Azania Sec. School (SPECIAL THREAD)

Azania Sec. School (SPECIAL THREAD)

Dah,
Kitambo sana.
Walimu kama Tokyo (History), Mugituti, Andrew Kwayu (Head Master), Mchwampaka (Discipline), Christian, Kuna wa Physics nadhan ndio alikua msaidiz wa Kwayu, Fuvu kwenye mathematics, etc.

Bifu Azania vs Jitegemee, Pigana sana bisibisi na viwembe pale feri kulikua na kituo Cha daladala mbele ya NBC Bank au ile bustani. Bifu lilikua eti kugombea hicho kituo Cha daladala.

Bifu Azania vs Al-haramain tukikutana kwenye mechi za UMISETA Ilala. Na Kuna bifu maaarufu la Azania vs Tambaza ambalo sikulikuta. Bifu hili lilipelekea kufutwa kwa O-Level Tambaza. Wanasema kuna mwamba wa Tambaza alitoka bonden Kwa madiba na formula ya kutengeneza mabomu ya petrol, hiyo ndio iliyoipa ushindi Tambaza against Azania.

🎶 Azania Azania Azania our school,
We look at you with pride,
you are known far and wide, you are always our guide,
we will never forget you 🎶
Da kumbe tupo wengi, nilipitia hapo 1994-1997 na kuelea Songea Boys kabla ya kurudi Tambaza hadi 2000. Mchwampaka angekuwa hai leo, zile fimbo zake za kuwaadabisha wachelewaji zingempeleka the Hague ya Milard Ayo TV.
 
Da kumbe tupo wengi, nilipitia hapo 1994-1997 na kuelea Songea Boys kabla ya kurudi Tambaza hadi 2000. Mchwampaka angekuwa hai leo, zile fimbo zake za kuwaadabisha wachelewaji zingempeleka the Hague ya Milard Ayo TV.
Yaani kusoma tu Azania mwanafunzi unajiona umemaliza kila kitu. Mabifu na makondakta ilikua kawaida tu.

Pale kituo Cha "fire" Kondakta akileta sijui mwisho wanafunzi watano anavutwa tu chini watu wanaingia, na wanaenda kukaa.

🎶In the heaven of peace, Azania stands at ease, forever, together, we always say,

You are known far and wide, you are always our guide, we will never forget you 🎶
 
Back
Top Bottom