Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,352
- 9,810
Azam TV japo wanatoa huduma nzuri za TV, lakini linapokuja suala la customer service kwa mtazamo wangu na uzoefu wa kuhudumiwa, ndo kampuni inayoongoza kuwa na huduma mbovu kuliko wote!
Kwanza hawaanzi kupokea simu wala kutatua matatizo ya wateja wao mpaka ifike saa 2 asubuhi katika siku za week days. Kali zaidi ni siku za weekend, pale unapotegemea kuwa weekend ndo siku ambazo watu wengi hawaendi makazini na mashuleni, hivyo kunakuwa na watazamaji wengi zaidi majumbani, wao wanawaza tofauti.
Wale wafanyakazi wa customer service nao wanalala nyumbani, hivyo hata kama kifurushi chako kimekoroga au unataka usaidiwe Jambo lolote hutopata msaada maana staff wote wapo nyumbani wanakula weekend!
Huwa najiuliza, ina maana hawaoni hata makampuni kama ya simu yanafanyaje? Na hata hizi siku za kawaida ikifika saa 4 usiku wote wanatimka kwenda kulala. Kweli mnafanya biashara kitajiri sana, mteja hata kama umelipia hela yako kifurushi halaf kifurushi kimekoroga weekend,utajua mwenyewe!
Hizi ni madharau.