Mimi pia nimestuka sana!!
Yule jamaa na mustachi yake kama Carl Peters kakazana kabisa kuwa eti hiyo ajali ni "kafara" ya mwenye shule,kama sio "kafara" basi ni majini ktk eneo hilo yalikuwa yanataka damu.
Jamaa na mustachi yake kakazana kabisa kuwa eti ndio maana maiti zote hakuna hata moja yenye damu,hii ni kwa sbb maiti za kafara na zile za majini huwa hazitoki damu hata kukiwa na ajali.
Jamaa ana imani kali kweli za ulimwengu wa pili,anasema mmiliki wa shule alimkataza mwanae kwenda katika hiyo ziara,so kwa kumkataza huko inamaanisha kuwa jamaa alijua leo ndio siku ya kafara.
Huyu jamaa aliyehojiwa hakupaswa kurushwa hewani,kwa mfano mimi toka jana...Ikifika taarifa ha habari nakusanya watoto na wajukuu waje waone taarifa za vifo vya wenzao,huku nikiwasisitiza kuwa nao wajifunze pale madereva wao wanapoendesha kwa kasi au bila kufuata taratibu za usalama,basi wapaze sauti.
Leo wakawa wanauliza,sasa ulisema ajali ni mwendokasi na korongo,mbona huyu anasema ni kafara na majini?Ina maana wamiliki wa hizi shule wanaweza kutufanya sisi kafara?Nimetumia nguvu sana kupangua hoja.
Azam Tv tunawapenda sana,ila msirudie "ujinga" kama wa leo.Muwe mna-hariri habari zenye "majungu" bila uthibitisho,mtasababisha taharuki na chuki miongoni mwa watu.
Asante mleta mada