Baada tu ya Honeymoon anamkuta mume na mwanamke mwingine

Baada tu ya Honeymoon anamkuta mume na mwanamke mwingine

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,437
Binti wa rafiki yetu mpendwa amesoma vizuri na kupata ajira, alimuintroduce nyumbani boyfriend wake wa muda mrefu tangu yuko chuoni. Kijana maridadi sana, anaheshima, mstaarabu, kwakweli rafiki yetu alikua anatuambia asingependa mwanae aolewe na mtu mwingine yeyote zaidi ya kijana huyu. Binti mwenyewe alikua anamwambia mama yake, "mama sijui kama nitauweza usafi wa yule mwanaume".

Dating yao kabla ya harusi, kijana hakumruhusu binti wa watu akae nje ya nyumba yao mpaka Zaidi ya saa mbili usiku. Ikitokea sherehe atakuja kuomba kwa wazazi na atamrudisha mtoto wa watu kabla ya saa nane usiku. Wazazi walimwaga sifa nyingi sana kwa wazazi waliomlea yule kijana.

Harusi ilifika tukasherehekea, baada ya harusi maharusi walikwenda honeymoon Visiwa vyo Comoro. Binti alikua anategemewa sana kazini kwake na kutokana na sababu nyinginezo Boss wake alimpa likizo ya wiki mbili tu kwaajili ya harusi wakati kijana alipewa mwezi mzima likizo na mwajiri wake, hivyo baada tu ya honeymoon binti alianza kazi wakati kijana bado yuko likizo.

Mapenzi mapya tena basi siku moja binti akiwa kazini aliamua arudi nyumbani kuenjoy siku na mume mpya. Aliamua kumsurprise jamaa.Alirudi akafungua mlango wa mbele taratibu, akaingia sitting room, hakuna mtu, lakini kulikua na glass na vinywaji design kama jamaa alikua na mgeni, basi bi harusi wetu akanyata mpaka chumbani, aliyoyakuta huko ilibidi akimbie, mume anapumuliwa na mwanaume mwenzie. ndoa ilifia hapo.
 
duh....kama ni kweli basi ni hatari tupu......kwa hali ya sasa.....
 
Sky Eclat leo una story nyingi, lakini kipaji cha kutunga hadithi unacho, hongera!
 
Last edited by a moderator:
Mmmh! Hii ni hatari sana, yaani hapa sipati picha genye zilivyomwishia ghafla binti wa watu hadi kutoka kazini mapema
 
Nasubiri nijue mwisho ilikuaje!?
Afu usafi unahusikaje!? make mi ni msafi pia.
 
Ptuuu..! Uchafu mwingine hata haufai kuweka kwenye ubongo.
 
thread zako nyingi zimekaa kishigongo shigongo, sio mbaya lakini, mradi siku zinaenda
 
Back
Top Bottom