Baada ya Dkt. Stergomena Tax kuteuliwa Ubunge leo na Rais Samia Mawaziri mliopo jiandaeni Kisaikolojia kuna Mmoja wenu anaondolewa

Kipindi alichotawala Nyerere sidhani Kama kilikuwa chepesi kiasi hicho unachofikiri
Inategemea huo ugumu unautafsirije,kizazi cha Sasa JPM ni bora Zaid huyo Nyerere muache abaki na mwamvuli wa baba wa Taifa tu na kama kuna yaliyobora na kukuvutia Zaid tuambie
 
Kipindi alichotawala Nyerere sidhani Kama kilikuwa chepesi kiasi hicho unachofikiri
Wala kwa nyinyi vijana hamuwezi kukijua kipindi cha Nyerere tulipitia yepi. Kila kitu kilikuwa shida, Tulikuwa tunapanga foleni hata bila kujua maduka ya RTC yanauza nini. Siasa ya ujamaa na kujitegemea, tunamuomba Mungu asiturudishe tena kule tulikotoka.
 
Kama alienda huko kwa merits hakuna shida, tatizo ni kama alibebwa na CV ikatengenezwa kwakupitia mbeleko, hawa huwa shida sana maana hawawezi kujisimamia...Simfahamu vizuri wala siijui CV yake...Tumpe nafasi akibahatika...Nitamhukumu baada ya kuona kazi zake
 
Alipambwa sanaaa.mimi nikiona mwana taaluma yeyote amekubali teuzi, napiga mkasii katika orodha ya wana taaluma.

Sababu tanganyika hiii siasa za wateuaji ndio zita amua mteuliwa afanye nini
Kama nafasi zenye power ni uteuzi mwanataaluma atawezaje kujaribu kusaidia nchi yake pasipokupewa huo uteuzi? Na akikataa kabla hajaenda kuona atajuaje kama anadhibitiwa? All in all kuna weakness katika watu wetu, mbona wapo wanaofanya kazi nzuri tu?
 
Yule Mama Mulamula tuliambiwa ni bonge la diplomat..lakini hamna kitu..
Ukiangalia kwa umakini utagundua shida ni ile ile ya watu kujenga CV kwakusaidia siyo kwa juhudi zao...Wenye juhudi hawapenyi...So tunalaumu watanzania bali institution memory yetu ya tangu uhuru ni mbaya...
 
Hao ni vijana wasiotumia akili kufikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…