WANGU

  Kwa kuwa nimekuwa nikilitumikia Taifa langu katika utumishi wangu wa umma kwa unyenyekevu na uadilifu mkubwa, huku nikijituma pasipo kudai wala kutegemea chochote bali mshahara wangu tu wa Tzs. 163,000 huku nikihangaika huku na kule kulipa pango la nyumba, ada za shule kwa watoto wangu watatu wanaosoma sekondari, chakula, gharama za matibabu, mavazi na matumizi mengine ya msingi.

  Nimegundua nchi hii kwa sasa unatakiwa kujali tumbo lako na si utumishi uliotukuka (public service), kwa sasa naahidi kula mezani kwangu kwa kila khali.

  Regards,

  Mlala hoi
  Tandale kwa Mtogole
   
 2. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Naambiwa eti Redet wanampa kichwa mkuu
   
 3. S

  Samat Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kula ndugu, kwakuwa nami ni miongoni mwa wale wa serikalini na team yangu tutaendelea kuandaa semina na vikao kila mwezi nje ya ofisi ili kufidia hayo mapengo yangu ya salary.

  Kila la kheri kwa wale wenye channels
   
 4. T

  Thegreat Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Labda ndicho alichomaanisha JK aliposema kila mtu ana akili zake, kwamba mishahara hapandishi, hakuna kugoma lakini kila mfanyakazi ajue namna ya kuendesha maisha. Matokeo yake ni ufisadi na wizi wa mali ya watanzania.
   
 5. d

  damn JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Msiwaombe tu walalahoi wenzenu rushwa, nao wanalipwa hiyo 104k. kuleni kwa style ya EPA.
   
 6. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si sahihi kutatua tatizo kwa kuleta tatizo lingine. Hao utakao waomba rushwa nao wanashida kama wewe. Kitu cha maana ni kuzidisha harakati zaidi za haraka ili kurudisha heshima ya wafanyakazi.
   
 7. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Kama umeamua kula rushwa kula tu kama wengine wanavyokula na sidhani kama hiyo hotuba ndio kichocheo ni hatari kuendesha maisha kwa kufuata hotuba za wanasiasa manake zinabadilika kutokana na odience na mazingira.
   
 8. I

  Inviolata Member

  #8
  May 6, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama Mheshimiwa Raid anasoma hii forum au angalau kama kuna watu wake wanaingia humu tunaomba ajibu hivyo vipengele 6, mambo yaliyotajwa hapo juu yakidhibitiwa hao wafanyakazi wanaweza kabisa kupata kiwango cha mshahari wanachoomba, bila ubishi kabisa.
   
 9. GY

  GY JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Umekua ukiishije kwa Tsh 163,000 kwa mwezi...Tunaomba mchanganuo tafadhali

  Probably huitaji kuanza kula rushwa kama umeshaonyesha kumudu maisha kwa kiasi hicho cha pesa
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Rais wetu nadhani anasikiliza zaidi muziki ya BONGO FLAVA kuliko kusoma vitabu!! Sidhani kama huyu bwana ni mwanafunzi mzuri wa historia , kwani ingekuwa hivyo angekumbuka kuwa huko nyuma serikali iliwahikupinduliwa kwa watu kuomba mkate toka kwa mfalme na malkia kumwambia awape keki!!! Sasa hawa wafanyakazi wa Tanzania wanamwambia Rais waliyemuweka madarakani kuwa unga unaotupa kukandia mikate hautoshi kwa sababu wenzetu wanasiasa unawapendelea, basi tafadhali gawa upya huo unga ili nasi tuambulie utakaotufikisha angalau mwisho wa mwezi!! Jibu lake Jakaya anasema huo unga mnaopata unawatosha siwezi kugawa upya kuwapunguzia wanasiasa na kuwapa nyinyi msipotaka basi msiupokee!! Jakaya anasahau kuwa hata hicho anachokula na wanasiasa wenzie kinazalishwa na hao hao anaowaambia kuwa wasipokubali mshahara huo mdogo basi waache kazi!! This speech will go down as one of the thoughtless speeches ever given by a head of state in Tanzania, it is a very sad episode!
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sielewi mtu anaishi vipi kwa kima cha chini cha mshahara. lets say yeye na mke wake wanalipwa mishahara hiyo. ina maana wana laki tatu kwa mwezi.

  tufikirie wana watoto watatu wanaosoma wawili primary na mmoja sekondari. watoto wa kike na wakiume. wataishi vip?
   
 12. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hahahaha ! Pole kaka. Kula rushwa kaka kwani wewe ulikuwa unayaamini mahubiri ya rushwa? Mimi nilishawahi kushika na PCCB na nikawapa rushwwa kikaeleweka. we karaga baho.
   
 13. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe 100%. Sijui aliandikiwa na nani? Na sina uhakika kama aliisoma na kutafakari impact yake kabla ya pale Diamond.

  Sasa naanza kuamini maneno ya Hayati Mwl. Nyerere, kwa kweli alikuwa sahihi kumkataa Kikwete!!
   
 14. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bulesi, umenena. Kinachoendelea nchini hivi sasa ni kwamba si wanasiasa pekee ambao wanapendelewa, hata watumishi wa ngazi zote za juu Serikalini wana mishahara mizuri na pensheni zao ni nzuri mno. Yupo ndugu yangu mmoja alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara akastaafu, alipata pensheni ya Sh. milioni 120 (120,000,000/=) achilia mbali zile ambazo atakuwa anapata kila baada ya miezi mitatu ama sita hadi mwisho wa maisha yake. Manaibu Katibu Wakuu na Wakurugenzi wa Idara nina uhakika pensheni zao hazipungui milioni 80. Kwenye Majeshi yetu ndio usiseme wakubwa wametengewa marupurupu ya kila aina ili waendelee kuilinda Serikali kwa kila njia ndio maana wale wote walikuwa wamekaa kwenye jukwaa na Rais walikuwa na nyuso za tabasamu wakati Rais akiwapiga nyundo na kuwakejeli watumishi wa Serikali wanaojaribu kudai na wao wafikiriwe kidogo. Kwa mtindo huu hatufiki popote maana walalahoi kila wanapojaribu kufurukuta na kudai haki yao wakuu hawa wataungana na kuwakandamiza!
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Thanks Bulesi! That day Monday, 03rd May, 2010, will always be remembered in my life. I used to think and I have come to realise kwamba I was very wrong kufikiri kwamba si kila mtu anaweza kuwa rais. Lakini sasa naamini hata kichaa kama watu wakiridhia anaweza kuwa rais na mambo yakaenda tu.Toka huyu mkwere aingie madarakani nimeshuhudia taasisi ya urais ikidhalilishwa mara kadhaa mchana kweupe. Mimi kama mtanzania I feel so bad kwa kweli maana rais ndio sura ya nchi sasa unapokuwa na rais then hachagui hata maneno ya kumtoka kinywani really inatuumiza sana watz na kutufanya tujute maisha kwa kumchagua. Mr. President alipokuwa anasign kwa mbwembwe ile sheria fake ya uchaguzi alisema anafurahi sana kwani kwa mambo yalivyokuwa tulikuwa kwenye hatari ya kuwa na rais kichaa simply tu kwa kuwa ana pesa. With this I dont see any difference with or without the new law we may have a crazy president. Woe to us Tanzanians hv ni kosa gani kubwa tulifanya kwa Mungu mpaka tunaadhibiwa kiasi hiki?
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  akikusikia MREMA AUGUSTINE unamtukana rais wake hivi itakuwa balaaa..................subiri
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  My God! Have Mercy!!!Babangu yupo huko kijijini alikuwa mtumishi ''mhasibu mwaminifu wa serikali'' asiyekula rushwa na amestaafu na ile hela yake ya pensheni imeishia kununua kanyumba kakumsitili.Najikuta nashindwa hata kumtumia elfu 30 ya kumsaidia kwa mwezi kutokana na gharama za maisha zimepanda jijini na mshahara hautoshi.Yesu tafadhali uje haraka!!!!!!!!!
   
 18. p

  posh77 Member

  #18
  May 6, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halahalo wanajamii hodi.
   
 19. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,250
  Trophy Points: 280

  Teh teh, kumbe unaishi pale, JK ana ghorofa lake hapo ukitoka kwa tumbo katikati ya Kwa Tumbo na Mtogole. Kapo kagorofa kazuri tu hapo. Tehe teheeee
   
 20. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,250
  Trophy Points: 280
  Ndo hayo matokeo ya mifuko ya Pension isiyo na ukomo.
   
Loading...