Baada ya Dkt. Stergomena Tax kuteuliwa Ubunge leo na Rais Samia Mawaziri mliopo jiandaeni Kisaikolojia kuna Mmoja wenu anaondolewa

Kipindi alichotawala Nyerere sidhani Kama kilikuwa chepesi kiasi hicho unachofikiri
Inategemea huo ugumu unautafsirije,kizazi cha Sasa JPM ni bora Zaid huyo Nyerere muache abaki na mwamvuli wa baba wa Taifa tu na kama kuna yaliyobora na kukuvutia Zaid tuambie
 
Kipindi alichotawala Nyerere sidhani Kama kilikuwa chepesi kiasi hicho unachofikiri
Wala kwa nyinyi vijana hamuwezi kukijua kipindi cha Nyerere tulipitia yepi. Kila kitu kilikuwa shida, Tulikuwa tunapanga foleni hata bila kujua maduka ya RTC yanauza nini. Siasa ya ujamaa na kujitegemea, tunamuomba Mungu asiturudishe tena kule tulikotoka.
 
Late Dr. Augusine Mahiga alipoingia Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alijaribu kuiweka nchi katika picha nzuri kwenye dunia. Baadae tukasikia anashindwa kwendana na JPM kwa hiyo akabadilishwa. Ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa nchi yetu kwa sababu Prof Kabudi kama waziri mpya hakuwa mwanadiplomasia zaidi ya kusifu na kuabudu maelekezo potofu na ya kishamba ya JPM. Kwa muktadha huo huo, Huyu Dr Tax pamoja na exposure yake hata akiwa waziri leo, bado atakutana na ukuta wa Rais wake na maelekezo ya CCM. CCM kumejaa uozo na incompetent figures. Atakwama. Hata hivyo huku SADC kulijaa Mugabeism, Lunguism, Zumaism...kwa hiyo hatakuwa na kipya. Mimi naamini zaidi viongozi waliopata exposure IMF, World Bank, UN, etc. Hawa wanaotoka EAC, AU, SADC, hawana jipya. Ni zao la mifumo ile ile ya rushwa, ukandamizaji, undemocratic na mangimeza. Mark my words.
Kama alienda huko kwa merits hakuna shida, tatizo ni kama alibebwa na CV ikatengenezwa kwakupitia mbeleko, hawa huwa shida sana maana hawawezi kujisimamia...Simfahamu vizuri wala siijui CV yake...Tumpe nafasi akibahatika...Nitamhukumu baada ya kuona kazi zake
 
Alipambwa sanaaa.mimi nikiona mwana taaluma yeyote amekubali teuzi, napiga mkasii katika orodha ya wana taaluma.

Sababu tanganyika hiii siasa za wateuaji ndio zita amua mteuliwa afanye nini
Kama nafasi zenye power ni uteuzi mwanataaluma atawezaje kujaribu kusaidia nchi yake pasipokupewa huo uteuzi? Na akikataa kabla hajaenda kuona atajuaje kama anadhibitiwa? All in all kuna weakness katika watu wetu, mbona wapo wanaofanya kazi nzuri tu?
 
Yule Mama Mulamula tuliambiwa ni bonge la diplomat..lakini hamna kitu..
Ukiangalia kwa umakini utagundua shida ni ile ile ya watu kujenga CV kwakusaidia siyo kwa juhudi zao...Wenye juhudi hawapenyi...So tunalaumu watanzania bali institution memory yetu ya tangu uhuru ni mbaya...
 
Hao ni vijana wasiotumia akili kufikiri
Hata taifa la Tanganyika halikuwepo achilia mbali Tanzania. Nchi ilikuwa mkusanyiko wa makabila zaidi ya 120 ambapo machifu walikuwa na mamlaka makubwa. Hatua za mwanzo kuchukuliwa ilikuwa ni pamoja na kupitisha sheria ya kufuta mamlaka ya machifu, matumizi ya kiswahili kwenye ofisi za serikali, kutaifisha shule ambazo nyingi zilikuwa za Wakatoliki (pamoja na Nyerere kuwa muumini mzuri tu wa dhehebu hilo), wafanyakazi wa serikali kutawanywa mikoa mbalimbali n.k. n.k. Lengo kuu lilikuwa kuua ukabila na kujenga umoja wa taifa. Haikuwa kazi rahisi hasa ukizingatia kuwa wakati huo wasomi walikuwa wachache sana wakihesabika kwenye kijanja cha mkono na wasienee. Ndugu yangu tumetoka mbali.
 
Back
Top Bottom