Azikwa akiwa hai Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azikwa akiwa hai Mbeya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by samirnasri, Apr 29, 2012.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"][TABLE]
  [TR]
  [TD]  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] UKISTAAJABU ya Mussa utayaona ya Firauni, ndivyo unavyoweza kusema baada ya wakazi wa Kitongoji cha Itezi Magharibi, Kata ya Itezi, jijini Mbeya, kuamua kumzika mwenzao akiwa hai.
  Wananchi hao wanaodaiwa kuwa na hasira kali walifikia hatua hiyo ya kutisha, kuhuzunisha na kusikitisha kwa mkazi mwenzao, Nyerere Kombwee, wakimtuhumu kuwa ni mchawi, wakimhusisha na kifo cha mtoto wa mdogo wake aliyejulikana kwa jina la Leonard Kombwee.
  Tukio hilo lilitokea jana katika kitongoji hicho, ambapo wananchi hao walimkamata Kombwee na kumpeleka mahali walipolichimba kaburi la kumzikia mtoto wa mdogo wake, ambalo lilikuwa na urefu wa futi tatu huku wakimlazimisha aingie ndani.
  Kombwee alipoingia ndani ya kaburi hilo wananchi hao walitumia fursa hiyo kumtupia jiwe kichwani na kumfukia akiwa hai.
  Awali kabla ya wananchi hao kufikia hatua hiyo, wakiwa katika shughuli za kuchimba kaburi hilo kwa ajili ya kumzika mtoto wa mdogo wake, walianza kujadili sababu ya Nyerere kutokuwapo kwenye msiba huo.
  Baada ya majadiliano ya muda mrefu walifikia makubaliano ya kuteua baadhi ya watu kwenda kumfuata ambapo walipofika nyumbani kwake hawakumkuta lakini waliamua kuwapiga mama na dada wa Nyerere ili wataje alipo wanayemhitaji.
  Mama na dada wa Nyerere walipoona kipigo kimewazidi walilalizimika kutaja alipo Nyerere, ambapo alikamatwa na wananchi hao kisha kumpiga huku wakienda naye lilipokuwa likichimbwa kaburi la mtoto wa mdogo wake.
  Maziko ya kumzika aliye hai
  Wananchi hao walipomfikisha mtuhumiwa wao kwa wenzao majira ya saa tatu asubuhi, walimlazimisha Nyerere kuingia kaburini na alipoingia walimsindikiza kwa kipigo cha jiwe na baadaye walimfukia.
  Mmoja wa watu waliokuwa makaburini hapo inadaiwa kuwa alimkandamiza kwa chepeo, hali iliyosababisha kushindwa kujinasua na kufukiwa kirahisi akiwa mzima.
  "Baada ya kuona mchanga unazidi kujaa huku akiwa amekandamizwa na chepeo marehemu aligeuka na kulala kifudifudi hadi mchanga ukajaa kaburi," alieleza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
  Baada ya tukio hilo baadhi ya watu waliokuwapo makaburini waliamua kutawanyika kwenye eneo hilo huku wengine wakitoa taarifa za tukio hilo polisi.
  Polisi walipofika eneo hilo majira ya saa nane mchana wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili DFP 474, walilazimika kufyatua risasi za moto na mabomu ya machozi ili kuwatawanya waliokuwapo na baadaye kufukua kaburi hilo ambapo walimkuta Nyerere amekwisha kufariki dunia.
  Kisa chaelezwa
  Baadhi ya majirani wa familia hiyo walidai kuwa tukio hilo limesababishwa na ugomvi wa kifamilia ambao umedumu kwa muda mrefu, ambapo inadaiwa marehemu Nyerere alikuwa akituhumiwa kumuua mtoto huyo wa mdogo wake na ndipo wananchi wakaamua kulipa kisasi.
  Walidai kuwa baada ya mtoto wa Leonard kufariki dunia Aprili 27 mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha majira ya saa tatu asubuhi, walimshuku Nyerere kwakuwa hakwenda kwenye msiba.
  Walidai kuwa hata hivyo Nyerere alizikwa hai kwa sababu alitoa vitisho kwa wananchi waliompeleka makaburini kuwa kipigo walimchompatia na kusababisha atoke damu hakitakwenda bure ni lazima atakilipa.
  Naye Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Frank Maemba, aliyekuwepo makaburini kusimamia hali ya amani wakati wa ufukuaji wa mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu alisema tukio hilo ni la kikatili na lisilopaswa kuvumiliwa.
  Maemba alisema wananchi wote walioanzisha uamuzi wa kuwashawishi wenzao kujichukulia sheria mkononi watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.


  source: Tanzania Daima- Jumapili


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Y

  Yasser5 JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  R.I.P marehemu
   
 3. m

  mussamhando Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah! hakuna utu kabisa
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nawashangaa sana hawa viongozi wanaochezea wananchi,kuna watanzania wakatili sana na wakiamua kuharibu basi hakutakalika hapa!
  RIP nyerere
   
 5. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  utu hatuna, cjui hiki ni kizazi kipi
   
 6. U

  Usokitabu Senior Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Waliofanya hivyo nao watafanywa hivohivyo siku moja..
   
 7. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Huwaga imani za kishirikina zinarudisha nyuma sn maendeleo mbeya,. Waache vijana wajichukulie sheria labda ndo watapungua ili tuijenge mbeya yetu,. Mungu ibariki mbeya
   
 8. Mtagwa lindi

  Mtagwa lindi JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 278
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hata wachawi hawana huruma kama kweli alikuwa mchawi anastaili kilichomtokea
   
 9. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnasema TZ kuna amani?TZ hakuna amani watu wametulia tuu.
   
 10. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbeya haiishi vituko kila kukicha, ee Mungu inusuru mbeya na mambo kama haya
   
 11. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Lala kwa Amani ya Bwana!
   
 12. Kifimbo Cheza

  Kifimbo Cheza JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Tushirikiane wauaji hao wapatikane, ni kwa wa-TZ kuendekeza ushirikina jamani!
   
 13. Kifimbo Cheza

  Kifimbo Cheza JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Tushirikiane wauaji hao wapatikane, ni AIBU kwa wa-TZ kuendekeza ushirikina jamani!
   
 14. M

  Mboerap Senior Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Walifanya pupa kumzika, wangembana amfufue mtoto kwanza
   
 15. T

  Toshack Kibala Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo siyo nzuri ila ni salamu kwa vyombo vya dola kuwa wanapofumbia macho mambo madogomadogo matokeo yake ndiyo haya
   
 16. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mbaya sana watanzania kujenga tabia ya kuchukua sheria mkononi
   
 17. n

  ngarambe Senior Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imenishtua,,,,,poleni ndugu jamaa na marafiki mbeya.
   
 18. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha enzi hizi za www bado watu wanashabikia ushirikina kiasi cha kuuana!
   
 19. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,455
  Trophy Points: 280
  tukio limetokea asubuhi polisi wanafika saa 8 hii inaonesha jinsi gani ambavyo vyombo vya usalama havitekelezi wajibu wake.
  Haya mambo haya ni hatari sana kwa mustakabari wa taifa letu.
  U will get what you deserve poor mr the late nyerere
   
 20. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  inatisha,hivi mtu unahakikishaje kuwa fulani ni mchawi kiasi cha kuamua kumuua?mi nahisi wengi wanauliwa bila hatia.
   
Loading...