OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,090
- 114,627
Kutokana na hali ya kukosekana kwa mvua katika sehemu nyingi inatazamiwa kukosekana kwa chakula katika sehemu nyingi.
Mpaka Chrissmas hii bado hali ya mvua haieleweki na mazao yaliyochipua yameanza kukauka. Kama hali itaendelea kuwa hivi ni dhahiri kwamba familia nyingi hasa za wakulima zitakumbwa na baa la njaa.
Ikumbukwe kwamba wahanga wa tetemeko la Bukoba walipoonyesha kuitrgemea serikali kwa malazi na chakula walionywa kuwa serikali haikuleta tetemeko hivyo wajifunge mkanda na kujipigania. Pia wahanga wa mvua ya mawe wilayani Kahama walipewa taarifa katika ziara ya Mh.Rais kwamba serikali haitawajengea nyumba kama ilivyoahidi katika awamu ya NNE
Kwa dalili hizi za baa la njaa(Mungu tuepushe) je tutegemee nini kwa serikali?Je,tujifunge mikanda kwa kuwa serikali haijazuia mvua kama ambavyo haikuleta tetemeko huko Bukoba?