Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?

BAK.. unanielewa vibaya kabisa. Mimi sipingi uraia wa nchi mbili at all.. napinga kanuni zinazopendekezwa. Hatuwezi kubadilisha nature ya uraia wetu kwa sababu ya rangi, nasaba, hali ya kiuchumi, kufuata mtindo n.k.. we have to articulate proper arguments why we have to change.. siyo nchi zote duniani zinaruhusu uraia wa nchi mbili hata zile za kiafrika au za kimagharibi. Sielewi kwanini tuonekane tunafuata zile za nchi fulani na zile za nchi nyingine tuone hazifai.

Mwanakijiji na wengine,
Hapa nakubaliana na nyie kuwa ni heri kuruhusu uDC kwa watu wa kawaida. Waweke mipaka kwa watu wa juu tu ambao itakuwa ni rahisi hata kuwachunguza. Sasa hivi kusema eti usalama wa taifa uje uchungeze kama mie hapa nina uraia wa nchi mbili, itakuwa kichekesho.

Ila kama watapunguza idadi na kubaki wanachunguza wale wa juu tu, itakuwa hata ni rahisi kufanya huo uchunguzi. Kwa nini tuwe na sheria nchini ambazo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wala hawawezi kufuatilia? Kibaya zaidi ni kuwa watawabana masikini na waaminifu ila wenye pesa zao na "mabaharia" wataendelea kudunda kama kawaida.
 
Si kweli,i beg to differ,nadhani watanzania wenye uraia wa nchi mbili ni hao mabalozi wanaoiwakilisha nchi huko middle east,nje ya hapo si watanzania tena,rather ni "waliokuwa watanzania" ambao sasa ni raia wa nchi nyingine,mfano huyo wa nchi ya Scandnavia,yeye si mtanzania tena,however angeweza kuwa mtanzania kama angepelekwa huko middle east ama kama sheria ingebadilishwa.
Like I said, usinichokonoe zaidi. Lakini Watanzania wenye uraia wa nchi mbili ni reality.
 
Like I said, usinichokonoe zaidi. Lakini Watanzania wenye uraia wa nchi mbili ni reality.

No,kuna waliokuwa watanzania ambao sasa wana uraia wa nchi nyingine na si uraia waTanzania tena,nadhani wanaweza wakawa na uraia wa nchi mbili,say US and UK,lakini si watanzania tena.
The only time tumeweza kuona kuna uwezekano wa kuwa mtanzania mwenye uraia wa nchi mbili "kihalali" Yani kwa maana nyingine mtanzania usiyekuwa raia wa Tanzania ni hao mabalozi wa middle east.
Inategemea in which angle you're trying to look at it....Nakubaliana na "Reality" unayoizungumzia ambayo "Kihalali" iko only in the middle east tho,nikiwa na maana ya raia asiyekuwa raia kukubalika na serikali regardless to wether sheria imevunjwa kwenye issue nzima ya asiyekuwa raia kisheria kuiwakilisha nchi "Kihalali"
 
No,kuna waliokuwa watanzania ambao sasa wana uraia wa nchi nyingine na si uraia waTanzania tena,nadhani wanaweza wakawa na uraia wa nchi mbili,say US and UK,lakini si watanzania tena.
The only time tumeweza kuona kuna uwezekano wa kuwa mtanzania mwenye uraia wa nchi mbili "kihalali" Yani wasiokuwa watanzania(kwa upande mwingine)ni hao mabalozi wa middle east.
Inategemea in which angle you're trying to look at it....Nakubaliana na "Reality" unayoizungumzia only in the middle east tho,nikiwa na maana ya kukubalika na serikali regardless to wether sheria imevunjwa ama la.
jmushi1,
Ninachosema ni kwamba tukienda DSM sasa hivi kuna Watanzania ninawafahamu wanazo pasipoti mbili. Bado wanashikilia uraia wa Kitanzania wakati wameshachukua uraia wa Marekani, Canada, etc. That's all.
 
jMushi1

Mkuu usibishe kitu ambacho hufahamu. Mimi binafsi nawafahamu wabongo wengi tu wana uraia wa UK, South Afrika, USA nk. hao wote bado wana passport za bongo na wanadunda tu tena usifikirie ni watu wenye hadhi za ubalozini au mawaziri etc. watanzania wa kawaida kabisa na wewe ukiambiwa utabisha. Dunia tambala bovu halikawii kuchanika.
 
Fuatilia mjadala na uelewe pointi yangu,hao si wabongo tena kisheria.
 
jmushi1,
Ninachosema ni kwamba tukienda DSM sasa hivi kuna Watanzania ninawafahamu wanazo pasipoti mbili. Bado wanashikilia uraia wa Kitanzania wakati wameshachukua uraia wa Marekani, Canada, etc. That's all.

Sawa lakini hao si "Halali" Kisheria,si raia wa Tanzania.
 
hapa ndiyo tatizo la uraia wa nchi mbili labda pia litaonekana. Je, tuko tayari rais wetu awe ni raia wa Tanzania na Kenya at the same time? au wa Rwanda na TZ at the same time au nchi nyingine yoyote? Vipi kuhusu Ubunge, Uwaziri, Ukuu wa Jeshi, vyombo vya usalama n.k?
Kuna ubaya gani kuhakikisha sheria zionyesha wazi kazi ambazo watu wenye uraia wa nchi mbili wanaweza kufanya?
 
Kuna ubaya gani kuhakikisha sheria zionyesha wazi kazi ambazo watu wenye uraia wa nchi mbili wanaweza kufanya?

kwa kweli hamna; binafsi ningependekeza viongozi wote wanaotajwa kwenye sheria ya Maadili ya Umma wasiruhusiwe kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja na kama waliwahi kuwa nao wawe wameukana angalau miaka mitano iliyopita..
 
Nafikiri hii kazi ya kuwakamata wanaodanganya ni wajibu wa serikali. Idara husika hapa watakuwa wamechemsha mno na kama tuko serious yaani mhusika wa hiyo idara hata angepoteza kazi.

Sasa Tz itakamata wangapi for this, mana leo hii kati ya watu milioni 42 wanaoishi Tz hatujui yupi ni raia wa Tz na yupi si raia!! Au unamaana tukamate watu kwa kuwapa post ya ubalozi kwanza!!!
 
BAK.. unanielewa vibaya kabisa. Mimi sipingi uraia wa nchi mbili at all.. napinga kanuni zinazopendekezwa. Hatuwezi kubadilisha nature ya uraia wetu kwa sababu ya rangi, nasaba, hali ya kiuchumi, kufuata mtindo n.k.. we have to articulate proper arguments why we have to change.. siyo nchi zote duniani zinaruhusu uraia wa nchi mbili hata zile za kiafrika au za kimagharibi. Sielewi kwanini tuonekane tunafuata zile za nchi fulani na zile za nchi nyingine tuone hazifai.

Hatufuati nchi yoyote ile Mkuu Mkjj bali ni kwenda na wakati. Nchi nyingi sana zinaona faida kubwa ya kuwashirikisha katika ujenzi wa nchi zao raia wanaoishi nchi za nje ambao tayari wana uraia wa nchi nyingine, hivyo sioni sababu zozote zile za Tanzania kusubiri kuwa nchi ya mwisho katika Afrika kufanya hivyo. Wenzetu wa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi etc wameshafanya hivyo sijui sisi tunangoja nini!

Leo kijana wa kibongo ambaye wazazi wote ni Wabongo akija kupata nafasi kubwa US au UK wote tutataka kumkumbatia kwamba yule ni Mbongo mwenzetu...lakini hapo hapo Serikali haioni umuhimu wa kuruhusu uDC eti hivi sasa hili si moja ya mambo ambayo yana priority nchini....hivi Tanzania tuna priorities zozote!? Ni zipi!? za kulinda mafisadi!? Labda litakuwa ni priority mwaka 3050.
 
jmushi1,
Ninachosema ni kwamba tukienda DSM sasa hivi kuna Watanzania ninawafahamu wanazo pasipoti mbili. Bado wanashikilia uraia wa Kitanzania wakati wameshachukua uraia wa Marekani, Canada, etc. That's all.

Sio lazima mpaka uende man. Wataje hata hapa tu kwani shida iko wapi?
 
Ooh jamani,ameukosa hivi hivi!sasa kama sababu ni hizo hilo pemdekezo lilitokaje wakati hakuwa na sifa?

Ni kwa sababu ya Tanzania kutokua na data base ya wananchi wake! Najua hili si tatizo la Tanzania peke yake, lipo na nchi zingine, lakini haina maana kuwa ni sawa.

Serikali ingeweza kuanza tu kwa kuingiza kwenye data base wananchi wote wenye hati za kusafiria na hiyo data base iwe updated mara kwa mara (si kama website zao!)

Basi tunaonekana wajiiinga! Aibu!
 
Poland kwa sasa wanaruhusu mtu kuchukua uraia wa nchi mbili.

Ila huyo bwana Sikorski alikuwa na wa British na Poland na alipochaguliwa kushika nyadhifa kubwa, ilibidi wamnyan'ganye uraia wa British. Maana ingelikuwa kichekesho kama leo hii alivyo, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Poland na pia ni Raia wa Uingereza.

Poland wanakitu kimoja kuwa kila raia wao anapewa Identity Card. Nilikutana na Mmoja ambaye kachukua uraia wa Tanzania na hivyo alirudisha passport ya Poland ila bado ana Kadi yake ambayo akiingia tu ndani ya Schengen, basi anaweza kuficha Pass ya Tanzania na akawa anatesa na hiyo Kadi yake.

Kwa faida ya WAZAWA, mtu anayerudisha Passport, anaweza kupewa Kadi ambayo itaruhusiwa kutumika mpakani mwa Tanzania. Hivyo, kama mtu anataka kwenda kuchakalika, basi anaweza kuchukua Passport mpya na kurudisha ya Tanzania. Akichoka kuishi huko, anaweza kurudi na kuomba Passport yake upya na ile ya ugenini wanaichukua na kuirudisha kwa wenyewe.
Mie walininyang'anya Driving Licence ya Tanzania na kuipeleka Berlin. Sijui iko pale au walishairudisha Tanzania? Unakuta wakati mwingine hata hawafahamu waifanye nini pale ubalozini. SIntashangaa nikisikia walilitupa maana hata muda wake umeisha.

Du hata driving leseni walikunyang'anya, sasa gaba la kijani si walilisaka sana? teh teh teh teh teh.
 
Du hata driving leseni walikunyang'anya, sasa gaba la kijani si walilisaka sana? teh teh teh teh teh.

Mkama, kama ningelikuwa nimeomba gamba lao, basi tungelikurupushana na ofisi ya Rais wa hapa hadi waniruhusu niwe na zote mbili. Wakikataa unagoma kuchukua na unaomba tena hapohapo. Mwisho wanachoka na kusema "mpe mpingo hilo gamba asitusumbue tena" na mchezo unakuwa umeisha. Ukisikia watu wanalaani DC, na wewe unajifanya unalaani sana kumbe mhhh!!!!!!
 
teh teh teh
kwa hiyo unamaana watu wanaochonga sana humu ndio wana miliki hayo magamba mawili nini?

gamba kitu gani zile page tu za karatasi , huyo jamaa wa-swidish wamemzibia tu ,jamaa kavumilia kuchuma strobeli na wakati anajisomea kajipatia donge, sasa waswidish wanambania wanataka aendelee kuchuma strobeli tu.

Unajuwa wazungu nao waongo kinoma wanachonga sana .teh teh teh teh teh
 
Hatufuati nchi yoyote ile Mkuu Mkjj bali ni kwenda na wakati. .

sidhani kama hii peke yake inatosha kuwa sababu; maana tukifuata yanayofanywa na nchi nyingine "zinazokwenda na wakati" tunaweza kufuata mambo mengi kweli. Kuna mambo ambayo sisi wenyewe ni lazima tuyafikiri na kuyaamua kwa nia yetu sisi wenyewe.

Lakini kwenye suala la UN2 hatuwezi tu kutoka na kusema every one go!! hakuna sehemu duniani ambao wamefanya hivyo, kila watu wana utaratibu wao na sababu zao. Sisi wa kwetu uweje? hilo ndilo swali au hutaki hata tufikirie tufanye vipi turuhusu tu alimradi tumeruhusu bila kufikilia masuala mbalimbali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom