Azam Tv mihemko itawapeleka shimoni

Azam Tv mihemko itawapeleka shimoni

Wacha waibe.... mbona bashite kutwa kufuja pesa kwenye sherehe..jamaa anapenda sherehe yule ndio mana alipata zero
Miya Mungu anakuona ujue sio kwa kumponda huku kumbuka mtoto wa mwenzio ni wako so mtoto wa Bashite ni sawa na mtoto wa Miya
 
Jana nilishtushwa kuona mnashindwa kujua uzito wa habari, kubalansi, kutawaliwa na mihemko zaidi ya kujua umuhimu wa vipaumbele kwa watu na nchi yetu.

Hakuna namna unaweza kunishawishi nikaelewa kwamba ni bora zaidi kuongelea "personality" tena kwa dakika5 kuliko kuongelea namna nchi yetu inavyoliwa na kuibiwa tukio lililokuwa likimhusisha raisi. Kwamba kukamatwa makontena 20 yenye kuhisiwa yanatoroshwa yakibeba dhahabu si habari nzito kwenu. Kwamba Nape ni habari nzito na muhimu kwenu kuliko mali na utajiri wa nchi yetu.

Lakini pia, hivi unaanza habari gani kwa siku, ya raisi ama ya aliyefukuzwa uwaziri? Tena mlivyo wa hajabu wakati mkitoa dakika 5 na kukaribisha wazungumzaji kwa tukio la mtu, upande wa pili mnatoa dakika1 halafu mnafukia as if anayeongea ni balozi wa nyumba kumi na kilichotokea ni kama mtu kutema mate.

Yawezekana hao wanaotuibia mali zetu waliwaambia msiwaoneshe sana ili wananchi wasipige kelele dhidi yao na badala yake muonesheni fulani ili wananchi wapige kelele dhidi ya utawala. Kama na nyie mlikubali hili na mkauvaa mkenge basi anzeni kujichunguza kabla, nchi yetu inaliwa na sote tunajua ila nyie hamuoni kama la kuliwa nchi yetu ni hoja. Mnatakiwa kuelewa hao wezi hawamuibii JPM tu, hawamwibii fulani tu, wanatuibia sisi sote na tunapopoteza wakati wenzenu wanapata ni kuihujumu nchi yetu. Ni kuhujumu serikali kwa kile inachojaribu kukifanya katika maendeleo, msivimbe vichwa mkajiona tayari.
Hacheni vyombo vya habari vitimize wajibu wao kwa kufanya kazi zao huru.
Hayo makontena ya mchanga si habari mpya labda kama wewe si msomaji wa guardian/citizen/east African. Hao wazungu wenye huo mzigo baada ile marufuku ya rais walishakuwa tayari container ambazo nyingine zilkuwa zinasubiri meli na nyingine zinakamilisha documentation na wala si kwamba agizo lilipotoka wao wakaendelea kuvuna huo mchanga.
Kuna barua yao imetembea sana kwenye mitandao ya kijamii zaidi ya wiki tatu kuhusu mawasiliano yao na wizara.
Kwa hiyo hizo container wala hazikuwa zimefichwa wala nini,zipo dry port huku wakisubiri muafaka baina yao na wizara.
Hacheni hizo political gimmicks zenu na ku twist mambo ili kutafuta sifa za kijinga.
 
Nukuu "habari ni mtu kungata mbwa sio mbwa kungata mtu " rais kuja bandarini tumeshazoea ila kutumbuliwa kwa Nape ni habari ya mwaka
 
Nchi ilishajengwa mkuu kinachohitajika ni sie watanzania kuwa wazalendo. Siwezi kuelewa kwanini tulilalamikia kukosa uzalendo na nchi yetu kuibiwa enzi za JK na sasa tumempata mtu anayeonekana kusimamia hayo bado huoni ni sehemu ya kuleta uzalendo. Pathetic!









Uzalendo ni dhana pana, huwezi kuujenga uzalendo katika nchi ambayo viongozi wake wanatanguliza ititkadi zao mbele. Unaposimama jukwaani na kurejea rejea kusema hii ni serikali ya ccm usitegemee wasio wanachama na wapenzi wa ccm wanafurahia nkauli hizo. Hawa wanajihisi kama serikali haiwahusu.

Nchi zenye uzalendo ni zile ambazo baada ya uchaguzi serikali iliyoko madarakani zinaacha kujinasibu kwa vyama vyao, zinakuwa serikali za wananchi wote. Lakini kwa Tanzania ni ndoto kuwa na uzalendo.
 
Back
Top Bottom