Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,034
- 7,590
Jana nilishtushwa kuona mnashindwa kujua uzito wa habari, kubalansi, kutawaliwa na mihemko zaidi ya kujua umuhimu wa vipaumbele kwa watu na nchi yetu.
Hakuna namna unaweza kunishawishi nikaelewa kwamba ni bora zaidi kuongelea "personality" tena kwa dakika5 kuliko kuongelea namna nchi yetu inavyoliwa na kuibiwa tukio lililokuwa likimhusisha raisi. Kwamba kukamatwa makontena 20 yenye kuhisiwa yanatoroshwa yakibeba dhahabu si habari nzito kwenu. Kwamba Nape ni habari nzito na muhimu kwenu kuliko mali na utajiri wa nchi yetu.
Lakini pia, hivi unaanza habari gani kwa siku, ya raisi ama ya aliyefukuzwa uwaziri? Tena mlivyo wa hajabu wakati mkitoa dakika 5 na kukaribisha wazungumzaji kwa tukio la mtu, upande wa pili mnatoa dakika1 halafu mnafukia as if anayeongea ni balozi wa nyumba kumi na kilichotokea ni kama mtu kutema mate.
Yawezekana hao wanaotuibia mali zetu waliwaambia msiwaoneshe sana ili wananchi wasipige kelele dhidi yao na badala yake muonesheni fulani ili wananchi wapige kelele dhidi ya utawala. Kama na nyie mlikubali hili na mkauvaa mkenge basi anzeni kujichunguza kabla, nchi yetu inaliwa na sote tunajua ila nyie hamuoni kama la kuliwa nchi yetu ni hoja. Mnatakiwa kuelewa hao wezi hawamuibii JPM tu, hawamwibii fulani tu, wanatuibia sisi sote na tunapopoteza wakati wenzenu wanapata ni kuihujumu nchi yetu. Ni kuhujumu serikali kwa kile inachojaribu kukifanya katika maendeleo, msivimbe vichwa mkajiona tayari.