Azam Tv mihemko itawapeleka shimoni

Azam Tv mihemko itawapeleka shimoni

Fa fa fa zipo nyingi Asee. Ulitaka watuonyeshe Yale magari yenye pret namba za kule zenji??
 
Tusipangiane bana,,

madini yote yaliyoko nchi hii hayafikii thamani ya mtu mmoja,waache waibe,we are less concern
 
Huyu mchawi sijui bashite anakufanya nn hadi unakosa kutambua maigizo na uharisia
 
Jana nilicheka sana Sizonje alivyokuwa anafanya maigizo yake pale Bandarini kakunja uso yupo serious kabisa kucheki pembeni anawaona Uhuru na Habari Leo akaishiwa nguvu kabisa.
 
Tatizo habari ya kuibiwa Mali zetu hazina ukweli yaani ni kama fiction tu imetengenezwa kwahiyo waliona ni bora kutangaza habari yenye uhalisia. By the way hukusoma gazeti la Uhuru waliripoti kama kipaumbele habari ya Mkuu kuvamia bandarini na kukamata magari na dhahabu.
Habari za uvamizi
 
kajifunze kwanza kuandika kiswahili
Honyo = Onyo
 
Azam walichemka kama uji wa maharagwe kwa ujumla sasa hivi hakuna chombo cha habari smart kama Azam ila wapunguze ushabiki waweke masilahi ya Taifa mbele bado mimi ni shabiki na mpenzi wenu ila jana mlichemka ilikuwa kama ni Tv ya familia ya Nape mmevuna aibu ninyi ni professionals kuanzia mkurugenzi wenu hata wasomaji wapo vizuri anagalieni msijitumbukize kwenye matope tunawategemeenni
 
Jana nilishtushwa kuona mnashindwa kujua uzito wa habari, kubalansi, kutawaliwa na mihemko zaidi ya kujua umuhimu wa vipaumbele kwa watu na nchi yetu.

Hakuna namna unaweza kunishawishi nikaelewa kwamba ni bora zaidi kuongelea "personality" tena kwa dakika5 kuliko kuongelea namna nchi yetu inavyoliwa na kuibiwa tukio lililokuwa likimhusisha raisi. Kwamba kukamatwa makontena 20 yenye kuhisiwa yanatoroshwa yakibeba dhahabu si habari nzito kwenu. Kwamba Nape ni habari nzuto na muhimu kwenu kuliko mali na utajiri wa nchi yetu.

Lakini pia, hivi unaanza habari gani kwa siku, ya raisi ama ya aliyefukuzwa uwaziri? Tena mlivyo wa hajabu wakati mkitoa dakika 5 na kukaribisha wazungumzaji kwa tukio la mtu, upande wa pili mnatoa dakika1 halafu mnafukia as if anayeongea ni balozi wa nyumba kumi na kilichokatokea ni kama mtu kutema mate.

Yawezekana hao wanaotuibia mali zetu waliwaambia msiwaoneshe sana ili wananchi wasipige kelele dhidi yao na badala yake muonesheni fulani ili wananchi wapige kelele dhidi ya utawala. Kama na nyie mlikubali hili na mkauvaa mkenge basi anzeni kujichunguza kabla, nchi yetu inaliwa na sote tunajua ila nyie hamuoni kama la kuliwa nchi yetu ni hoja. Mnatakiwa kuelewa hao wezi hawamuibii JPM tu, hawamwibii fulani tu, wanatuibia sisi sote na tunapopoteza wakati wenzenu wanapata ni kuihujumu nchi yetu. Ni kuhujumu serikali kwa kile inachojaribu kukifanya katika maendeleo, msivimbe vichwa mkajiona tayari.
Mkuu fungua macho kumekucha hayo mambo unayoyataka AZAM MEDIA wafanye ndio yamesababisha mzozo huko CLOUDS MEDIA au umetumwa na Albert? AZAM ni chombo huru hawapangiwi habari ya kurusha hewani hatakama huyo prezidaa atumie kichwa kumove badala ya miguu AZAM wanayo maamuzi warushe ama washiti
USHAURI :- kama unamiss sana habari za prezidaa wako tazama na sikiliza TBC.
Wanatuzingua tu, mpaka Magu aende ndio utasikia ooh tumekamata Container sijui limefanyafanya madudu gani sijui Inamaana aspokuja huwa hamkamati?
 
Nyie ccm simna tv yenu tbc sasa mnamlalamikia azam wann nawakati mna tv yenu ambayo kaziyake nikusifia upuuzi kama uliokuwa unaendelea bandalini..hamuwezi kumlazimisha mtu kuonesha kipindi chenu ..kosalenu nikuibadilisha tv ya serikari kuwa tv ya ccm sasa imekoswa wakuitazama mnalazimisha azam ioneshe maigizo yenu..ss tumeshachoka maigizo hayo
 
"Heri kujikwaa kidole kuliko ulimi" waswahili walinena hivyo
 
Maisha ya mtu mmoja ni ya thamani kuliko makontena zaidi ya 200 ya dhahabu. Mh. Rais anapaswa kujua hilo. Lakini pia mnatakiwa kuelewa kwamba kiongozi ndiye dira ya jamii anayoiongoza, ukiona wafuasi wako wameanza kutokukufuatlia ni wajibu wako kujitathmini kwanza.
Inategemea unatafsiri hipi juu ya "dhahabu". Nchi yako ni ya thamani sana as nikasema wewe una thamani ya " gold". Sasa kuiacha nchi yako na thamani yake iliyonayo ichezewe ni sawa na kutokujua umuhimu wa kitu unakiita "nchi yangu" ijapo kwingine wako radhi kuzilinda nchi zao hata kwa gharama ya damu. Na ndo maana nimekwambia ilivyo dhahabu ndo heshima na thamani ya nchi yako, sasa kama huwezi kulifikilia hilo kwa mapana hutaelewa pia wajibu wako kwa nchi yako iwe leo ama kesho. Haijalishi yupo nani (hai) leo na nani kaondoka, nchi itabaki na thamani yake itabaki pale pale. Kama unabisha nenda kwenye nchi za watu halafu ukaingie kienyeji ndo utajua kwenu wapi. Walikufa wangapi, ni wapi ukasikia Tz ilikufa nayo? Mwl. Nyerere yuko wapi, Mzee Kawawa yuko wapi? A. Jumbe yuko wapi? Hata wewe kesho hutakuwepo ila watabaki wengine na tunataka hata wanaozaliwa leo nao waje waikute Tz na waiheshimu pia kwasababu ni nchi ya mababu zao.
 
Kituo chao wenyewe wamewekeza kwa hela zao wenyewe!! wewe ni nani mpaka uwapangie? Wao ndiyo wanajua habari gani iwe ya kwanza na ipi iwe ya pili, umeumia sana fungua kituo chako muonyeshe sizonje asubuhi hadi jioni!!!
Mpendwa nakurushia Halotel pesa japo ukapate Maji ya Dafu.
 
Jana nilishtushwa kuona mnashindwa kujua uzito wa habari, kubalansi, kutawaliwa na mihemko zaidi ya kujua umuhimu wa vipaumbele kwa watu na nchi yetu.

Hakuna namna unaweza kunishawishi nikaelewa kwamba ni bora zaidi kuongelea "personality" tena kwa dakika5 kuliko kuongelea namna nchi yetu inavyoliwa na kuibiwa tukio lililokuwa likimhusisha raisi. Kwamba kukamatwa makontena 20 yenye kuhisiwa yanatoroshwa yakibeba dhahabu si habari nzito kwenu. Kwamba Nape ni habari nzuto na muhimu kwenu kuliko mali na utajiri wa nchi yetu.

Lakini pia, hivi unaanza habari gani kwa siku, ya raisi ama ya aliyefukuzwa uwaziri? Tena mlivyo wa hajabu wakati mkitoa dakika 5 na kukaribisha wazungumzaji kwa tukio la mtu, upande wa pili mnatoa dakika1 halafu mnafukia as if anayeongea ni balozi wa nyumba kumi na kilichokatokea ni kama mtu kutema mate.

Yawezekana hao wanaotuibia mali zetu waliwaambia msiwaoneshe sana ili wananchi wasipige kelele dhidi yao na badala yake muonesheni fulani ili wananchi wapige kelele dhidi ya utawala. Kama na nyie mlikubali hili na mkauvaa mkenge basi anzeni kujichunguza kabla, nchi yetu inaliwa na sote tunajua ila nyie hamuoni kama la kuliwa nchi yetu ni hoja. Mnatakiwa kuelewa hao wezi hawamuibii JPM tu, hawamwibii fulani tu, wanatuibia sisi sote na tunapopoteza wakati wenzenu wanapata ni kuihujumu nchi yetu. Ni kuhujumu serikali kwa kile inachojaribu kukifanya katika maendeleo, msivimbe vichwa mkajiona tayari.
hata mchambuzi wa masuala fulani flani wawe(AZAM TV) wanachagua mtu neutral, ndio atakayesema ukweli. kuna wachambuzi hawaonagi positive about Govt though hawana chama.
 
Back
Top Bottom