DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,470
Nafikiri hizi stori za Aziz Ki kuuzwa Wydad tuzizike rasmi na tuachane nazo.
Yanga haijawahi kutaka kumuachia Aziz Ki na kitendo cha aliyekuwa kocha wa Mamelodi, Rulani Mokwena kumsogeza na kuanza "kumnong'oneza" baada ya ile mechi ya robo fainali kati ya Mamelodi na Yanga ilichukuliwa kama ishara ya dharau kwa Yanga na ikawapa hasira, kiburi na kisingizio cha kuapa kwamba hawatakuja kumuuza kwa Mamelodi au popote pale Mokwena atakapokuwa.
Harakati za kumuozesha kwa Hamisa Mobetto zilikuwa zina nia hiyo hiyo ya kumnasa katika tundu bovu. Sasa hivi Aziz Ki anajinenepea tu, hana habari za Club World Cup wala nini.
Mokwena mwenyewe amekalia kuti kavu huko Wydad, muda wowote kibarua chake kinaota nyasi.
Ninachoona siyo tu Yanga wamekwepakwepa fursa za kumuachia Aziz Ki kwa Wydad, ila pia wametoa masharti magumu yasiyotekelezeka ili tu dili lijifie. Kiufupi wanataka wapigiwe magoti huku wakiwa na dhamira ya dhati ya kutomuuza.
Club World Cup inaanza mwezi June, Wydad hawawezi kumnunua mchezaji kwa pesa ndefu na kutekeleza masharti ya kiduwanzi wanayopewa na Yanga halafu wategemee kumuandaa kwa wiki mbili tu kabla ya mashindano makubwa kama ya CWC kuanza na wakati huo huo anayetaka kumleta wanataka kumtimua muda wowote.
Tufunge stori za Aziz Ki. Huyu tupo naye hapa hapa hadi kiama.