Azam TV ndo kampuni inayoongoza kwa huduma mbaya kwa mteja

Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
5,526
2,000
Azam TV japo wanatoa huduma nzuri za TV, lakini linapokuja suala la customer service kwa mtazamo wangu na uzoefu wa kuhudumiwa, ndo kampuni inayoongoza kuwa na huduma mbovu kuliko wote!

Kwanza hawaanzi kupokea simu wala kutatua matatizo ya wateja wao mpaka ifike saa 2 asubuhi katika siku za week days. Kali zaidi ni siku za weekend, pale unapotegemea kuwa weekend ndo siku ambazo watu wengi hawaendi makazini na mashuleni, hivyo kunakuwa na watazamaji wengi zaidi majumbani, wao wanawaza tofauti.

Wale wafanyakazi wa customer service nao wanalala nyumbani, hivyo hata kama kifurushi chako kimekoroga au unataka usaidiwe Jambo lolote hutopata msaada maana staff wote wapo nyumbani wanakula weekend!

Huwa najiuliza, ina maana hawaoni hata makampuni kama ya simu yanafanyaje? Na hata hizi siku za kawaida ikifika saa 4 usiku wote wanatimka kwenda kulala. Kweli mnafanya biashara kitajiri sana, mteja hata kama umelipia hela yako kifurushi halaf kifurushi kimekoroga weekend,utajua mwenyewe!

Hizi ni madharau.
 
Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,380
2,000
Hawa nliacha tumia kifurushi chao baada ya kuwapigia simu almost two days hawapokei. Siku wamepokea mpokeaji anajivuta kuongea namweleza tatizo kuwa nimeweka kifurushi toka juzi hakisomi ananambia sasa yeye afanyeje?

Kama nilikosea masharti imekula kwangu.nikamuuliza masharti gani zaidi ya kujiunga tv ikiwa on?akanambia nimpigie mtu mwingine yeye nisimsumbue anaenda kuswali maana nina maswali kama polisi.akakata na simu. Imagije nmepiga two days hawapokei anakuja pokea mtu namna hiyo?
 
sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
379
1,000
Kwanini unachanganya Azam TV na king'amuzi za Azam? Ni zawa na kusema timu ya azam inajisikia sana mana hawapokei simu kuhusu mambo ya king'amuzi, kingine wakuu acheni kua biased,
 
Cyb

JF-Expert Member
Jun 6, 2014
362
1,000
Subiri mashekhe waje mbio mbio kutetea maslahi yao.
Huyu hapa kashafika.
Kwanini unachanganya Azam TV na king'amuzi za Azam? Ni zawa na kusema timu ya azam inajisikia sana mana hawapokei simu kuhusu mambo ya king'amuzi, kingine wakuu acheni kua biased,
Angalia comment hii hapa chini. Ameeleza kama mtu wa pili kwenye huu uzi, hivyo kusema kwamba wapo watu zaidi ya 100 waliopata adha hii haitakuwa kuongeza chumvi.

Halafu, hauna hoja. Hata madish yao yamechorwa swoosh yenye maneno Azam Tv kwa ndani, hata ving'amuzi vina logo hiyo.

Azam wajitafakari.
Hawa nliacha tumia kifurushi chao baada ya kuwapigia simu almost two days hawapokei. Siku wamepokea mpokeaji anajivuta kuongea namweleza tatizo kuwa nimeweka kifurushi toka juzi hakisomi ananambia sasa yeye afanyeje? Kama nilikosea masharti imekula kwangu.nikamuuliza masharti gani zaidi ya kujiunga tv ikiwa on?akanambia nimpigie mtu mwingine yeye nisimsumbue anaenda kuswali maana nina maswali kama polisi.akakata na simu. Imagije nmepiga two days hawapokei anakuja pokea mtu namna hiyo?
 
Podcast

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
376
500
Kwanza ukipiga simu ukaelezea shida yako ni kama wanakufokea yani, mbona kwingine hakuna haya, alafu kwani hakuna chumba maalumu kwa kazi hii mpaka ukipiga simu unasikia ni kelele tu kama wapo sokoni.
 
fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
3,298
2,000
Azam TV japo wanatoa huduma nzuri za Tv, lakin linapokuja suala la customer service ndo kampuni inayoongoza kuwa na huduma mbaya kuliko wote!
Kwanza hawaanzi kupokea simu wala kutatua matatizo ya wateja wao mpaka ifike saa 2 asubuhi katika siku za week days. Kali zaidi ni siku za weekend...
Nimeuchukua huu ujumbe na kumpa kuongozi wao mmoja mkubwa.
 
The Underboss

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,580
2,000
Nakumbuka miaka 3 iliyopita nilikua kwa ndugu yangu, sasa nikawa namsaidia kufanya configuration ya hicho king'amuzi. Baada ya muda nikapiga simu customer care ilikua jumamosi, kwanza namba hakikupokelewa, nikasubiri Jumatatu nikawapigia wahakunipa msaada niliokua nahitaji. Wakashauri niende ofisini kwao, nikajiuliza itakuaje kama mtu uko mkoani.

Baada ya hapo nikasema king'amuzi cha azam hakitakuja kukanyaga nyumbani kwaku hata kwa bunduki.

Na vile mimi sio shabiki wa mpira wowote ule, azam kitafuata nini nyumbani kwangu?

Naamini hata wenye azam ni vile wanafuatilia hii local football ya tff, otherwise sidhani kama kuna mtu angenunua azam king'amuzi.
 
Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
248
500
Azam TV japo wanatoa huduma nzuri za Tv, lakin linapokuja suala la customer service ndo kampuni inayoongoza kuwa na huduma mbaya kuliko wote!
Kwanza hawaanzi kupokea simu wala kutatua matatizo ya wateja wao mpaka ifike saa 2 asubuhi katika siku za week days..
Maneno yako yawezakuwa kweli.

Lakini, kauli uliyotumia ni nzito sana.

Ni kauli ambayo ukikalishwa chini uitetee, sijui kama utaweza.

(Thibitisha bila shaka kuwa ni ya mwisho).

Mfano: ni kwa utafiti gani na ulilinganisha makampuni mangapi mpaka Azam wakawa ni watoa huduma mbaya zaidi kwa kipengele tajwa.

Wakati mwingine tujaribu kutoa hoja zetu bila kutumia maneno yasiyothibitishwa kitaalamu/yasiyo na uthibitisho.

Pia niwasihi watanzania, mara nyingi tunalalamika kwa makampuni mengi kutokutuajiri. Lakini, tunapopewa kazi matokeo yake huwa si mema sana. Ukifuatlia hapo wengi katika kitengo ni wenzangu na mimi, wameizoea kazi na matokeo yake ni hivyo tena.

Tufanye kazi kulingana na taratibu za kazi husika (SOPs).

Samahani kama nimekukwaza au kuna aliyekwazika.
 
Gamba la Mbu

Senior Member
Jun 28, 2020
110
250
Hawa nliacha tumia kifurushi chao baada ya kuwapigia simu almost two days hawapokei. Siku wamepokea mpokeaji anajivuta kuongea namweleza tatizo kuwa nimeweka kifurushi toka juzi hakisomi ananambia sasa yeye afanyeje? Kama nilikosea masharti imekula kwangu.nikamuuliza masharti gani zaidi ya kujiunga tv ikiwa on?akanambia nimpigie mtu mwingine yeye nisimsumbue anaenda kuswali maana nina maswali kama polisi.akakata na simu. Imagije nmepiga two days hawapokei anakuja pokea mtu namna hiyo?
Ahahahaaa. Ungemnasa vibao vya hewani hata viwili tu.
 
Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
5,526
2,000
Maneno yako yawezakuwa kweli.
Lakini, kauli uliyotumia ni nzito sana.
Ni kauli ambayo ukikalishwa chini uitetee, sijui kama utaweza.

Mfano: ni kwa utafiti gani na ulilinganisha makampuni mangapi mpaka Azam wakawa ni watoa huduma mbaya zaidi kwa kipengele tajwa.

Wakati mwingine tujaribu kutoa hoja zetu bila kutumia maneno yasiyothibitishwa kitaalamu/yasiyo na uthibitisho. Samahani kama nimekukwaza.
Hiyo ni kwa wajibu wa mtazamo wangu binafsi na uzoefu
 
Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
5,526
2,000
Hawa nliacha tumia kifurushi chao baada ya kuwapigia simu almost two days hawapokei. Siku wamepokea mpokeaji anajivuta kuongea namweleza tatizo kuwa nimeweka kifurushi toka juzi hakisomi ananambia sasa yeye afanyeje?...
Yan ndugu yangu hiyo ni kawaida yao, maana Kuna siku nilimpigia muhudumu simu,nikamweleza tatizo ambalo nadhani alikuwa hana uwezo wa kulitatua,sasa badala hata anisubirishe ili aweze kulitafutia ufumbuzi na wenzake ambao wana ujuzi na hilo jambo, ye alikata simu kabisa! Nikabaki nashangaa...
 
Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
5,526
2,000
Kwanini unachanganya Azam TV na king'amuzi za Azam? Ni zawa na kusema timu ya azam inajisikia sana mana hawapokei simu kuhusu mambo ya king'amuzi, kingine wakuu acheni kua biased,
Sijui hata unajua unaongelea Nini!? King'amuzi Cha azam kinamilikiwa na kampuni gani ya TV?!! Au wewe unamaanisha Uhai TV inayomilikiwa na Azam TV?..Mkuu angalia siku ingine usiingie choo cha kike..
 
Ceftriaxon

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
230
500
DSTV haina usumbufu,haina kukata hata wakati wa mawingu au mvua,...customer service wako vizuri...hamia huku mkuu,mwaka wa 7 natumia dstv sijawahi pata usumbufu.
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
3,054
2,000
Walee jamaa kali yao ni pale kisimbusi chako kitakapo haribika thennuwapelekee pale ofisi kwao hapo ndipo utakapo amini ya kuwa umetupa pesa yako .... Mm nikipeleka king'amuzi kitengenezwe toka mwaka jana mpaka leo hawajawahi kunipigia simu kuniambia labda king'amuzi chako kimetengemaa ...na ukienda pale wana kwambia ofisi imefungwa sababu ya corona
 
Snipes

JF-Expert Member
Jul 2, 2013
8,652
2,000
Sijui hata unajua unaongelea Nini!? King'amuzi Cha azam kinamilikiwa na kampuni gani ya TV?!! Au wewe unamaanisha Uhai TV inayomilikiwa na Azam TV?..Mkuu angalia siku ingine usiingie choo cha kike..
kuna mtu alisema watetezi wake watakuja.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom