Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Kwa sasa tupo kwenye mapambano ya madawa ya kulevya ambalo ni janga kwa sasa ktk Taifa teule la Tanzania mengine haya yasubiri tu.
Tunakushukuru sana mh.Makonda kwa kuweka amsha amsha ya madawa ya kulevya na hatuko tayari kuingia kwenye mada nyingine mpaka la MADAWA YA KULEVYA LIELEWEKE NA TUJUE MWISHO WAKE.
 
Sasa wewe paskali mwandishi wa habari za uchunguzi wewe binafs ni uchunguzi gani umeufanya kubainaisha hilo??
Maana naona ume attach habari zilizo fanyiwa uchunguzi na watu wengine
Leta kile ulichokifanya wewe...
Nili tegemea uje na habari kuwa umeenda tabora na umemuhoji huyo paul
Nikajua utakuja na habari kuwa umekutana na wanafunzi na waalimu walio mfundisha paul..
Badala yake unaleta story za mange kimambi..
Na kukubali sana ila hapa umechemka inatakiwa uonyeshe utofauti kati yako na hao waandishi uchwara
Mkuu Massawee, nilitegemea mtu anasoma kwanza bandiko, akiishaelewa maudhui ndipo anachangia!, sasa wewe ndugu yangu Massawee, jee ulisoma mwanzo wa bandiko langu?. Jee unaelewa nini hapa?.
Wanabodi,
Declaration of interest. Mimi Paskali Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo wa kufanya investigative story kuhusu jambo looted, ila nimeamua kujikita kwenye kuandika developmental news only zenye maslahi kwa taifa, hivyo hii hoja kwenye uzi huu haina maslahi yoyote kwa taifa hivyo siifanyii uchunguzi, ila ina maslahi kwa usafi wa mtu, truthfulness na the audacity kunyooshea watu vidole kumbe...
Uwongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli.

Paskali.
Dr.Kigwangalla alipotuhumiwa humu, kuna mtu yoyote alifanya uchunguzi akaja na uthibitisho?!. Mbona ni Kigwangalla mwenyewe alikuja kukanusha! .

Mbona Mwigulu Nchemba alipotuhumiwa, kuna mtu yoyote alifanya uchunguzi na kupata uhakika wa tuhuma?!. Mbona ni Mwigulu mwenyewe alikuja kukanusha? .

Why tufanye uchunguzi kumhusu Makonda?.
Hii issue ni personal, yuko free kuacha uongo usemwe sana na kygeuka ukweli, au aukanushe na kuusema ukweli wake! .

Paskali
 
Mwacheni Mungu aitwe Mungu

Ukiona dalili yakujigamba sana na ukaribu na Mungu, ikiwa matendo yako binafsi yanakusuta, basi huo ukaribu wa Mbingu na Mungu, na kujigamba ni Mtu wa Mungu, ni kama nguvu ya soda, ambao inajustify udhaifu wa Mtu, yaani ni udhaifu wa kisaikolojia ambao unataka kuulinda na provocative actions, kwa maneno mengine unaweza kusema watu wa namna hii ni attention seekers on dope, but in true nature ni sehemu ya dhambi ya unafiki na udhaifu mkubwa.

Sasa inabidi jambo forum tujitolee kwa kiakili na kimaarifa twende too deep kufichua madhambi ya hawa watu, kuweka ukweli wa Mungu ubaki ni sehemu ya Mungu, na uongo ubakie kuwa wa shetani, na kamwe hatutarudi kuwa mashetani.

CCM bila udanganyifu inawezekana, tusichoshane, we have to start seeing the critics as a moral pillar which need to be protected at any cost. Tupigeni madongo Tukae sawa.

Inawezekana.
 
Jina lake ni DAUDI BASHITE 100% na uhakika atoke apinge ntaomba chuo na sehem zote nilizosema wanivue elimu zangu kama atakanusha
 
Majina yake sisi hayatusaidii kitu ila makonda nikiongozi bora mtetezi wa wanyonge anatufaa full stop

No No No, not at all; wizi ni wizi na forgery is forgery, using someone's certificate so as to achieve or attain a particular 'post' is criminal. Kazi kwa mawaziri Kairuki, Simbachawene na Prof Ndalichako to iron out all irregularities and inform the President accordingly.
 
Paskal Mayala tupige vita madawa ya kulevya vijana wetu wanaangamia.Paul Makonda amepuliza tarumbeta kitu ambacho viongozi wengi kimewashinda.

Najua kila mmoja atatafuta taarifa za Makonda ili mradi tu ziwe ni za kumkatisha tamaa na hii ni tabia ambayo tumekuwa nayo sana watanzania pale anapojitokeza MTU kugusa maslahi yao.

Biashara hii INA mtandao mkubwa ndani na nje ya Serikali na wengi wakubwa hawajapenda pale Makonda alipolianzisha.

Kuhusu majina hilo ni personal Sina comment labda wenye taarifa.ila kwangu si la msingi sana maana hata Mimi najua kuna watu wengi tu wamesoma na majina ya watu wengine miaka ya nyuma ilikuwa kama kawaida toka primary.

La msingi kwangu mimi ni hii vita ya madawa ya kulevya lazima tupigame wote na tu support juhudi za Makonda na sio kuanza kuzizima kwa namna yoyote ile.
Upo sahihi wewe unaweza kukubali watu wakuseme uongo..

Jibu unalo katika nafsi yako vyovyote utakavyonijibu ni sawa!
 
Hakuna vita ya madawa bali kuna vita ya kudhibiti soko, hii ni vita ya magenge ya wauza dawa za kulevya kumalizana huku dola ikitumika bila kujijuwa.

Kuna wahusika siku wakitajwa tu hata wasipokamatwa ndio tutaamini ni kweli kuna hiyo vita dhidi ya dawa za kulevya na rehab zote zifungwe, unapojenga gereji maana yake unaingiza magari na yatahitaji matengenezo.

Mnaimport rizzla halafu mnajifanya mnapiga vits bangi, huu ni unafiki.
Amen mtumishi wa Mungu... hapo ulipo malizia pamegusa hisia zangh..

amen saana Mungu akubariki!
 
Paskali kila siku nakuambia weledi wa kupambanua mambo huna.

Hivi unadhani mtu akikanusha kitu ndiyo Inasaidia nini?

Kama kitu ni cha ukweli, na akikanusha unadhani nini kitabadilika? Kwaiyo acha kulikomalia suala la kukanusha.
 
Unatafuta uchochoro eeenh? Kwani shida ipo wapi? Zoezi la kuthibitisha hizi allegatins halichukui hata dakika moja
 
Unaleta habari ya vyeti ili tusahau ukwasi wake, je ni tajiri au anasingiziwa? Hata hii vita ya madawa ya kulevya naona kama sanaa iliyopangiliwa vizuri sana, leo unaitwa central, kesho mahakamani, keshokutwa unaachiwa hakuna ushahidi. Tunaishi kwa matukio na tunasubiri kwa hamu tukio litakalofuata angalao inatusaidia kusahau makali ya bei ya vyakula. Zidumu fikra za mwenyekiti wa Chama Chetu Makini!!
 
Huyu Makonda anapaswa kusimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili
1. Tuhuma za kushirikiana na wauza dawa za kulevya ambao inasemekana wanafadhili harakati zake
2. Mali nyingi zisizoendana na kipato chake anazotuhumiwa kumiliki
3. Tuhuma za kudanganya/kugushi vyeti/kutumia majina yasiyo yake kujiendeleza kitaaluma na kujipatia ajira serikalini.

Ili kuonyesha kuwa Mkuu wetu wa kaya ana dhamira ya dhati ya kukomesha ufisadi wa aina zote ikiwa ni pamoja kuwafagilia mbali makanjanja wa taaluma kupitia ukaguzi wa vyeti unaondelea serikalini, tunamuomba asimwache huyu "kijana wake" la sivyo madai kuwa anapendelea kabila lake na kushambulia makabila mengine yatakuwa na mashiko na hali hii ikiendelea itatupeleka mahali pabaya sana.
 
Upo sahihi wewe unaweza kukubali watu wakuseme uongo..

Jibu unalo katika nafsi yako vyovyote utakavyonijibu ni sawa!
Mamlaka zipo za kufanya kazi hiyo sisi tutapiga kelele tu.

Kama aipa mbele ya Rais kuwa Mkuu wa Mkoa baada ya Rais kuthibitishiwa na wataalam wake kuwa anaweza kushika nafasi ya mkuu wa mkoa wa Dar mimi na wewe zaidi wataalam wa Ikulu tunao waamini

Na kama Rais wa awamu ya Nne alithibitishiwa na wataalam wake wa Ikulu tunaowaamini wakati anateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni wewe na mimi ni nani wa kusema hayo.

Ina maana Mh Makonda ni zaidi ya Rais Magufuli au Rais mstaafu Kikwete mpaka aweze kujika kiasi hicho kwa wataalam wa Rais tunaowakubali mimi sidhani kama ni kweli katika hilo.
 
Back
Top Bottom