Baada ya haya, CHADEMA 2015 hakuna kizuizi kuingia ikulu!

Baada ya haya, CHADEMA 2015 hakuna kizuizi kuingia ikulu!

wasioamini na wasiamini ila ukiona hata sikonge kimenuka basi mapambano yameiva ...CDM ikuru 2015
 
Mkuu unachokisema ni sahihi sana lakini bado kuna mambo yafuatayo ambayo tunapaswa kuyazingatia na kuyasimamia kikamilifu na kuayweka sawa.

Kwanza hakuna ubishi kwamba mtaji mkubwa wa CDM hivi sasa ni vijana ambao wako shule za sekondari,waliomaliza,walioko vyuo mbalimbali na waliomaliza,na ambao wengi wao hawana ajira,hili kundi kiukweli halitaki mchezo na haliipendi CCM!,lakini tatizo ni moja kwamba bado wanahitaji elimu ili kufunguka zaidi kiakili.

Kwa nini nasema hivyo,kwa sababu ukiajaribu kuangalia chaguzi na hasa ule wa mwaka 2010 CDM ilipata sapoti kubwa sana kutoka kwenye kada hii niliyoitaja na hata ukiangalia kwenye majimbo ambayo CDM inaongoza ushindi wao ulipatikana kupitia kad hii,lakini tatizo ni mojka kwamba hawa ni watu ambao ni wepesi sana kurubuniwa,wanaingia kwenye chama kwa uchungu mkubwa na wana hasira lakini linapofika suala la malahi wanajikuta wameyumba na kurudi nyuma,hili ni tatizo kubwa.

Ndiyo maana nasema kwamba wanahitaji elimu kali ya kuwaingia akilini sawasawa,ili waweze kujisimamia,hata hivyo si wote kwa hiyo kinachohitajika hapa ni mipango ya hali ya juu ili wawe wanamabadiliko kwelikweli sio wa kujaribu.Pipoooooz??
 
Nakuunga mkono binafsi nimepata ripoti ya mkoa wa kigoma , hakuna mpinzani wa mgombea yeyote wa CDM kwa urais
 
hata mgonjwa wa ukimwi huwa anakuwa na matumaini labda kesho atapona ..lakini ndo agona agona

Ukimwi siyo ugonjwa, ndo maana Mchungaji Mtikila alishinda kesi yake ya kumsema mtu kuwa ana ukimwi. Ni hari tu ya maisha na uwatokea wengi sana, just kinga ya mwili kupungu.
 
"If wishes were horses, beggars would ride"!.

It good to keep high hopes for the best, but also get prepared for the worst!.

2015, kuna watu watacheka, na kuna watu watalia, atakaye cheka zaidi, ni atakayecheka mwisho, na atakaye lia sana, ni atakaye lia mwisho, na anayecheke mwisho, haijalishi ushindi unapatikana vipi, just the end justifies the means,
kwa mwendo huu wa Chadema inao endelea nao kwa sasa, 2015 ni CCM Tena!.
P.
 
Kwanza niombe radhi kwa hoja zangu chokonozi dhidi ya chama chetu pendwa cha CHADEMA.

Kabla ya kuanza likizo yangu nilijaribu kufanya japo utafiti usio rasmi kuhusu siasa za Tz na mstakabali wa CHADEMA kuelekea

2015. Hadi mwisho wa likizo yangu iliyonipisha zaidi ya mikoa minne ya kanda ya ziwa pamoja na dsm nimethibitisha bila

shaka kuwa CHADEMA wataingia ikulu kwa kishindo. Anayebisha amuulize KINANA na NAPE.


Namshukuru Mungu kwani hoja zangu chokonozi dhidi ya CHADEMA zilifanya nikoswekoswe vipigo ktk baadhi ya maeneo hasa Musoma, Bunda , Geita na Kahama.


Kwa heri CCM, karibu CHADEMA 2015!
nusura ukoswe koswe, vipigo yaani ww utoe hoja, uambulie kukoswa koswa kipigo sasa hayo ni mapungufu, hata ww siku ya kupiga kura ,ukikumbuka na mwingine akikumbuka litazuka neno TUMECHAKACHULIWA KURA ZETU, ikulu inanidhamu zake toka kwa mgombea, shabiki na mpiga kura.wakitambua hilo ntaungana nawe.
 
tatizo la wana-ccm wengi wanaupeo mdogo sana. Haya ndo matunda ya kukulia ktk jamii yenye fikra mgando ! hata kusoma thread na kuelewa ni tatizo?! Subiri kama unadhani huo msamiati wako wa kuchakachua utakuwa na maana tena 2015! Kwa heri ccm , karibu cdm!
 
Kama kura utapiga kwa niaba ya Watanzania wote usihofu itashinda tu.
 
waacheni tu jamani kwani kukosa macho hata maskio nayo wamenyimwa ...uzuri wanazidi kumpaisha Dr.Slaa pasipo kujua
 
kama CCm wamekulia kwenye fikra mgando. niambie hao chadema walikulia sayari gani ambayo iliwaepusha na fikra mgando?
 
Naunga mkono hoja tumpe Dr Silaa siku 100 watu wahame nchi Peoples............!!!!!!!!!! Jamani tumeibiwa sana au sisi ni sugu wakuibiwa? Jibu ni No..... Mwisho 2015
 
Wanajukwaa huku tukimaliza mwaka kuna hili;

29 October 1995 Presidential Election* [Results by Region]
Registered Voters 8,929,969
Total Votes (Voter Turnout) 6,846,681 (76.7%)
Invalid/Blank Votes 333,936
Total Valid Votes 6,512,745
Candidate (Party) Number of Votes % of Votes
Benjamin Mkapa (CCM) 4,026,422 61.82%
Augustine Mrema (NCCR-Mageuzi) 1,808,616 27.77%
Ibrahim Lipumba (CUF) 418,973 6.43%
John Cheyo (UDP) 258,734 3.97%
*In seven constituencies of Dar-es-Salaam, the results were nullified in seven constituencies due to irregularities. A new round of voting took place in these constituencies on 19 November 1995.

29 October 1995 National Assembly Election*
Registered Voters Not Available
Total Votes (Voter Turnout) Not Available (N/A)
Invalid/Blank Votes Not Available
Total Valid Votes 6,440,913
Party Number of Votes % of Votes Number of Seats 232 (269)***
Chama Cha Mapinduzi (CCM) 3,814,206 59.22% 186 (214)
National Convention for Construction and Reform-Mageuzi
(NCCR-Mageuzi) 1,406,343 21.83% 16 (19)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 396,825 6.16% 3 (4)
Civic United Front (CUF) 323,432 5.02% 24 (28)
United Democratic Party (UDP) 213,547 3.32% 3 (4)
Tanzania Democratic Alliance (TADEA) 76,636 1.19% -
National Reconstruction Alliance (NRA) 60,707 0.94% -
Union for Multiparty Democracy (UMD) 41,257 0.64% -
Tanzania Labour Party (TLP) 27,963 0.43% -
National League for Democracy (NLD) 26,666 0.41% -
United People's Democratic Party (UPDP) 19,841 0.31% -
Popular National Party (PONA) 18,155 0.28% -
Progressive Party of Tanzania-Maendeleo (PPT-Maendeleo) 15,335 0.24% -

MY TAKE; TUTEGEMEE MABADILIKO 2015 AU HISTORIA KUJIRUDIA 1995 ????????

Happy new year in waiting.
 
Ngoja ntarudi muda si mrefu hapa..
 
Embu fafanua kidogo mkuu,sijakuelewa ulikuwa unataka kutueleza nini!
 
Kwa uwezo wa Mungu wa Mbinguni anayewahurumia Watanzania kuendelea kuwa chini ya mfumo dharimu wa ccm atawasidia tu Watanzania tupate mabadiliko kupitia Chadema.

Na Wana Historia mkumbuke kuwa KILA LENYE MWANZO LINA MWISHO, ccm nayo mwisho wake umefika, watake wasitake.
 
Nilipoona chadema kuingia ikulu kwa kishindo kwa haraka haraka nikadhani kuna maandamano yanaelekea ikulu baada ya kusoma vizuri kumbe hamna kitu?tumeyamiss maandamano lakini!

ha ha ha haaaa hujaenda mtwara
 
Back
Top Bottom