Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,590
- 8,726
Hakuna hata sera moja ya Nyerere ambayo inatumika TZ sasa hivi.
Nyerere VS Mwinyi
Socialist Free Market
Dictator Democracy
Kwa hiyo Azimio la Arusha ni HISTORY. Ni Sera ambazo zilishapitwa na wakati. " Hatutarudi kwenye Ujamaa" Mwinyi. Ni Capitalism na sera za Mwinyi ndizo zilizoshinda.
FMEs heshima mbele mkuu,
NAdhani unaposema kuwa azimio lilishapitwa na wakati unakosea, kwani hayo maadili ya viongozi unayotaka tuyajadili kama taifa tunaweza kuyaona hapa:
(a) The Leadership
1. Every TANU and Government leader must be either a peasant or a worker, and should in no way be associated with the practices or capitalism or feudalism.
2. No TANU or Government leader should hold shares in any company.
3. No TAN U or Government leader should hold directorships in any privately owned enterprise.
4. No TANU or Government leader should receive two or more salaries.
5. No TANU or Government leader should own houses which he rents to others.
6. For the purposes of this Resolution the term leader should comprise the following:
Members of the TANU National Executive Committee; Ministers; Members of Parliament; senior officials of organizations affiliated to TANU; senior officers of par-statal organizations; all those appointed or elected under any clause of the TANU Constitution; councilors; and civil servants in the high and middle cadres. (In this context leader means a man, or a man and his wife; a woman, or a woman and her husband.)
Maoni yangu, tunaweza kubadilisha baadhi ya vifungu katika azimio ili liendenane na wakati huu, then tatizo la maadili tunaweza kulisolve kwa kiasi fulani.
Mkuu wa idara FMES,
Wewe ndio unaniachaga hoi kabisaa, yaani kila kitu kumlaumu mwalimu tuu, kwani unafikiria Azimio la Arusha (AA) liliandaliwa na mwalimu peke yake?
Hii tabia ya kumlaumu mwalimu kwa kila kitu itaisha lini jamani? Unaijua hadithi ya Karumekenge ambaye hakutaka kwenda shule na akawa anausingizia umande!
Amani.
Mkuu wa idara ZAKUMI,
Nadhani sasa wewe ndio unaeongea crap! hakuna anayesema Azimio ndio substitute ya utawala wa sheria! bali tunachosema Azimio ni muhimu kwa kuwa nchi inakuwa na malengo yanayoeleweka sio kama sasa hivi ambapo hatuna mwelekeo wowote ule. Hata hayo mataifa ya mabepari wakubwa bado wana maazimio yao ambayo daima yanawaongoza.
Halafu unanishangaza unavyowasema wachina huoni kuwa bila ya maazimio yao wasingekuwa hapa walipo leo?? walichofanya ni kurekebisha zile sehemu ambazo haziendi na wakati na sio kuachana na maazimio yao kabisa na matokeo unaona mda mfupi ujao wao ndio watakuwa the world next biggest superpower!
Amani.
Mkuu wangu maelezo yako yote yanashambulia Azimio la Arusha pasipo kufikiria kwamba SHERIA inatakiwa kusimama vile vile.. Huwezi weka sheria mahala pasipo kuwa na AZIMIO na huwezi kutekeleza Azimio kama hakuna SHERIA..Azimio la Arusha ni pure crap. Matatizo yako ni kuwa ujalisoma mpaka mwisho na kuelewa implications zake katika maisha yako.
Kutokana na viongozi wengi kukiuka maadili ya uongozi, watu wanaona kuwa Azimio la Arusha ni silaha ya kuweka sawa maadili ya uongozi. Lakini ukweli wa mambo, Azimio linagusa mambo mengi yakiwemo ya kiuchumi ambayo hayatumii principal za uchumi. Hivyo basi kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayokabili jamii za kiAfrika, utakuwa na machaguo mawili tu. Utumie sehemu ya azimio hilo au tafuta something new.
Ngoja nikupe mifano. Kwa maneno ya Chifu Kunambi. Anasema kuwa safari ya Nyerere UNO ilichangiwa na wananchi. Na kabla ya safari pesa zilikuwa hazitoshi. Rupia ikabidi akate pesa na akaonekana shujaa.
Azimio la Arusha lilipotangazwa, mmoja wa watu wa mwanzo kuona athari zake alikuwa Rupia kwa sababu mali zake zilikuwa tayari ni unyonyaji.
Mwamwindi tayari alikuwa ni mwekezaji mzawa ambao kwa sasa hivi watu kama hao tunawatafuta kuwekeza kwenye kilimo.
Moja ya matunda ya ujamaa ni benki za umma. Nyerere alikopa pesa kujenga nyumba yake ya Msasani. Na kwa maneno yake mwenyewe alishindwa kulipa. Kama rais wa nchi anashindwa kutumia Azimio la nchi kujiendeleza ni nani anayeweza ?
Pure Crap? Pengine ni kwa akina Zakumi! Umelisoma lakini hukuelewa yaani umesoma kama kasuku.Azimio la Arusha ni pure crap. Matatizo yako ni kuwa ujalisoma mpaka mwisho na kuelewa implications zake katika maisha yako.
Kutokana na viongozi wengi kukiuka maadili ya uongozi, watu wanaona kuwa Azimio la Arusha ni silaha ya kuweka sawa maadili ya uongozi. Lakini ukweli wa mambo, Azimio linagusa mambo mengi yakiwemo ya kiuchumi ambayo hayatumii principal za uchumi. Hivyo basi kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayokabili jamii za kiAfrika, utakuwa na machaguo mawili tu. Utumie sehemu ya azimio hilo au tafuta something new.
Ngoja nikupe mifano. Kwa maneno ya Chifu Kunambi. Anasema kuwa safari ya Nyerere UNO ilichangiwa na wananchi. Na kabla ya safari pesa zilikuwa hazitoshi. Rupia ikabidi akate pesa na akaonekana shujaa.
 Azimio la Arusha lilipotangazwa, mmoja wa watu wa mwanzo kuona athari zake alikuwa Rupia kwa sababu mali zake zilikuwa tayari ni unyonyaji.
 Mwamwindi tayari alikuwa ni mwekezaji mzawa ambao kwa sasa hivi watu kama hao tunawatafuta kuwekeza kwenye kilimo.
Moja ya matunda ya ujamaa ni benki za umma. Nyerere alikopa pesa kujenga nyumba yake ya Msasani. Na kwa maneno yake mwenyewe alishindwa kulipa. Kama rais wa nchi anashindwa kutumia Azimio la nchi kujiendeleza ni nani anayeweza ?
FMES,
Lakini mkuu wangu huwezi kutunga sheriua kama hakuna ustaarabu fulani uunaotangulia hizo sheria. Kwa mfano huwezi weka sheria za madereva wabaya ikiwa hakuna utaratibu wa kuendesha magari hayo, hakuna alama za barabani, hakuna sheria za vyeti kwa madereva na kadhalika.
Kinachoombwa hapa ni kama vile leo hii Tanzania nzima inaendeshwa na amri ya Lowassa kuruhusu magari kwenda upande mmoja kulingana na traffic iliyopo (Azimio la Zanzibar)..Hali ambayo imesababisha kuvunjika kwa sheria zote za barabarani na huwezi kuzi apply hata kidogo..Imefikia kiasi kwamba kila kona inatakiwa askari kuongoza magari badala ya taa za traffic au alama za barabani bado wewe unajaribu kutueleza ni lazima hizo alama zitumike tu kwa sababu ni sheria hali uendeshaji wa magari wenyewe haufuati sheria hizo tena..
Msongmano huu wa kiuchumi ni sababu kubwa ya Ufisadi, hata kama madai yako yanasema Nyerere alishindwa kulisimamia Azimio la Arusha hiyo sii hoja tena..Binafsi naamini kabisa aliweza isipokuwa tatizo ni wananchi wenyewe kufuata sheria hizo..hata huku Ulaya kwenye sheria za barabani watu wanakiuka kila siku haina maana sheria zinawashiinda viongozi..
Makosa ya Nyerere yapo pale alipoongeza sheria zisizofungamana na Azimio hilo kama vile kupiga marufuku, magari madogo ya usafiri kuwa ni anasa, TV, na mengineyo mengi, hivyo badala ya kujenga Taifa lenye kufahamu kinachoendelea nchi za nje ikwa anajenga Taifa la wafungwa. Kifupi nyerere aliongoza nchi kama gereza la Ukonga hivyo sheria za nidhamu zinakuwa zinazidi mpaka wa uungwana kwani ktk fikra zake Nyerere hakumuamini mtu.. sisi sote tulikuwa kama wafungwa vile kesho tunaweza toroka..
Kifupi Azikmio la Arusha lina vipengele vingi vya kufanyiwa marekebisho hasa pale panapohusu chama kimoja lakini mfumo huo unaweza kuwa dira ya taifa zima.. mahala ambapo kunasema CCM ibadilike kuwa kiongozi yeyote wa Taifa, maswala ya Uchumi na biashara yatazamwe upya kuwapa Wawekezaji nafasi ndani ya uzalishaji na umiliki wa mali hizo..Kuna vifungu vingi muhimu sana ambavyo havitaki changes zozote na vinafit ktk serikali yoyote ile kwani mambo mengi yaliyozungumzwa ktk Azimio hilo yanakubalika hata katika Constitution ya Marekani, Uingereza, Canada na hata China.
Hili swala la kusema Azimio la Aeusha liliandikwa na mwalimu Nyerere, mkuu wangu siii hoja kabisa kwani hakuna Azimio lolote la utawala ambalo halikuandikjwa na mtu mmoja. hata hizo Consitituion.. Kwa mfano hiyo yenu ya Marekani ilitungwa na James Madison ambaye alikuwa rais wa nne wa Marekani..na hata yeye hiyo constitution ilimshinda kutimiza yote ikawa inafanyiwa marekebisho kulingana na wakati..
Mkuu wangu lisome vizuri Azimio la Arusha kisha changanua pumba toka mchele kulingana na walaji (lWATU na MAZINGIRA) upate vibaba tosha vya kuwalisha hawa Wadanganyika waliokaa na njaa kubwa..
Biafsi naaamini kabisa inawezekana, Azimio liwe ndio DIRA ya Taifa tumnalotaka kujenga..Mkuu wangu hatuwezi kabisa kusimamisha nguzo za nyumba pasipo kuwa nauelewa wa jengo gani linakusudiwa kujengwa. Ndio mahesabu ya Wadanganyika (Miafrika)..kufikiria kujenga wakati huna plan ya mjengo zaidi ya kutazama kwanza mfuko wako. Ndivyo tunavyoijenga Tanzania ya leo, kiholela habisa.
Siku zote unapojenga nyumba fuata ramani na agiza mali kulingana na ujenzi laa sivyo kila siku utaibiwa simenti, mabati, mchanga, mbao na kadhalika kwa sababu mwenye mali hufahamu anataka kujenga nyumba ya aina gani na ni vitu gani vinahitajika. Ile kufikiria tu unajenga nyumba na kuanza kufyatua matofali haitoshi kabisa mkuu wangu ktk Ujenzi wa Taifa ndani ya mfumo huu..mababu zetu walifanya hivyo kulingana na wakati ule wakimiki ardhi kubwa na vifaa vilikuwa vya asili pia... sii leo walijaribu kufyatua matofali tu pasipo plan, wengi hadi leo baada ya miaka 20 hadi 40 bado hawajajenga kitu, matokeo yake wameuza hata hivyo viwanja..Na ndiko Tanzania tunakoelekea.
Mkuu Priorities hujenga na Malengo ambayo ndio AZIMIO tunalozungumzia.
Hivi kweli mkuu wangu unaweza nambia sababu haswa ya nchi yetu kukosa UMEME na MAJI kisha kila siku tunaenda nchi za nje kuwavuta wawekezaji!.. Does it make sense!
Mkuu wangu maelezo yako yote yanashambulia Azimio la Arusha pasipo kufikiria kwamba SHERIA inatakiwa kusimama vile vile.. Huwezi weka sheria mahala pasipo kuwa na AZIMIO na huwezi kutekeleza Azimio kama hakuna SHERIA..
Hivyo sote kutubaliane kwamba Nyerere aliweka Azimio lakini alishindwa kusimamisha Sheria.Hilo tumejifunza toka kwake, Leo hii tunaitaka Sheria mahala pasipokuwa na Azimio ambalo ni Malengo yetu Kitaifa. Pia HAIWEZEKANI tume/tutashindwa vile vile.
Wasomi kama nyie ni watu ambao mnatakiwa kutazama kwa undani makosa yaliyowahi tokea na kuweka kitu safi ambacho kinaweza fanya kazi.. Kwanza ni lazima tuwe na Azimio ambalo kwa kufupisha kazi wachangiaji wengi wamekubaliana na mengi mazuri ktk Miiko na maadili ya Viongozi.. Hakuna mtu aliyepongeza Azimio la Arusha sehemu ya kusimamia Uchumi wetu...
 
Pure Crap? Pengine ni kwa akina Zakumi! Umelisoma lakini hukuelewa yaani umesoma kama kasuku.
Hakuna nchi ulimwenguni ambayo inaendeshwa kwa misheni town, hizo nchi za dunia ya kwanza zina maazimio yao tatizo lako upeo mdogo wa kuelewa mambo yanavyokwenda kwenye karne hii ya 21st bado uko kwenye 16th
 
Tafsiri zilizopitwa na wakati nani alikwambia matajiri walikuwa ni wanyonyaji? Beggars' belief, matajiri wanachotakiwa ni kulipa kodi yao jinsi wanavyochuma, angalia kina RA, EL, JK, et al hawawezi kukuonyesha kodi wanazolipa na hivyo kulitia hasara taifa kwenye hazina yake. Uko radhi muuza madafu alipe kodi then JK na kundi lake la mafisadi wasilipe kodi ingawa wanachuma zaidi kuliko muuza madafu - pumbaf kabisa.
 
Angalia vizuri historia usipotoshe ukweli Mwamwindi alikuwa ni mkulima na wapo wengi sana kama yeye mkoani Iringa, au hufahamu maana ya the big 4? Klerlu alikuwa anakula mkewe ndio sababu akala shaba acha hizi alinacha za Pwagu na Pwaguzi,
Hivi unafahamu Mwalimu alikuwa anachukua mshahara kiasi gani? Naona kati ya watu sifuri wewe ni mojawapo au ni kuwadi wa Mafisadi.
- Bob, ninakusikia sana mkuu, isipokuwa ni kwamba naona mimi na wewe hapa tuna tofautiana na one ishu, mimi ni muumini mkubwa sana na a strong beliver wa respect kwa rule of law na ubepari, siamini kitu chochote kingine zaidi ya utawala unaoheshimu sheria, siamini US au UK, wamefikia hapo walipo kimaendeleo kwa kutumia maazimio, labda maazimio ya kisheria, lakini sio ya kichama through siasa.
- Sipendi haya maneno ya kurudisha maazimio ya CCM, kwa sababu in the first place ndiyo yametufikisha hapa tulipo as a nation yaani tumekwama, waziri ni mwizi ameiba na inafahamika kuanzia na wananchi hata authorities, lakini anaitwa kwenye chama na kuambiwa amevunja ibara ya 10 ya Azimio la Arusha, kwa hiyo anahamishiwa kuwa RC Lindi, garademiti haya ndiyo yametufikisha tulipo mkuu, huyu waziri alitakiwa afikishwe kwenye mkono wa sheria na kula mvua za kumpeleka Segerea.
- Bob, ninasema tupiganie utwala unaoheshimu sheria za jamhuri, sio kurekebisha maazimio ya Arusha, ni waste of our time na hatuwezi kabisa kuendelea na hiyo mentality ya maazimio maazimio, kwanza hayo yalikuwa intended kwa chama cha CCM, sio taifa sasa taifa tuna vyama vingi vya siasa, how do we promote maazimio ya chama kimoja over ya vyama vingine, maana hapo sasa itabidi ukubali maazimio ya vyama vingine pia vya siasa,
- Tanzania, tunahitaji heshima kwa utawala wa sheria, sio heshima kwa Azimio la Arusha, ule wakati ulishapita sasa huwezi kataza viongozi wasiwe na mishahara miwili tena, au wasiwe na nyumba mbili are you kidding me or what? Ukifuatilia kwa makini sana hilo Azimio, viongozi kama Mbowe, Ndesamburo hawatakiwi kuwa kwenye uongozi wa taifa kutokana na utajiri mkubwa wa binafsi walionao tayari hata kabla ya kuwa viongozi wa siasa, hatuwezi kuendesha nchi namna hiyo, Azimio lilikuwa na lengo moja tu nalo ni kuhakikisha kwamba umasikini ni kigezo muhimu cha kuwa kiongozi wa taifa, that by-itself is insanity kwa sababu huwezi weka hizo taratibu za umasikini na uongozi leo mwaka 2009!
- Bob, I am a strong believer of Ubepari na katika ubepari serikali inakaa nyuma na kuruhusu individualism ku-shine to the full end, huku ikihakikisha kwamba the field is levelled kwa kila individual kula kwa skills zake, serikali ni ku-regulate sheria na kukusanya kodi, sio ku-impose maazimio nje ya sheria za jamhuri.
Respect.
FMEs!
Zakumi hiyo Katiba unayodai kuwa ndio inatuunganisha nalo ni zao la Azimio la Arusha alilolifia Seti Benjamini Mpinga. Azimio lilitamkwa 1967 na Katiba ikatungwa 1977. Katiba inalikubali Azimio la Arusha kama toleo hili la mwaka 1977 linavyosema:
LENGO NA MADHUMUNI YA KATIBA HII NI UHURU, HAKI, UDUGU NA AMANI, MAMBO AMBAYO MISINGI YAKE NI HII IFUATAYO-
...
B. KWAMBA Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru
...
5 February 1967
The Arusha Declaration
Written: for Tanganyika African National Union by Julius Nyerere, 1967;
The Declaration was discussed and then published in Swahili. This revised English Translation clarifies ambiguities which existed in the translation originally issued.
The Arusha Declaration and TANUs Policy on Socialism and Self-Reliance
PART ONE
The TANU Creed
The policy of TANU is to build a socialist state. The principles of socialism are laid down in the TANU Constitution and they are as follows:
WHEREAS TANU believes:
Nyerere Archive
Hivi nikikuuliza Ujamaa ni nini? na kujitegemea ni nini? Je unaweza kupata tafsiri ya kuonyesha kujenga jamii ya watu walio sawa na huru?
Au wakati mwingine tunakubali maneno ya watu bila kufikiri?
Nyerere alishawahi kusema lolote baada ya kifo cha hili Azimio??