Azam Tv jirekebisheni katika hili

Azam Tv jirekebisheni katika hili

kakusikitisha sana alafu unacheka
Hujui kucheka kwa dharau?
Unapomuona mtu mzima anaongea na kuamini anachoamini na unamuhutumia/unamsikitikia kwa imani yake potofu

Ulitaka nilie? Unamlilia mwendawazimu na wale watoto waliokufa utafanya nini si utajinyea wewe?
 
Una maana gani kusema kama ni kweli? Kwa nini kama huamini usimuulize mleta taarifa ujue ni kweli au la??
Kwa sababu sikubahatika kuona hivyo pamoja na kuwa mleta mada kahabarisha hivyo,naangalia pande zote kabla ya kufanya hitimisho(conclusion)!
 
Kashaharibu biashara ya mtu Azam TV. Unadhani hapo wazazi wenye imani potofu watapeleka watoto katika hiyo shule? Na wengine watahamishwa
 
Kama ni kweli, Azam wamefanya kosa kubwa sana kuruhusu hilo.
ni kweli mkuu hata mimi nimeona na nikajisikia vibaya hawa azam two wamefanya vibaya tena wamemuacha kwa dakika zaidi ya tatu akisisitiza ni kafara
yaani mtu anasema kabisa eti mkuu wa shule alimkataza mwanaye asiende kwa sababu alijua wanaenda kutoa kafara!!
azam mmeukosea sana uongozi wa shule ile
 
Kwa sababu sikubahatika kuona hivyo pamoja na kuwa mleta mada kahabarisha hivyo,naangalia pande zote kabla ya kufanya hitimisho(conclusion)!
Nadhani sasa baada ya kusoma comments za wengi umeamini kuwa hiyo habari imerushwa na Azam TV.
 
Mungu atusaidie, superstitious people, hata ndege zinanguka killing all on board tuwaombee hao wazazi mungu awape nguvu.
Hata school management and pupils ni wa kuwapa faraja sio kuropoka nonsense mambo ya kafara huo ni upuuzi mtupu.
 
Na Mimi nimesikia nikashangaa kweli...

Mwandishi alitakiwa akate mahojiano baada ya kuona anayehojiwa anatoa habari za kupotosha.

Kusema kuwa inawezekana hao wanafunzi walitolewa kafara na mkuu wa shule ni habari ambazo hazina uthibitisho, na zinaweza kusababisha chuki kutoka kwa wazazi na wananchi kwa jumla.
....Wewe siyo mwanahabari, waache wenyewe watabalance hiyo story, acheni mambo ya kibabe ya kuficha ficha habari, eti angekata mahojiano!! Eboo!!
 
Lakini Yale ni mawazo ya mtoa hoja sio ya Azam TV..mtangazaji alichokifanya ni kuhoji..kwenye kuhoji kila mtu na mawazo yake..nadhani busara ilitakiwa mtangazaji awake msisitizo kwamba bado kuna watu wenye mawazo yakishirikina..akimtolea mfano huyo mzungumzaji wa mwisho masharubu toka kigoma..
 
Hata siku mbili hazijaisha udaku umeanza tena kwenye tv kubwa tu sijui hizi shule walienda kusomea nn
 
Sio kila anachohojiwa mtu kiripotiwe. kuna mtu kahojiwa kuhusiana na ajali ya arusha anasema mkuu wa shule anahusika kisa alimzuiya mwanawe kwenda. sio justification. kuhusisha ajali na kafara kisa hakukuwa na damu ni imani zinazoweza kuhatarisha amani. tuwe makini kwenye kuripoti
Kwani si maoni yake, huwezi kuignore hiyo kitu hasa kwa maisha yetu yaliozidi sana usanii.
 
Sio kila anachohojiwa mtu kiripotiwe. kuna mtu kahojiwa kuhusiana na ajali ya arusha anasema mkuu wa shule anahusika kisa alimzuiya mwanawe kwenda. sio justification. kuhusisha ajali na kafara kisa hakukuwa na damu ni imani zinazoweza kuhatarisha amani. tuwe makini kwenye kuripoti
Kwa kweli hata mimi nimeiona habari hiyo azam tv
Imenisikitisha hasa ukizingatia sheria za nchi yetu hazitambui imani za kishirikina
Habari kama hii inaleta chuki miongoni mwetu
Hapo azam mmekosea
Hope tcra watafanya kazi yao
 
Azam siku hizi wameanza kupoteza weledi kwenye habari zao kwa ujumla
sasa Azam hapo wana kosa gani? inamaana wao ndio walimwambia huyo jamaa atamke hayo aliyoyaogea, au azam walijua akimuhoji ataongea nini?, haya ni yale yale ya mkuu wa kaya kulalamikia Tv zinazoonyesha vita vya wafugaji ..........
La muhimu ni je ni kweli mtoto wa mkuu alizuiwa kwenda???
 
Ndio masna tunasisitiza ukaguzi wa vyeti upite kote hadi makampuni binafsi.
 
ni kweli mkuu hata mimi nimeona na nikajisikia vibaya hawa azam two wamefanya vibaya tena wamemuacha kwa dakika zaidi ya tatu akisisitiza ni kafara
yaani mtu anasema kabisa eti mkuu wa shule alimkataza mwanaye asiende kwa sababu alijua wanaenda kutoa kafara!!
azam mmeukosea sana uongozi wa shule ile

Mi nawaunga mkono Azam. Hata kama utanichukia, poa tu.

Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake, ili mradi asivunje sheria.

Shkamoo Baby shem DEMBA
 
Sioni kosa la Azam TV iwapo kazi yao ni kutuletea habari na mawazo ya wana nnchi kulingana na tukio husika nyie mlitaka kama ya Jecha "VIVA AZAM" kumbe shule zina mengi behind the seen
 
Sio kila anachohojiwa mtu kiripotiwe. kuna mtu kahojiwa kuhusiana na ajali ya arusha anasema mkuu wa shule anahusika kisa alimzuiya mwanawe kwenda. sio justification. kuhusisha ajali na kafara kisa hakukuwa na damu ni imani zinazoweza kuhatarisha amani. tuwe makini kwenye kuripoti
Sijaangaalia kipindi. Nawaza kama Kilikua kinarushwa live najua hapakuwa na jinsi ya kuzuia hicho kitendo ila kama ni recorded lawama ziwe juu yao azam tv.
 
Back
Top Bottom