Baa la Njaa: Rais Magufuli, Serikali haijazuia mvua?

Nyie ni washirikina wakubwa. Mnaamini mambo ya kijinga kabisa. Mwenye mamlaka ya kuleta na kuzuia mvua ni Mungu pekeee
Kama umekariri kua Mvua ndio chanzo cha maji pekee watu wanachoweza kukitumia kulima basi iko kazi kubwa sana,
 
Kiukweli mtukufu sehem nyingine anakosea sana maana njaa aina mgambo police mwanajeshi wala commando na kuusu Chakula NFRA haikupewa fungu la kutosha...Na RC atakaeomba Chakula cha msaada kazi hana...kauli ya mtakatifu
 
Kutokana na hali ya kukosekana kwa mvua katika sehemu nyingi inatazamiwa kukosekana kwa chakula katika sehemu nyingi.
Mpaka Chrissmas hii bado hali ya mvua haieleweki na mazao yaliyochipua yameanza kukauka. Kama hali itaendelea kuwa hivi ni dhahiri kwamba familia nyingi hasa za wakulima zitakumbwa na baa la njaa.

Ikumbukwe kwamba wahanga wa tetemeko la Bukoba walipoonyesha kuitrgemea serikali kwa malazi na chakula walionywa kuwa serikali haikuleta tetemeko hivyo wajifunge mkanda na kujipigania. Pia wahanga wa mvua ya mawe wilayani Kahama walipewa taarifa katika ziara ya Mh.Rais kwamba serikali haitawajengea nyumba kama ilivyoahidi katika awamu ya NNE

Kwa dalili hizi za baa la njaa(Mungu tuepushe) je tutegemee nini kwa serikali?Je,tujifunge mikanda kwa kuwa serikali haijazuia mvua kama ambavyo haikuleta tetemeko huko Bukoba?
Tuangalie ile option ya kuzalisha mvua. Sio far fetched kama tunavyofikiri. Merry xmas
 
Kwa hali inavyoenda huenda kukawepo na upungufu mkubwa wa chakula, ukame umezidi kwa kweli
Hali imeanza kuwa mbaya. Kwa mfano Morogoro moja ya mikoa iliyozoeleka kama food basket of the nation, tayari wameanza kupatwa na tatizo la uhaba wa chakula. Kuna ukweli kwamba moja ya sababu kubwa ni mabadiliko ya tabia nchi lakini ni muhimu tukatambua pia kwamba sera mbovu chini ya serikali pia ni sababu nyingine kubwa katika hili. Bado hatuna mfumo mzuri unaoangalia maslahi ya wazalishaji. Kwa mfano nchi za wenzetu zilizopiga hatua, huwa ni Jambo la kawaida kwa serikali kununua mazao ya vyakula kwa bei zenye tija kwa wazalishaji hata kama uzalishaji unakuwa mkubwa kuliko mahitaji ya nchi. Serikali hizi huwa zipo tayari hata kutupa ziada hii kama sio kuipeleka nje au kuigawa umoja wa mataifa (WFP) ili mradi mzalishaji wa nyumbani asife moyo kuzalisha, hivyo kufanya taifa kuwa na "food security."

Kwetu mkulima akiuza kwa serikali anapewa hati garani badala ya Fedha taslimu. Akitaka kujiongezea rizki kwa kuuza mipakani au nchi jirani, wakuu wa wilaya kazi yao ni kuzuia hilo. Ukitazama kiasi cha fedha zinazotengwa kibajeti kwa ajili ya sekta hii ni masikitiko matupu. Sekta ya kilimo ndio inayoongoza katika kutupatia fedha za kigeni (ingawa kwa sasa inashindana vikali na sekta ya utalii). Sekta hii ndio sekta mama ya uchumi wa taifa kwa maana ya kulisha taifa na pia kutoa mali ghafi kwa viwanda vyetu. Lakini uzito huu hauendani kabisa na mikakati ya serikali kuhakikisha kwamba mapato ya kodi yanaenda huko kwa wingi. Hata ukitizama mikopo ya serikali (deni la taifa) kutoka nje, ni kiasi kidogo sana kinaelekezwa kwenye sekta ya kilimo. Lakini ni wakulima hao hao ndio wanatarajiwa kulipa sehemu kubwa ya mikopo hii. Nk. Nk.

Matokeo yake ni mzalishaji kuvunjika moyo na kupunguza kasi ya uzalishaji.

Tuendako:
Wananchi wataanza kufa njaa lakini kwa vile DCs wameshaambiwa kwamba 'tusisikie watu wanalalamila njaa kwako', wakuu hawa watakaa kimya kuogopa kutumbuliwa. By the time hatua za maana zinakuja chukuliwa na serikali kuu, hali itakuwa imeshafikia pabaya. Kwa watu wa mijini, hasa DSM, hili halitaonekana mapema kwa sababu most food inapelekwa huko. Wataanza kufikwa kwanza na mfumuko wa bei bidhaa za vyakula na baadae ndio uhaba utawakumba. Kipindi cha 2017-18 kitakuwa ni kigumu sana kwa watanzania.
 
Mwaka ujao kutakuw na njaa sana. Hadi leo hii katika pita pita yangu mitaani mazao yamedhoofika na kuanza kukauka. Tumuombe Mungu atuepushe na baa la njaa maana tutakwisha
 
Kwanza lazima upite UHAKIKI wa wenye njaa feki
Utachukua miezi sita,watakao kuwa hai watapata msaada wa kilo tano tano za mahindi makavu
 
Punguzeni fitna, unafik na kunyoosha vidole ......jiulize ww utajipangaje kukabili baa hilo la njaa....ama unasubiri serekali ikubebe kama mtoto mdogo ...
fitna iko wp hapoo??...anyways yawezakua uko kweny chain lazma utetee
 
Kwa mtazamo wangu, kwa mustakabali wa maendeleo ya kiuchumi kwa wote hasa ktk nchi yetu kilimo ktk subsistance level lazma kipewe support na serikali.

Ila kuondokana na madhara ya kukosa chakula kutokana na ukame serikali lazima ishawishi wafanya biashara wakubwa waingie ktk kilimo kutokana na uwezo wao mkubwa wa mitaji watazalisha kwa wingi na kwa ubora
 
Ni moja ya mapigo Tisa ya Mungu kwa Watanzania baada ya kulikataa JIWE KUU LA PEMBENI.Njaa ni pigo la kwanza bado nane yanakuja.Stay tuned, usipoguswa na njaa utaguswa na mengine yanayokuja.
Sijawahi kuona raia wa inchi wakuombea mabaya inchi yao. Huu ni uzuzu kweli unazani hayo mabaya yakitokea ndio kutakufanya wewe uishi maisha mema. Acheni siasa mjue mtu anayeombea mabaya mtu au taifa ni kumuombea aishi maisha marefu ili Mungu amuonyeshe jinsi unavyofanikiwa ama inchi itakavyopiga hatua. Hayo mabaya yasikatishe tamaa serikali iendelee kufanya kazi kwa juhudi zaidi.
 
Japo kuwa mm sijawahi kuwa rais ila najua mtu unapo kuwa rais na unapo zungumzia mwaswala ya nchi inabidi uongee kitaalamu au uwaache wataalamu wa hiyo sekta wanzungumze ila sio kuongea kama mshilikina.

Kuhusu swala mvua rais ilibidi awahasishe wananchi wake kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kwamba tuyatunze amazingira ili nayo yaje yatutunze.
 
kwenye mvua hapo hapo mungu ameweka vikwazo sbb nchi imeminya demokrasia!bado na wazungu
 
Hakuna fitna na unafiki kuzungumzia ukweli kuhusu hali halisi ya nchi yetu. Serikali ndiyo inatakiwa iwe mstari wa mbele kuwatoa hofu wananchi kuhusu uwezekano wa kuwepo balaa la njaa na kuwahamasisha nini kifanywe badala ya Mtanzania mmoja mmoja kuamua mwenyewe kipi afanye. Kuna umuhimu gani basi wa kuwa na Serikali ambayo inaona nchi inanyemelewa na balaa la njaa halafu inakuwa kimya!? Acha hizo Mkuu!

Punguzeni fitna, unafik na kunyoosha vidole ......jiulize ww utajipangaje kukabili baa hilo la njaa....ama unasubiri serekali ikubebe kama mtoto mdogo ...
 
Hivi waliotangaza kuwa maisha ni magumu sana mabasi yamepaki hamna abiria wa kusafiri, wanajisikiaje kuona watu wamekosa mabasi ,na wengine wakidandia coaster kwa nauli mara mbili.

Aibu ya kufungia mwaka hii.
Wewe mwenyewe unapumlia mashine halafu unajifariji na thread za ajabu ajabu hapa. Hivi mtu asiyeona ugumu Wa maisha kwa sasa anafanya makusudi au ametumwa na WALE...!!
 
Hali imeanza kuwa mbaya. Kwa mfano Morogoro moja ya mikoa iliyozoeleka kama food basket of the nation, tayari wameanza kupatwa na tatizo la uhaba wa chakula. Kuna ukweli kwamba moja ya sababu kubwa ni mabadiliko ya tabia nchi lakini ni muhimu tukatambua pia kwamba sera mbovu chini ya serikali pia ni sababu nyingine kubwa katika hili. Bado hatuna mfumo mzuri unaoangalia maslahi ya wazalishaji. Kwa mfano nchi za wenzetu zilizopiga hatua, huwa ni Jambo la kawaida kwa serikali kununua mazao ya vyakula kwa bei zenye tija kwa wazalishaji hata kama uzalishaji unakuwa mkubwa kuliko mahitaji ya nchi. Serikali hizi huwa zipo tayari hata kutupa ziada hii kama sio kuipeleka nje au kuigawa umoja wa mataifa (WFP) ili mradi mzalishaji wa nyumbani asife moyo kuzalisha, hivyo kufanya taifa kuwa na "food security."

Kwetu mkulima akiuza kwa serikali anapewa hati garani badala ya Fedha taslimu. Akitaka kujiongezea rizki kwa kuuza mipakani au nchi jirani, wakuu wa wilaya kazi yao ni kuzuia hilo. Ukitazama kiasi cha fedha zinazotengwa kibajeti kwa ajili ya sekta hii ni masikitiko matupu. Sekta ya kilimo ndio inayoongoza katika kutupatia fedha za kigeni (ingawa kwa sasa inashindana vikali na sekta ya utalii). Sekta hii ndio sekta mama ya uchumi wa taifa kwa maana ya kulisha taifa na pia kutoa mali ghafi kwa viwanda vyetu. Lakini uzito huu hauendani kabisa na mikakati ya serikali kuhakikisha kwamba mapato ya kodi yanaenda huko kwa wingi. Hata ukitizama mikopo ya serikali (deni la taifa) kutoka nje, ni kiasi kidogo sana kinaelekezwa kwenye sekta ya kilimo. Lakini ni wakulima hao hao ndio wanatarajiwa kulipa sehemu kubwa ya mikopo hii. Nk. Nk.

Matokeo yake ni mzalishaji kuvunjika moyo na kupunguza kasi ya uzalishaji.

Tuendako:
Wananchi wataanza kufa njaa lakini kwa vile DCs wameshaambiwa kwamba 'tusisikie watu wanalalamila njaa kwako', wakuu hawa watakaa kimya kuogopa kutumbuliwa. By the time hatua za maana zinakuja chukuliwa na serikali kuu, hali itakuwa imeshafikia pabaya. Kwa watu wa mijini, hasa DSM, hili halitaonekana mapema kwa sababu most food inapelekwa huko. Wataanza kufikwa kwanza na mfumuko wa bei bidhaa za vyakula na baadae ndio uhaba utawakumba. Kipindi cha 2017-18 kitakuwa ni kigumu sana kwa watanzania.
Ni sahihi kabisa nchi inalegalega kusaidia wakulima hasa pale ambapo hali ya hewa ni nzuri bado tuna tatizo kubwa la uongozi kuanzia juu mpk chini. Lkn kwa kipindi cha ukame uliokithiri kama hiki kwa nchi inayotegemea hali ya hewa lawama zinapungua sababu ni beyond their power.
 
Back
Top Bottom