Nadhani muda muafaka wa serikali kuunda sheria ya uchawi maana kuendelea kukataa kuwa serikali haitambui uchawi ni uongo na wengi watakufa na wengine huenda ni muhimu katika jamii yao na wanaleta manufaa katika jamii zao
Nashauri wasajiliwe kuliko kukana kuwa haupo hali wanasiasa wanaenda kupata huduma za kiutawala na maamuzi katika mikutano iliyo ya siri mbon mambo ya Freemanson yapo wazi na anayetaka kujiunga anaruhusiwa?
Nashauri pia waelimishwe kuutumia kwa manufaa bora wazungu tunatumia sayansi yao kwanini ya kwetu isitambuliwe
Nafikiri watu washauriwe na wajitokeze kila mmoja na nguvu zake na aambiwe yeye anaweza kufanyia nini nchi hii ikapata
faida na uchawi wake badala ya kinachoendelea cha kuwaua kikatili
Na watu wa haki za binadamu wako wapi? maana mtu anaonesha ujuzi wake hawamtetei na kumtangaza!
Pawepo utaratibu na si ajabu kwani hamsoni habari za Firauni?Farao na Mtume Musa? Mbona hapakuwepo na madhara baada ya wao kuwa wanajumuishwa katika utawala
Wengine wanauwezo wa kuzuia mvua/kuleta mvua na kuleta ndege (Queleaquelea), kuleta maradhi, kuua na kufufua kwa mazingaumbwe/ kuondoa mguu na kuuficha,kuuondoa uume na kuuficha, kuzuia uzazi mwanamke asizae, kuharibu nyumba kwa upepo, kuchukua mazao ya wenzake nk
Huenda tungepunguza matumizi ya dawa za uzazi za mpango, gharama za mvua kama za Lowasa, kupunguza gharama za kuua ndege, maradhi, gharama za opereshaji ya uzazi na