Azam Tv jirekebisheni katika hili

Azam Tv jirekebisheni katika hili

Boeing

Senior Member
Joined
Apr 16, 2017
Posts
151
Reaction score
422
Sio kila anachohojiwa mtu kiripotiwe. Kuna mtu kahojiwa kuhusiana na ajali ya Arusha anasema mkuu wa shule anahusika kisa alimzuia mwanawe kwenda. Hiyo sio justification.

Kuhusisha ajali na kafara kisa hakukuwa na damu ni imani zinazoweza kuhatarisha amani.

Tuwe makini kwenye kuripoti
 
Na Mimi nimesikia nikashangaa kweli...

Mwandishi alitakiwa akate mahojiano baada ya kuona anayehojiwa anatoa habari za kupotosha.

Kusema kuwa inawezekana hao wanafunzi walitolewa kafara na mkuu wa shule ni habari ambazo hazina uthibitisho, na zinaweza kusababisha chuki kutoka kwa wazazi na wananchi kwa jumla.
 
Na Mimi nimesikia nikashangaa kweli...

Mwandishi alitakiwa akate mahojiano baada ya kuona anayehojiwa anatoa habari za kupotosha.
Kwanza sio live. Kuna editors ilipaswa waedit wamtoe yule jamaa.

Ila amekomaa huyo anasema ni majini au kafara. Kama ni majini hata wangefunga mikanda wangekufa. Halafu yuko serious kabisa yule mzee. Anaonekana sijui mlokole hahaaa
Kanisikitisha sana
 
Ndio tatizo la live a.k.a mubashara
Na Mimi nimesikia nikashangaa kweli...

Mwandishi alitakiwa akate mahojiano baada ya kuona anayehojiwa anatoa habari za kupotosha.

Kusema kuwa inawezekana hao wanafunzi walitolewa kafara na mkuu wa shule ni habari ambazo hazina uthibitisho, na zinaweza kusababisha chuki kutoka kwa wazazi na wananchi kwa jumla.
n
 
Alafu anaongea hear say eti nimesikia mtoto wa mkuu wa shule alizuiliwa kwenda alafu unairusha habari ya namna hiyo
 
Azam siku hizi wameanza kupoteza weledi kwenye habari zao kwa ujumla
 
Aisee mambo kama hayo jamaa aliyohojia akaanza kuropoka si mazuri kabisa AZAM ni chombo cha habari kikubwa wanaangalia watu wengi sana, sasa hii tayari imeingia kwenye ubongo wa wengi na nafikiri wanaanza kuunganisha doti.
 
Mimi siamini katka hayo ,ila huenda yanasemwa sana underground, au simanzi imewachanganya wengi,watu wanajisemea chochote
 
Kwanza sio live. Kuna editors ilipaswa waedit wamtoe yule jamaa.

Ila amekomaa huyo anasema ni majini au kafara. Kama ni majini hata wangefunga mikanda wangekufa. Halafu yuko serious kabisa yule mzee. Anaonekana sijui mlokole hahaaa
Kanisikitisha sana
kakusikitisha sana alafu unacheka
 
Kama ni kweli,AZAM wanatakiwa waombe radhi kabisa umma. Huo ni uchonganishi. I hope wasipoomba radhi mamlaka zichukue hatua kali ikiwemo kuwapa onyo kali/karipio au kupigwa fine. Maneno ya hisia za vijiweni huwez kuviacha viruke hewani. Ovyo kabisa(kama ni kweli).
 
Mimi pia nimestuka sana!!
Yule jamaa na mustachi yake kama Carl Peters kakazana kabisa kuwa eti hiyo ajali ni "kafara" ya mwenye shule,kama sio "kafara" basi ni majini ktk eneo hilo yalikuwa yanataka damu.

Jamaa na mustachi yake kakazana kabisa kuwa eti ndio maana maiti zote hakuna hata moja yenye damu,hii ni kwa sbb maiti za kafara na zile za majini huwa hazitoki damu hata kukiwa na ajali.

Jamaa ana imani kali kweli za ulimwengu wa pili,anasema mmiliki wa shule alimkataza mwanae kwenda katika hiyo ziara,so kwa kumkataza huko inamaanisha kuwa jamaa alijua leo ndio siku ya kafara.

Huyu jamaa aliyehojiwa hakupaswa kurushwa hewani,kwa mfano mimi toka jana...Ikifika taarifa ha habari nakusanya watoto na wajukuu waje waone taarifa za vifo vya wenzao,huku nikiwasisitiza kuwa nao wajifunze pale madereva wao wanapoendesha kwa kasi au bila kufuata taratibu za usalama,basi wapaze sauti.

Leo wakawa wanauliza,sasa ulisema ajali ni mwendokasi na korongo,mbona huyu anasema ni kafara na majini?Ina maana wamiliki wa hizi shule wanaweza kutufanya sisi kafara?Nimetumia nguvu sana kupangua hoja.

Azam Tv tunawapenda sana,ila msirudie "ujinga" kama wa leo.Muwe mna-hariri habari zenye "majungu" bila uthibitisho,mtasababisha taharuki na chuki miongoni mwa watu.

Asante mleta mada
 
Mimi siamini katka hayo ,ila huenda yanasemwa sana underground, au simanzi imewachanganya wengi,watu wanajisemea chochote
Kusemwa chochote ni jambo moja lakini kuripoti chochote ni jambo lingine.
 
Kama hili ni kweli wanapaswa kuomba radhi......
 
Kama ni kweli,AZAM wanatakiwa waombe radhi kabisa umma. Huo ni uchonganishi. I hope wasipoomba radhi mamlaka zichukue hatua kali ikiwemo kuwapa onyo kali/karipio au kupigwa fine. Maneno ya hisia za vijiweni huwez kuviacha viruke hewani. Ovyo kabisa(kama ni kweli).
Una maana gani kusema kama ni kweli? Kwa nini kama huamini usimuulize mleta taarifa ujue ni kweli au la??
 
Back
Top Bottom